Siri ya kuwa huru kwenye ndoa

Na kwa mwanamke fanya the same. Usimuulize anarudi saw ngapi wala usinune, ILA na wewe pitia bar na mashosti, kasalimie aunt zako WA mbagala Rudi saa sits usiku. Yeye mwenyeewe ndo ataanzisha mazungumzo ya kuwahi kurudi.

ivi ni kwann siku izi wanawake wanapenda kuwa even? ukifanya hivi na mimi nafanya afu tuone sasa. ivi haiwezekani mwanamke kumkera mmewe kwa njia tofauti na kulipiza kilekile alichofanya? Lets say nimerudi saaa nane kwani lazima na wewe urudi saa nane? Mi naona inakuwa poa kama mwanamke nae akamkera mumewe akiwa kwenye anga zake. yani mwanaume harudi saa nane kumkomesha mkewe it happens naturally. ila mkewe analipiza alichofanya mumewe.
 
ni vigumu sana kuwa ndani ya ndoa na kupata uhuru wa kibachela. lazima uchague moja uoe na ubaki umefungwa pingu za maisha. au usioe uendelee kula ujana(nimekumbuka ney wa mitego anakula ujana)

mbona mimi sijaoa lakini sirudi kwangu saa kumi na moja?weekend chache sana naweza kurudi saa saba/nane. watu wengine hawakui,ushaoa bado unataka uishi kama teenager ushamba huo!!!
 
Mkuu utaratibu huo utakugharimu hasa pale utakapopata matatizo,kila mtu atasema ni kawaida yake mpaka utakapokutwa kwenye mtaro umeishaoza.
Binafsi niko huru,na mke wangu yuko huru kwa sababu tumejiwekea utaratibu wa kurudi nyumbani pindi unapomaliza lile lililokufanya utoke nyumbani,ukichelewa ukirudi unamwambia mwenzio kilichokufanya uchelewe kupita muda wa kawaida uliozoea kurudi.
Pia naamini kuulizwa na mwenzio kwa nini umechelewa kurudi ,siamini kama ni swali la shari,maana wakati mwingine huishia na kupewa pole kama unaistahili hiyo pole,na aliyeulizwa kama alikuwa sehemu salama kwa nini awe na kigugumizi kujibu hili swali?
Style ya mleta uzi naifananisha na ile ya IGA UFE.
 
Ukweli sijawahi tamani ndoa, na sitakuja niishi Ktk ndoa, bora kuwa km jlo, maisha ya ndoa ni kichefuchefu hasa ukutane na mme/mke asiye muelewa km huyo mtoa mada hapo juu...

Tukubaliane kutokukubaliana inatoooosha
Mara nyingi viapo kama hivi vina background! Dont be offended pls
 
Mmmmmmmmmmh!!!!!!!!!!!!

Kwenye kurudi mda anaotaka My Mdingi is a PRO! Trust me when i tell you hata akirudi asubuhi hamna kesi.

He just uses a SIMPLE TECHNIC!!!!!!!!!! Na hii technic ni timelss anaiumia since the dark 1985 to digital 2014.
Anachofanya anaoa taarifa tu, leo nitachelewa siji nitarudi saa ngapi ila nitakuwa Pub flani na mzee falani, na flani tunakunywa na kudiscuss mamboe ya kiume." ukiona huniamini mda wowote njoo unichngulie au tuma mtu, usiponikuta ndo uanze kurap. Ukinikuta wahi kulala ila uwahi kufungua mlango. N dont get any funny ideas kuwa nitaanza kondoka kabla ya wenzangu, hilo litakuwa gumu, let it be remembered mimi ndo NIMEKUOA! And let it stay that way. Ukiona hupati usngizi unakaribishwa kunywa meza ya jirani. Hahaaaaa.

Simple like that. Vijana wa siku hizi mnawekewa ngumu kuchelewa kwanza MMEOLEWA na wake zenu, pili ambiguity nyingi sanaa unachelewa wapi. Ila ukiweka wazi unachelewa wapi na kwa nini maisha simple sanaaaaaaaaaaaa!

Unadhani hiyo ilikuwa fair kwa mama yako? Baba yako ni bonge la selfish. How on earth can you make your wife a watchman just because of alcohol? Kama ingekuwa ni shughuli ya kipato, inaeleweka but kunywa, aah No!
 
Ukweli sijawahi tamani ndoa, na sitakuja niishi Ktk ndoa, bora kuwa km jlo, maisha ya ndoa ni kichefuchefu hasa ukutane na mme/mke asiye muelewa km huyo mtoa mada hapo juu...

