hata mimi
JF-Expert Member
- Oct 17, 2017
- 1,356
- 1,442
Ukiwa shuleni unafundishwa michezo mingi sana (kwenye Masomo ya "Maarifa ya Jamii" mfano Stadi za Kazi na Haiba na Michezo)
Michezo hiyo imegawanywa katika namna mbili yaani michezo isiyo ya asili na michezo ya asili
Michezo isiyo ya asili inajumuisha michezo ya kisasa iliyobuniwa karibuni na michezo mingine yote ya asili ya watu wengine yaani ambayo haikwepo kwenye jamii zetu bali imefanya kuletwa tu mfano aina zote za michezo ya mpira, drafti, karata, dart nk
Michezo ya asili ni michezo yote ambayo imekuwa ikichezwa na jamii zetu tangu enzi na enzi. Mfano wa michezo hiyo ni bao, shabaha, rede, mieleka, simba ni mkali, ukuti ukuti, ulinge bayoyo, kombolela, mbio, kuvuta kamba, kukamata kuku nk
Binafsi huwa nikichunguza nagundua hata hiyo michezo tunayoaminishwa ni ya kwetu ya asili, siyo kweli! Hii inatokana kwamba namna ya uchezaji wa michezo hiyo kuna viashiria vingi kabisa kudokeza ni michezo ya watu tumecopy halafu tukapaste kisha kwa baadhi ya michezo tukainstall kabisa
Nitatoa mifano kadhaa:
Kuna mchezo wa kita/ kipande/ kinato (kila watu wana jina lao ila itoshe kusema tu kwamba ni mchezo wa kucheza kwa kigae kidogo kwa mguu mmoja kwenye vyumba vilivyochorwa chini)
Katika mchezo huo kuna stage ikifika mchezaji anafunga macho huku anaruka katika vile vyumba akiuliza "maraiti" akipatia wanajibu "yesi" akikosea wanasema "no". Tukienda kwenye ukweli wa maneno hayo ni kwamba unauliza "I'm I right?" Yaani je niko sahihi na ndomana wanajibu yes-ndiyo au no-hapana. Wewe na mimi tujiulize watoto wa wazee (mababu) wetu walishindwa kuulizana kwa lugha zao hapo?
Mchezo mwingine ni hii rede ambapo wakati wa kucheza akipatwa mtu na dharura anaomba kusitisha mchezo kwa muda kisha ikiisha anaruhusu mchezo uendelee kwa kusema rede. Ready yaani tayari ndio iliyotoa jina kwa mchezo huo. Pia kwenye rede kunatumika maneno kama stop nk
Michezo ya bao, ulinge bayoyo na kombolela pia kuna uzungu ndani yake. Michezo mingine kuna uchina na uhindi mfano drafti tombora na chess.
Muda mwingine huwa nahisi huenda Waafrika walikuwa wakijishughulisha sana na uzalishaji kiasi kwamba labda kipindi hiko (wao wazungu wakibuni michezo) Waafrika walikuwa zao bize kufanya shughuli za uwindaji urinaji uvuvi na shughuli nyingine za kiuchumi.
Yaani ukichimba utakuta mwafrika alikuwa na michezo yake kadhaa tu aliyofanya tena nayo ilikuja kuingiliwa ikabadilika mfano mieleka na shabaha. Dah! Sijui walitufanyaje hata hawa jamaa.
Swali: Muafrika michezo yake halisi ya asili ni ipi?