Sitarudia kuitetea tena CCM. Nimechoka

..Nimesikitika sana wazalendo wa chama tunaachwa, wanachukuliwa watu ambao hawajui machungu na mateso tuliyoyapata sisi wengine ambao muda mwingine tumepambana kupindisha ukweli ili walau tukumbukwe siku moja.

What makes you think Mama Anna Mghwira sio mwanachama mtiifu wa CCM? Did you even know her kabla ya ACT kuanzishwa/Uchaguzi mkuu was 2015?

Wewe endelea tu kuipigania CCM kwa uaminifu. May be utakumbukwa one of these days. Mzee si alishawaambia muache kugombania fito maana "mavyeo yenyewe yapo mengi tu"
 
Mkuu Hivi Ni Lini Umehama Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo ( CHADEMA ) ???

Mkuu Wewe Sio Ndio Ulitangaza Nia Ya Kugombea Ubunge Jimbo la Karatu Kupitia Chama Chako Pendwa Cha CHADEMA...

Kama Propaganda Zimeisha Basi Jitahidi Kuingia Chimbo Ili Kuleta Propaganda Zenye Mashiko.

Mwenyekiti Wetu Anakula Bata na Sepenga Huku
 
Kumbe mnateteaga pumba za lumumba kasababu ya vyeo !!!! Ila kupotea njia ni mara moja tu,ukipotea mara yapili basi wewe utakuwa mjinga.Heri yako wewe umeokolewa uzezeta na usukule unakutoka.Karibu kwenye mapambano kuikombo nchi kutoka kwa wanyonjaji wa rasilimali zetu ccm.
 
What makes you think Mama Anna Mghwira sio mwanachama mtiifu wa CCM? Did you even know her kabla ya ACT kuanzishwa/Uchaguzi mkuu was 2015?

Wewe endelea tu kuipigania CCM kwa uaminifu. May be utakumbukwa one of these days. Mzee si alishawaambia muache kugombania fito maana "mavyeo yenyewe yapo mengi tu"
Mkuu sasa sisi ndio tunataka tuwekwe wazi na wasemaji wa chama chetu kama ACT ndio Tawi letu lililoko kwa jirani ili tujuane kwa alama.
 
Kitendo hicho kimetusononesha wengi, lakini mwarobaini si kuhama chama - tuendelee kukijenga na kukitumikia kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo wa hali ya juu ili kiendelee kuunda serikali.

Hata wakati wa kampeni zake Mbeya JPM, moja ya ahadi zake ilikuwa kuwapa ajira walioshindwa kura za maoni lkn kinachotokea ni tofauti kabisa. Naamini atafanya masahihisho kwa kuwa CCM kina hazina kubwa.
 
Hata mbuzi akivunjika mguu huludi zizini hamna namna wewe nenda tu mwenda kwao sio mtoro twakutakia maisha mema naona malengo yako hayakuitimia maana unaonyesha ulijibendekeza ili nawe uwe kama Bashite
 
Waosha vinywa wengi wa siasa mitandaoni ni mabaragumu ya wanasiasa na wachumia tumbo tu
 
Wanabodi habari za jioni,Poleni sana na Majukumu

Awali ya yote naomba kudeclear interest, mimi ni CCM , Damu yangu ya kijani kibichi kabisa, mzalendo wa hali ya juu.

Najitokeza rasmi mbele yenu leo hii kuonesha hisia zangu kuhusu uteuzi wa Mh. Anna ambae ni Mwenyekiti na Chama cha upinzani.
Nimesikitika sana, nimenyong'onyea sana, nimejisikia vibaya mno.
Nimekuwa nikifanya vema kazi za chama changu cha CCM kwa ufanisi wa hali ya juu na uzalendo, nimekuwa nikipambana na kila anaejaribu kukashfu chama changu ama kiongozi wangu hasa Rais wetu Mtukufu , nimepambana pia muda mwingine kupindisha hata ukweli ili mradi tu chama kisipate kashfa yeyote. Nimefanya kazi hii kwenye mitandao yote ya kijamii, nimepambana vilivyo na mtu anaeitwa Mange Kimambi kwenye mtambo wa Instagram, hii yote ni kwa sababu ya kulinda chama ili chama nacho kinilinde.

Nimesikitika sana wazalendo wa chama tunaachwa, wanachukuliwa watu ambao hawajui machungu na mateso tuliyoyapata sisi wengine ambao muda mwingine tumepambana kupindisha ukweli ili walau tukumbukwe siku moja.
Nimejiuliza sana, huyu mama kipindi cha kampeni alinadi sera zake, sisi tulinadi pia sera zetu, leo hii anaenda kutekeleza ilani ya chama ipi?? Otherwise tunaomba viongozi wetu watuweke wazi kama hawa walikuwa mapacha wetu ama walikuwa sehemu ya mkakati wetu kudhoofisha wapinzani wetu kipindi hicho.
BTW,
Mimi ni mtu mwenye vyeti vyangu halali , sina waswasi wowote , nimeachwa , Mheshimiwa katika hili amenisikitisha sana, sasa naangalia utaratibu mwingine, vijana wenzangu wa upinzani nakuja mtaani naomba msinitenge, nimechoka kuitesa dhamira yangu.

Najiunga rasmi na nyie wazalendo wenzangu, naomba mnipokee .....

Wasalaam!!!!!!!
Kujiunga na kutetea chama si kigezo cha kupewa cheo
 
Mkuu hata wewe dhamira inakusuta kwa kutetea hicho ulichotolea povu. Ondoka huko nyumba ya laana hiyo

Eeeeh povu tena!!! Ukweli ndio huo

Nyumba ipi unaongelea ya laana?

Hii ni awamu ya tano, inaelekea nyie wenyewe mlijilemaza humo kwenye chama chenu. Hivi mlizoeaje na kivipi kabla ya hii awamu? Vyeo mliomba au?

Uko unaposema umekuwa unatetea chama, ulitumia jina lako au la feki?

Na nini haswa unaona labda ungefaa kuwa RC, kivipi? Raisi anakufahamu kuwa upo CCM na unatetea mitandaoni?
 
Hakika ukitaka kuteuliwa ndani ya chichi em,unapaswa kuanzia kwenye upinzani,uwaponde CCM weeee then baadaye jiunge nao,kila kitu kitaenda sawa,tazama MTELA MWAMPAMBA,baada ya kuenguliwa CHADEMA alijiunga na CCM,muda fupi baadaye akaula,na sasa ni katibu tawala wilaya moja ya jijini kwa ZIRO BRAIN!!!

JULIANA SHONZA alikuwa CHADEMA,baad ya kutemwa akajiunga na CHICHI EM,muda mfupi baadaye akaula,na sasa ni mbunge wa viti maalum,anahesabu posho za vikao na marupurupu lukuki!!!

Na wengine weeeengi wa aina hiyo,kwa hiyo vijana wa ndani ya CHAMA sisi kazi yetu ni moja tu,kukitetea chama kwa nguvu zetu zote,lakini kwenye uteuzi hatufikiriwi mpaka wenyewe wapende!!
 
Back
Top Bottom