Tukubaliane kutokukubaliana inatoooosha
Kama ni kwasababu ya negativity kama hizi sikubaliani na wewe;
1. jitathimini wewe binafsi ukoje,
2. tathmini ni vitu gani hupendi mtu afanye kwako (akufanyi), vitu gani unapenda afanye,
3. wewe unafanya vile unavyopenda tu? vile ambavyo hupendi kufanyiwa, wewe humfanyii mwingine?
4. kwa dini zote ukikuomba Mungu anakuongoza mahali sahihi!
Kukana ndoa maanake unakana hata uzao, kwahiyo unajikana pia.
Ni comlex, we have to solve accordingly
usikane ndoa mkimbizi toka tz
 
Last edited by a moderator:
Ni mtazamo tuu
Kila mtu anapenda kuwa huru na maamzi yake mahali popote pale iwe kwenye ndoa, kazini n.k....
Shida ni kutoa uhuru kwa mtu mwingine mfano kumruhusu mke/mme kurudi nyumbani muda anaotaka!
Kwa wanaume, ukitaka kuwa huru usiulizwe ulizwe maswali ulikuwa wapi na nani au mke ananuna nuna! baada ya kumuoa ndani ya siku tatu za mwanzo wa maisha ya ndoa hasa siku ya kwanza nenda kapige story kitaa rudi saa nane, kesho yake wahi mapema. Siku inayofuata rudi saa sita, kesho yake rudi saa kumi na moja, siku inayofuata rudi asubuhi, kesho yake rudi mapema, namaanisha kuchelewa iwe jadi yako mzee hutakuwa unauluzwa ulizwa na utakuwa huru kinoma!
Namaanisha kwa wale wanao taka uhuru katika ndoa zao nje nahapo kama ulianza na A wanataka umalize na A, Hii ni kwa wale ambao hawajaoa ili wakiingia wa-practice! uliyeoa don't try in ur marriage itakula kwako!!!!!!!!!
 
Mmmmmmmmmmh!!!!!!!!!!!!

Kwenye kurudi mda anaotaka My Mdingi is a PRO! Trust me when i tell you hata akirudi asubuhi hamna kesi.

He just uses a SIMPLE TECHNIC!!!!!!!!!! Na hii technic ni timelss anaiumia since the dark 1985 to digital 2014.
Anachofanya anaoa taarifa tu, leo nitachelewa siji nitarudi saa ngapi ila nitakuwa Pub flani na mzee falani, na flani tunakunywa na kudiscuss mamboe ya kiume." ukiona huniamini mda wowote njoo unichngulie au tuma mtu, usiponikuta ndo uanze kurap. Ukinikuta wahi kulala ila uwahi kufungua mlango. N dont get any funny ideas kuwa nitaanza kondoka kabla ya wenzangu, hilo litakuwa gumu, let it be remembered mimi ndo NIMEKUOA! And let it stay that way. Ukiona hupati usngizi unakaribishwa kunywa meza ya jirani. Hahaaaaa.

Simple like that. Vijana wa siku hizi mnawekewa ngumu kuchelewa kwanza MMEOLEWA na wake zenu, pili ambiguity nyingi sanaa unachelewa wapi. Ila ukiweka wazi unachelewa wapi na kwa nini maisha simple sanaaaaaaaaaaaa!
Exactily lara 1 muhimu ni taarifana usiwe muongo hata kidogo (yaan being honest to your wife and to yourself). mie nina rafiki yangu kanizid kama 5yrs hici. ana mke na mtoto (mie bado sijaoa) yaan bado tunazunguka nae starehe zote kama alivokuwa bachellor.

tunaenda kula nyama, tunapiga pombe na ikifika saa 6 usiku tunazama club na hom kwake anarudi saa 11 asbuhi na anafunguliwa mlango anala.

kwanza kabisa anaomba ruhusa kw mkewe kutoka na sisi, na akikataliwa hatoki ng'o hata uje wa crane humtoi nyumbani kwake, akikubaliwa sasa tukatoka kila hatua anamjulisha mkewe.., utasikia mama j ndo tunatoka kimara saiv, mara ama j ndo tumefika sinza tunaelekea bills, nk..nk..

so ni makubaliano yenu tu, ila la mhimu ni kutoa taarifa na uwe mkweli haswaaaa.
 
