nzalendo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 11,726
- 12,006
Kuna umri ukifika ...utaelewa haya yoote uliyoandika si kitu............oa kijana oaa...Habarini,
Mimi ni mtu mzima na nina Akili timamu nimefikia maamuzi ya kutokuja kuoa wala kuwa na moto maisha yangu yote! Sio kwamba sina uwezo wa kuoa lahasha nina uwezo wa kuoa hata wanawake wa 5 na kupata watoto chungu nzima lakini nimekaa nimetafakari sana nimeamua kufikia mamuzi hayo.
Baada ya kuteseka sana na mapenzi ya umri wetu, baada ya kushuhuduia ujinga na usaliti wanao fanya akina dada wa miaka hii, mateso ya kwenye ndoa wanayo yapata watu na adha zingine chungu nzima mimi nimefikia hatua kutotaka kuoa wala kupata mtoto
Nina kazi yangu nzuri tu ambayo naweza kumudu kulea familia hata ya watu 10 lakini kamwe sitokaa kudhubutu kuoa na kuwa na mtoto na sitaki utani katika hili! Nimesh ichosha sana akili yangu katika mapenzi na nimeshuhudia mengi sana katika mapenzi sasa bahati mbaya yote niliyokuwa nayashuhudia ni ya usaliti na mateso katika ndoa na hii inatoka na akili walizonazo dada zetu.
Hivyo sina mda wa kukaa kuchambua kupata huyu anafaa huyu hafai huo mda sina nitahakikisha nafanya kila niwezalo kwa kutumia uwezo wangu wote niwe na maisha mazuri miaka yote! Jasho langu watafaidi wadogo zangu na wazazi wangu, nitapigania kufa na kupona katika kusaka pesa! Katika kumshukuru Mungu kwa pale alipo nifikisha nita adapte mtoto mmoja yatima nitamsomesha na kuishi naye miaka yote tena shule nzuri nitampeleka! Nyumba yangu itakuwa na mfanyakazi mmoja na mtoto mmoja na mimi basi.
Dada yoyote hatadhubutu kuja kwangu kwa namna yoyote ile na wala asijipendekeze kuja kwangu labda awe hana uwezo wa kuzaa ambao hospitalini wamethibitisha ili asije kunikeletea vimimba vya uwongo na ukweli.
Sitaki stress siku hata nikiwa sina hata mia nitaishi kwa amani hakuna wakunisumbua kuliko kuwa na mke sa nne usiku kakuomba hela unamwambia sina mnalala wote sa kumi na mbili asubuhi anakuomba tena hela hivi usiku anadhani alilala peke ake? Mimi nilikuwa kutafuta pesa? Mwisho wa siku mnaishia kugombana na kununiana hiyo mimi hapana sitaki kabisa.
Mwisho haya ni maamuzi binafsi nimeamua kushare nanyi.