Siri Ya Mtungi.

jouneGwalu

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,687
1,782
"Siri ya Mtungi" ni tamthilia ya televisheni inayofurahisha, inayoonyesha maisha ya Cheche, mpigapicha mwenye bashasha na mmiliki wa Studio ya Kupiga Picha ya Mtungi. Ana mke mrembo, Cheusi, aliyemzalia watoto wawili wenye afya na huku akiwa na ujauzito wa mtoto wa tatu.

kizito-family.jpg

Cheche anampenda sana mkewe, lakini mawazo ya kuanzisha biashara mpya na kuwepo ujio wa mtoto mwingine wa tatu yanawapa wakati mgumu. Anajaribu kuwa baba mwema, lakini, kama ni uchawi au bahati tu, anawavutia sana wanawake…na wale makahaba! Cheche pia ana uhusiano wa karibu na mpenzi wake wa shuleni, Tula.

cheche-mtungi.jpg

Kizito, ni baba mkwe wake Cheche, aliyemsaidia kuanzisha biashara yake. Ni mtu anayeheshimika sana katika jamii ya Bagamoyo na kila mara anashughulika na watoto wake Nuru na Matona katika karakana yake ya magari. Pamoja na hayo, Kizito ana watoto wengine wengi aliozaa na wake zake watatu, Farida, Mwanaidi na Vingawaje, aliyefariki hivi karibuni.

Mhalifu wa mjini ni Masharubu, tajiri mwenye nguvu anayemiliki mabanda na biashara za kitapeli. Baada ya kuvumilia matusi kwa muda mrefu, mkewe alimkimbia na kumwachia binti yao mrembo, Nusura. Nusura ni ua la yungiyungi lililochanua kwenye lile geto. Ni mjanja, mwanamke shupavu ambaye udhaifu wake ni mahusiano yake na Duma, mmoja wa wapangaji wa Masharubu. Duma ana moyo wa dhahabu lakini anahangaika kimaisha

kama DJ mjini Bagamoyo.Karibuni tu alimleta mdogo wake, Stephen, toka kijijini, ili mvulana huyo aingie shule ya kujitegemea na kupata fursa ya maisha bora lakini, mpaka muda huu Duma anashindwa kumtimizia mahitaji muhimu. Muhimu zaidi, Duma anashindwa kuwa mfano bora kwa mdogo wake, Stephen anayechoshwa na shule na kutaka kuwa ‘mtoto wa mjini' kama kaka yake.

duma-door.jpg
nusura-vert.jpg
kizito-vert.jpg

Nyendo za Nusura na Kizito zinapishana kuashiria bahati kwa Kizito, ambaye yuko tayari kuendelea mbele na maisha yake kufuatia kifo cha mkewe mdogo. Nusura kwa upande wake amechoshwa na wasiwasi katika mahusiano yake na Duma, hivyo yuko tayari kwa mambo ya kiungwana zaidi. Nusura anajikuta yuko njia panda kati ya penzi la Duma na lile lililotulia kama maji lenye uelekeo wa ndoa na Kizito. Hana ufahamu wowote kuwa kuna dhoruba inayochemka katika maji yale ya samawati. Siri zitasimuliwa, maisha kuchanwachanwa na mioyo kuvunjwa kwenye mji huu wa Bagamoyo.

‘Siri ya Mtungi' imetayarishwa na MFDI Tanzania ikishirikiana na JHUCCP Tanzania kwa msaada wa Wau wa Marekani kupitia USAID.

character-bottom.jpg
 
Ninaweza kusema kuwa hizi ni miongoni mwa kazi kubwa ambazo zinathibitisha kuwa wasanii wetu wakipata mtaji wanaweza sana na tuna hazina kubwa ya wasanii kuliko hawa ambao tunaaminishwa wa "bongo movie".....

Ila ni bahati mbaya kuwa kazi hizi huwa hazipeperushwi na kasuku wetu na hivyo inaenedelea kuaminika kuwa bongo movie ndio mwisho wa uwezo wetu!
Bishop Hiluka, unaizungumziaje hii kazi?
 
Last edited by a moderator:
Ni tamthilia? ipo station gani na inarushwa siku gani?

Yap, ni tamthiliya ya Kitanzania, inarushwa ITV siku ya Jumapili baada ya Kipindi cha Mizengwe.

Pia huwa inaonyeshwa EATV siku ya Jumatano saa 9:30 Usiku....

Iwahi keshokutwa EATV utaikuta Episode ya 4.