Mme wa dada yangu alikuwa na rafiki kama wewe,dada alikuwa anamchukia usiombe kusikia,kama na wewe ulikuwa hujui naomba nikujulishe kuwa huo urafiki wa kumchukua mme wa mtu mnarudi saa kumi na moja asubuhi bila kwenda na mkewe,usidhani huyu shemeji yako anaifuraia tabia hiyo,ni basi tu hana la kufanya.
Wadau wameshauri kama unaona bado unapenda viwanja,usioe kuumiza watoto wa watu,ukiona viwanja vyote umemaliza oa.Nami niongezee kuwa mabachera waende viwanja na mabachera wenzao ili kunusuru ndoa za waliokwisha oa zikae kwa amani.
 
Nimekuwa na uhusiano niseme km mchumba au mpenzi ndani ya miaka 12, tumejaliwa watoto wawili, wakike na kiume, maisha niliyoishi na huyo mtu km sio uvumilivu basi sina Jina la kulipatia sahihi, kwanza ni vile
Nilizaa nae nikawa naogopa sana kutengana nae, na yeye alitumia huo udhaifu wangu ipasavyo, mbinfsi, mnafki, mchoyo, kiburi Yaani wkt mwingine mwanamke
/mwanaume ukiishi na mtu wa namna hii ata unatamani ufanye jambo baya iLi maisha yako yawe na amani, ndugu zangu walinionea huruma
Sana, ila kwakuwa nilikuwa naogopa sana kuwatenga wanangu na baba Yao wakiwa wadogo, na kuanza uhusiano mwingine ambao sijawahi ujua pia, nilivumilia sana, anapokosea kitu mfano umemfumania na mwanamke au umeona kurudi kwake usiku wa manane sio sahihi ukamweleza kwa upole sio tabia njema kunitendea hivyo na watoto wanaona unachokifanya, atakujibu kwani nimekuoa, si tumezaa tu!! Unaweza kuendelea na maisha yako ukiona nakusumbua na "maisha yangu" well mi ni mwombaji sana, nilimuomba sana Mungu anipe nguvu ya kutojali hayo, nilipata chuo uk na nikaja kusoma hapa miaka 2, nikamuacha na watoto ! Akaona watoto wanamsumbua sana kuwa huru atakavyo, akawapeleka kwa mama yangu, mara Ampeleke pesa za matunzo mara aseme kwani huyo wa ulaya kazi yake
Nini uko, atume yeye, Ukweli Mungu alinipa neema ya ajabu , nikaanza kufanya vibarua hapa ulaya na shule pia, baadae nikaomba wanangu waje kunitembelea, walipoingia tu , nikaomba kuongeza muda wa kusoma , wkt huo haukuwa ngumu km sasa , kwahiyo hata watoto wangu waliweza kubaki na kuanza shule hapa uk. Nilipomaliza shule yangu nikapata kazi hapa uk , Ukweli nimeuona mkono wa Mungu ,wanangu sasa wako university na wanafanya vizuri sana, hutanielewa kabisa Nilikuambia sijawahi tena jiingiza kwenye mahusiano na mwanaume
Kwanza kwa uoga,
Pili maumivu niliyo pitia?tatu wanangu bado wananijihitaji kuliko yeyote Yule duniani? Sio kwamba sijawahi kujaribu? But kwa vile niling'atwa na nyoka hata nikiona unyasi tu nakimbia, bahati mbaya hayo nimepitia ndani ya usichana wangu wote, sina ushuhuda mzuri juu ya suala mahusiano, na hapo haya ndoa haikufungwa!! Kwavile mwenzangu ye kila
Siku anakuambia hajaamua kuoa bado , mtu km mimi bado nataka tena ndoa jamani!!! BIG NO, ndio
Maana nikiona mtu km mtoa mada hapo juu Ukweli najizuia sana kutoa koment Kali , but all in all maisha yanaebdelea na nina furaha zaidi ya muda wote
Nilipokuwa kwenye mahusiano.

Tukubaliane kutokukubaliana inatoooosha
Binafsi nimekuelewa,pole sana
Hiyo ilikuwa bahati mbaya,ila wapo wenye ushuhuda mzuri juu ya waume zao nawenye shuhuda mbaya za wake zao
 
ni vigumu sana kuwa ndani ya ndoa na kupata uhuru wa kibachela. lazima uchague moja uoe na ubaki umefungwa pingu za maisha. au usioe uendelee kula ujana(nimekumbuka ney wa mitego anakula ujana)

Hezbend jana umerudi saa 5 kisa uko na washkaji, sasa leo ukirudi mida hiyo wallah utalala ndani ya gari...
 
