Wakati nikifungua akaunti hii nilikuwa na furaha sana tena sana kwani niliona hakika Taifa linaenda kuongozwa na brain. Ukiangalia tarehe ya kuanza kwa akaunti hii na tukio lililokuwepo wakati huo utanielewa vizuri. Kwangu SSH ni brain hata katika Bunge la Katiba alionesha hilo na alikuwa very very very rational katika kuongoza kwake.
Ninajiuliza kila siku ni kitu gani kimempata huyu Rais wangu, anaogopa nini? Kwani kadri anavyoogopa na kukubali na kushauriwa na watu ambao hawako vizuri kichwani basi NIMECHOKA KABISA. Eti Amos Makala anawananga wapinzani na kusema wazi kuwa CCM wana fedha. Hivi kweli jamani tunatambia fedha. Mpaka kusingizia CHADEMA kuleta maambukizi ya magonjwa, hivi kweli tumekwa watupu hivyo vichwani mwetu. Amos Makala hivi wewe kweli ni CPA wewe! Du! Nchimbi mwenyewe amekuwa bendera fuata upepo, hana lolote na hata speech zake hazivutii kusikiliza. Mbaya zaidi hamna msafi CCM, akina Mwigulu Mchengerwa, wote wachafu tu. Wezi wa Uchaguzi hawa. Tunawaona na Mwenyezi Mungu wetu anawaona. Wanatuchafulia sana Chama chetu!
Mpaka sasa nina uhakika tunaharibu sana, tunaweka doa kubwa sana ndani ya Chama chetu. Chama chetu CCM kinaonesha udhaifu wa hali ya juu. This time nina uhakika hata mabango ya picha za Mgombea wetu baadhi ya sehemu yatachomwa moto na baadhi ya sehemu CCM wanaweza kudhuriwa sana. Wananchi wameshajaa chuki, wanasubiri mtu mmoja tu auwawe ili waingie mtaani. Rais wangu epusha kifo hata cha mtu mmoja pls, toa maelekezo kwa kutumia vyomba vyako hali irekebishwe. Tume ya Uchaguzi kufanya marejeo ya Kanuni na kuzifanya ziwe nzuri ni siku moja tu. Tafadhali SSH epusha chuki inayojengeka hapa Tanzania. TAMKA NENO RAIS WANGU.
Binafsi ni CCM hasa lakini ninaona aibu kwa tunayotenda. Kailima atakuja kuwa kama yule bwana wa Kenya au Jecha siku za usoni. Watoto wa Kailima wataishije huko baadaya wakichangamana na WaTanzania hawa kama vitu vya wazi kabisa anashindwa kuvisimamia. Hivi kweli tumekosa kabisa ujasiri wa kusimama katika Uchaguzi wa Haki JAMANI.
Ninajisikia vibaya sana sana. Nafsi yangu inanisuta sana, sishiriki siasa lakini iwapo CCM itaendelea hivi, nitashiriki siasa za wazi na ni kweli kabisa nitahamia CHADEMA hata kama hakitashiriki Uchaguzi huu. CHADEMA wanasimamia mambo ya kweli ambayo yakizingatiwa basi nchi yetu haitakuja kukumbwa na lawama kuwa sio ya kidemokrasia. CCM yangu mbele yake ni giza tena giza nene, sababu tu ya KUVIMBIWA MADARAKA.
TUTAKUFA VIBAYA SANA kwa sababu ya kunyonga demokrasia. YANGU MACHO!