Nisamehe sikuweka timing huku kwangu mtandao unanisumbua sana hata nikatuma bila kukamilisha baadhi ya taarifa!
 
ahsante sana, nitajitahidi kufuatilia, ingawa wabongo walio wengi wanaigiza kuigiza, mara nyingi niko selective sana kwenye hizi tamthilia zetu, nikiona longolongo huwa siendelei kabisa, ngoja nijaribu hii
 
Aine tembelea hapa Siri ya Mtungi..
Nadhani utaelewa kwanini mpaka nimeianzishia thread yake hapa JF.
Hiyo sio tamthiliya ya kipuuzi kama hizi maigizo za madogo ambao hawajui hata sanaa ni nini.
Ndio maana nikasema ni kazi kubwa kwani inahusisha team ya wafadhili na team ya watu wenye vipaji huku kila mtu akionyesha kulijua eneo lake.
Ni vitu ambavyo huwa vinatokea mara moja moja sana kwenye medani zauigizaji hapa kwetu na baadhi ya nchi za barani Afrika.
Kama wewe ni mpenzi wa sanaa kwa ujumla hautaangushwa na kazi hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Niliwahi kuangalia mara moja sikuimaliza haifai kuangalia na watoto kwani inakiuka maadili ya kitanzania mambo ya ngono hayajafanyiwa editing inayostahili ni tamthiliya ya waigizaji wa kitanzania iliyorekodiwa Tanzania yenye maudhui ya kimagharibi
 
Mkuu uliona nini? Mbona mi naiangalia na family hapa home kila inapoonyeshwa.....
Hii tamthiliya inafasili maisha ya watu wa Pwani, na imeigiziwa Bagamoyo na tabia za mule ni za watu wa Pwani hasa sijui huo umagharibi unaousema wewe ni upi!
Ndio maana hata Monalisa ambaye kwenye hii anaitwa Lulu ametokea kwa mara ya kwanza akiwa na nguo nzuri za vitenge na bado ulimbwende wake ulikuwa bayana.

Nadhani wabongo tunamtazamo mbovu na kitu kinachoitwa ngono na inatupa wakati mgumu sana kuiwakilisha kisanii kwa ufuatiliaji wangu wa movie za kiafrika naona hawa jamaa wamejitahidi sana kwenye hilo eneo japo tatizo litabakia kwa watu kama nyie mnaodhani suala la mapenzi ni la wamagharibi tu.
 
Picha za Familia - Siri ya Mtungi

Published on 7 Dec 2012Siri ya Mtungi ni tamthilia ya televisheni inayofurahisha, inayoonyesha maisha ya Cheche, mpigapicha mwenye bashasha na mmiliki wa Studio ya Kupiga Picha ya Mtungi. Ana mke mrembo, Cheusi, aliyemzalia watoto wawili wenye afya na huku akiwa na ujauzito wa mtoto wa tatu.

Shoti anampenda msichana ambaye anakuja kupiga picha kwenye studio ya Mtungi.

:israel:video zote hisani ya swahiliwood wa youtube
 
Last edited by a moderator:
kuna sehemu jamaa alikuwa anaingia na demu wake kufanya mapenzi kitendo cha kuingia humo kilitosha kuonyesha watu wanafanya nini lakini walianza kuonyesha mpaka wanavuana nguo nilikuwa na watoto ikabidi niamishie sehemu nyingine na ukichukulia muda ni saa 3 na nusu usiku hiyo ilikuwa sehemu ya kwanza kabisa tangia hapo nimeacha kuangalia
 
hahahahaha Mkuu rodrick alexander acha hizo bwana, mbona hakukuwa na kuvuana nguo bwana hebu cheki hizo clip ametuwekea Mkuu bagamoyo hapo afu sema huo uchafu upo wapi Mkuu....

Ipo hivi, ngono ni kitu ambacho kipo na kwenye simulizi lolote kama limehusisha hicho kitu ni vizuri kuwasilishwa kwa namna fulani yenye usawazo katika kuzingatia mazingira husika ya jamii husika, waafrika tumekuwa wasiri mno katika mambo haya ndio maana hata watu waki-kiss tu utaona familia mnatizamana machoni lol

Hiyo part unayoisema ni pale Cheche alimpeleka Tula kumuonyesha studio yake mpya, walipofika chumba cha kusafishia picha Cheche akamvuta Tula kimahaba na kuchokoza huku Tula akijileta kuneng'eneka basi ikawa imekatwa ila watu wazima tukawa tushaelewa nini kiliendelea, mbona hapo hamna chochote cha ajabu sana.

Ila ukipata nafasi iangalie tena kidogo wiki hii tena kesho Jtano EATV mida hiyo hiyo......
 
Last edited by a moderator:
Picha za Familia - Siri ya Mtungi

Published on 7 Dec 2012Siri ya Mtungi ni tamthilia ya televisheni inayofurahisha, inayoonyesha maisha ya Cheche, mpigapicha mwenye bashasha na mmiliki wa Studio ya Kupiga Picha ya Mtungi. Ana mke mrembo, Cheusi, aliyemzalia watoto wawili wenye afya na huku akiwa na ujauzito wa mtoto wa tatu.

Mkuu bagamoyo safi sana pia nashukuru mno kwa kuweka vipande hivi.

Sikufikiria kwenda youtube kuzicheki, nilidhani ningeifanya thread ndefu sana, ila ulivyoweka hapo wewe imekuwa poa zaidi kwa kutanua nilichokiweka awali.....!