Unadhani hiyo ilikuwa fair kwa mama yako? Baba yako ni bonge la selfish. How on earth can you make your wife a watchman just because of alcohol? Kama ingekuwa ni shughuli ya kipato, inaeleweka but kunywa, aah No!

Wakwetu, I wish nimuone mkeo alivyonenepa roho yake... Make wanaume wa aina yako ni wachache sana.... :thumbup:
 
Nimekuwa na uhusiano niseme km mchumba au mpenzi ndani ya miaka 12, tumejaliwa watoto wawili, wakike na kiume, maisha niliyoishi na huyo mtu km sio uvumilivu basi sina Jina la kulipatia sahihi, kwanza ni vile
Nilizaa nae nikawa naogopa sana kutengana nae, na yeye alitumia huo udhaifu wangu ipasavyo, mbinfsi, mnafki, mchoyo, kiburi Yaani wkt mwingine mwanamke
/mwanaume ukiishi na mtu wa namna hii ata unatamani ufanye jambo baya iLi maisha yako yawe na amani, ndugu zangu walinionea huruma
Sana, ila kwakuwa nilikuwa naogopa sana kuwatenga wanangu na baba Yao wakiwa wadogo, na kuanza uhusiano mwingine ambao sijawahi ujua pia, nilivumilia sana, anapokosea kitu mfano umemfumania na mwanamke au umeona kurudi kwake usiku wa manane sio sahihi ukamweleza kwa upole sio tabia njema kunitendea hivyo na watoto wanaona unachokifanya, atakujibu kwani nimekuoa, si tumezaa tu!! Unaweza kuendelea na maisha yako ukiona nakusumbua na "maisha yangu" well mi ni mwombaji sana, nilimuomba sana Mungu anipe nguvu ya kutojali hayo, nilipata chuo uk na nikaja kusoma hapa miaka 2, nikamuacha na watoto ! Akaona watoto wanamsumbua sana kuwa huru atakavyo, akawapeleka kwa mama yangu, mara Ampeleke pesa za matunzo mara aseme kwani huyo wa ulaya kazi yake
Nini uko, atume yeye, Ukweli Mungu alinipa neema ya ajabu , nikaanza kufanya vibarua hapa ulaya na shule pia, baadae nikaomba wanangu waje kunitembelea, walipoingia tu , nikaomba kuongeza muda wa kusoma , wkt huo haukuwa ngumu km sasa , kwahiyo hata watoto wangu waliweza kubaki na kuanza shule hapa uk. Nilipomaliza shule yangu nikapata kazi hapa uk , Ukweli nimeuona mkono wa Mungu ,wanangu sasa wako university na wanafanya vizuri sana, hutanielewa kabisa Nilikuambia sijawahi tena jiingiza kwenye mahusiano na mwanaume
Kwanza kwa uoga,
Pili maumivu niliyo pitia?tatu wanangu bado wananijihitaji kuliko yeyote Yule duniani? Sio kwamba sijawahi kujaribu? But kwa vile niling'atwa na nyoka hata nikiona unyasi tu nakimbia, bahati mbaya hayo nimepitia ndani ya usichana wangu wote, sina ushuhuda mzuri juu ya suala mahusiano, na hapo haya ndoa haikufungwa!! Kwavile mwenzangu ye kila
Siku anakuambia hajaamua kuoa bado , mtu km mimi bado nataka tena ndoa jamani!!! BIG NO, ndio
Maana nikiona mtu km mtoa mada hapo juu Ukweli najizuia sana kutoa koment Kali , but all in all maisha yanaebdelea na nina furaha zaidi ya muda wote
Nilipokuwa kwenye mahusiano.

Tukubaliane kutokukubaliana inatoooosha
Mkimbizi toka tz,nakushauri pamoja hayo yasikufanye kuikimbia nchi yako,watoto wako wakimaliza masomo,rudi nchi mwako tz anza maisha na Mungu atakufanikisha katika yote.
 
Sijakimbia TZ asilimia mia, japo wanangu wanamchukia sana baba Yao, na hawapendi kabisa likizo kuja TZ, ila mimi nakuja kila baada ya mwaka kwa ajili ya mama yangu,maana mama yangu ni muhimu sana na apendi kuja kuishi ulaya, na pia ningependa nikistafu km nipo hai bado, nimalizie uzee wangu TZ, kwahiyo tunajenga nchi pamoja mkuu :)

Tukubaliane kutokukubaliana inatoooosha
 
Back
Top Bottom