Hicho kipande cha Shoti kumpenda binti wa mteja kilinichekesha sana pale alipomtia kofi Cheche eti utani wakati lilikuwa kofi la ukweli la uso, Cheche akaondoka kwenda kupumzika!
 
Last edited by a moderator:
Ninaweza kusema kuwa hizi ni miongoni mwa kazi kubwa ambazo zinathibitisha kuwa wasanii wetu wakipata mtaji wanaweza sana na tuna hazina kubwa ya wasanii kuliko hawa ambao tunaaminishwa wa "bongo movie".....

Ila ni bahati mbaya kuwa kazi hizi huwa hazipeperushwi na kasuku wetu na hivyo inaenedelea kuaminika kuwa bongo movie ndio mwisho wa uwezo wetu!
Bishop Hiluka, unaizungumziaje hii kazi?

Ni kweli mkuu, wengi wanaamini kwenye kipaji na kusahau elimu,
kwa kweli shule ni muhimu ili kuijua misingi ya utengenezaji kazi...
 
Ni kweli mkuu, wengi wanaamini kwenye kipaji na kusahau elimu,
kwa kweli shule ni muhimu ili kuijua misingi ya utengenezaji kazi...

Mkuu ulikuwa wa kwanza kuniletea stori za Swahiliwood hapa jamvi, ila sijui kwanini hukuleta habari njema kama hii.....

Vipi jamaa kuna vitu walikuzingua??

Kupitia mifano kama hii ya Siri ya Mtungi, nilidhani kazi yako ya kuwaelimisha watu juu ya Filamu Bora ilitakiwa iwe nyepesi sana....!
 
Siri ya Mtungi ni bonge la tamthilia imekaa kitanzania zaidi maisha ya pwani hamna ya kuigiza ya wazungu naipenda sana imerudisha hamu ya kuangalia kazi za nyumbani
 
Siri ya Mtungi ni bonge la tamthilia imekaa kitanzania zaidi maisha ya pwani hamna ya kuigiza ya wazungu naipenda sana imerudisha hamu ya kuangalia kazi za nyumbani

Dah Mkuu umeongea sentensi fupi ila inabeba ombwe ambalo limekuwepo kwa mda mrefu sana kwenye tasnia ya uigizaji.

Mi nilipoiona mwanzoni nilipata msisimko ambao niliwahi kuupata mwanzoni wakati wa Tamthiliya ya Tausi ila nayo mwishoni iliharibika tu.

Muhusika gani amekusisimua mpaka sasa??

Binafsi Mzee Kizito amenifurahisha sana, amenifundisha namna mpya ya kudeal na warembo lol....

94d43e327d9303539cb1e2aac7032668_L.jpg
 
Mkuu bagamoyo safi sana pia nashukuru mno kwa kuweka vipande hivi.

Sikufikiria kwenda youtube kuzicheki, nilidhani ningeifanya thread ndefu sana, ila ulivyoweka hapo wewe imekuwa poa zaidi kwa kutanua nilichokiweka awali.....!

Hicho kipande cha Shoti kumpenda binti wa mteja kilinichekesha sana pale alipomtia kofi Cheche eti utani wakati lilikuwa kofi la ukweli la uso, Cheche akaondoka kwenda kupumzika!

Mkuu JouneGwelu,
Ni kweli mkuu, mie nikiona naweza kuongezea kitu ktk thread ya Mwana JamiiForums huweka kuliko kuanzisha thread nyingine yenye suala/mada hiyohiyo kwa faida ya wasomaji wa Jamiiforums kupata habari toka posti moja ya thread.
 
Pamoja sana Mkuu....

Ngoja nikupe zawadi hii ya Mwaka Mpya....

d61d44254608dd06ccdd2ff02982d14d_L.jpg

Mtoto Nusura....

Shindana na Duma na Mzee Kizito kubeba mtoto huyo lol
 
Mkuu ulikuwa wa kwanza kuniletea stori za Swahiliwood hapa jamvi, ila sijui kwanini hukuleta habari njema kama hii.....
Vipi jamaa kuna vitu walikuzingua??
Kupitia mifano kama hii ya Siri ya Mtungi, nilidhani kazi yako ya kuwaelimisha watu juu ya Filamu Bora ilitakiwa iwe nyepesi sana....!

Hahahahaaaaaaa!... Ni kweli tulifika sehemu tukazinguana, hata hivyo
wiki hiyo hiyo nikapata kazi nyingine kutoka kwenye taasisi moja ya Canada
ambapo nililazimika kusafiri kwenda kutengeneza documentary ambayo ilinichukua
takriban miezi mitatu.

Kuhusiana na kazi hii ya 'Siri ya Mtungi' panapo majaaliwa nitaandika
makala maalum ikiwa kama somo maalum kwa watengeneza filamu wetu...
 
Sijawahi kupata muda kuitazama tamthilia hii lakini kwa kuona vionjo humu ndani imenipa mzuka niitafute!
 
Back
Top Bottom