rr4
JF-Expert Member
- Mar 19, 2015
- 3,567
- 5,111
Nadhani nyote mnajua kuwa Rwanda, Zambia, DRCongo, na Uganda walikuwa ni watumizi wakubwa wa hii bandari yetu lakini sasa wamegoma na kutokana na ukithiri wa WIZI, UJAMBAZI, RUSHWA, hatutaki kutumia teknolojia ya kisasa, Kodi zisizoeleweka ambazo zinabadilika kila masaa 24 etc.
Lakini pamoja na Rais Magufuli na Kassim Majaliwa kujitahidi lakini ni ngumu sana wao kuweza kufanya chochote kwani Bandari (si ya Dar tuu bali bandari zote za Tanzania) zimekuwa kama vile Cancer na si jipu tena.
Hali hii inatokana na ukweli kuwa kuna wanasiasa waliopo madarakani na wengine wamestaafu kuwa katika kundi linaloitwa THE UNTOUCHABLES kutumia Uongozi na Menejimenti na bodi ya Bandari kukwamisha kwa makusudi jitihada za kuweka mambo wazi kwa njia ya teknolojia.
Lakini hii cabal ya mafisadi (bodi, menejimenti na marafiki zao ambao ni wanasiasa) waliweza kumzidi kete mpaka Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) na ndio maana hata ripoti ya Bandari hamtoiona kwenye website ya CAG!
Lakini haikuishia hapo, special audit ambayo ilitakiwa ifanywe na KPMG nayo ilitupwa pembeni kwani ingeonyesha jinsi gani wafanyakazi wa TPA na hususan Dar es salaam wanavyo manipulate system kuanzia kwenye mageti mpaka kwenye mtandao wa kompyuta (AUTOMATED TERMINAL SYSTEMS (ATM) ambao wanaweza kubadilisha taarifa ambazo hata zile alizonazo Waziri Mkuu Majaliwa zilikuwa ni punje tuu ya gunia la ufisadi unaendelea hapo Bandarini.
Kana kwamba hii haitoshi, hii ATM ilikuwa imewekwa kwa ajili ya kurahisisha mambo kama vile a ship planning, vessel, traffic management, billing and tracking of cargo na hasa ma kontena...
Lakini taarifa ambazo hata TISS (Usalama wa Taifa) walikuwa nazo ni kuwa Bandari ya Dar haina Intergrated Security Systems (ISS) na iliyokuwepo nayo ilichakachuliwa na hili yote ni kurahisisha wizi na ufisafi uliokithiri ambao umebarikiwa na Menejimenti na Bodi ya Bandari. Usalama kama kawaida yao wao walifanya kazi yao kwa weledi uliotukuka lakini ripoti ilipofika kwa vyombo vya juu kama vile Wizara na Polisi hakuna kilichofanywa kwani maslahi ya watu wengi yangeguswa.
Hawa jamaa hawana sana tofauti na Mamlaka nyingine inayoongoza kwa ufisadi Tanzania kwa jina la Tanzania Revenue Authority (TRA), namba mbili ni Wizara ya Ardhi na hawa TPA ni namba tatu. Sasa ukitazama kama zilivyo system za TRA, Wizara ya Ardhi na hawa jamaa wa Bandari kwa kusudi kabisa kila mara majibu yao ni yale yale, system imefeli lakini ukichunguza ni kuwa kuna wajanja wameamua kuibadilisha ili iwe rahisi zaidi kuifanyia manipulation, distortion and breakdown na hii inapelekea Serikali kukosa mapato na pia utaona kabisa kuwa data hizo data zilizomo hazina integrity yoyote ile.
Kwa kifupi ni kuwa mtu yoyote yule anaweza kuingia manually na kubadilisha staus ya cargo kisha unaanza kupigwa kalenda wakai huohuo unapigwa faini ya storage na mengineyo.
Lakini pia shipping lines nao kwa kujua jinsi gani TPA walivyo mafisadi na wenyewe hawajali kuwapatia TPA container loading list ili wafanye reconciliation ya list ya kontena kabla ya billing.
Na kana kwamba hiyo haitoshi, saa zingine visingizio pale bandari vinavyotumika kupiga dili hizi ni umeme kukatika au kuambiwa kuwa mtandao au mfumo wa ki eletroniki umefeli hivyo mambo itabidi yafanywe ki manual manual hivyo watu wanapita tuu kwenye mageti (kote huko watu wanakuwa wamewekwa kupitisha na kugonga mihuri tuuu makaratasi kwa maneno mengine mizigo inapitishwa bila kulipwa ushuru na hakuna anayejali kuweka hizi rekodi kwenye mfumo wa ki elektroniki.
Zaidi ya hayo ni kuwa X-Ray machines zao hazifanyi kazi, Kamera zao hazifanyi kazi, metal detectors nazo hawana na zilizopo zilichakachuliwa na data zote zilizomo kwenye ISS nayo ni feki au zimechakachuliwa, wafanyakazi hawana elimu kwani hawafanyiwi training yoyote ile ya maana na walio na elimu nao washakuwa compromised.
Mimi nashauri TPA iwekwe chini ya emergency taskforce kama enzi zile jiji lilipokuwa chini ya KEENJA hata kwa mwaka mzima, na kama ikishindikana bora tuangalie namna ya kubinafsisha na ubinafsishaji uwe wa wazi, tija, uwe na maslahi kwa taifa, bidding process zote ziwe wazi na kila kitu kiwekwe wazi kwenye mtandao wa Taifa.
Kwa sasa narudi tena kulala nikiamka nitaendelea kuwapa zaidi.
Eee mola... kwani sisi tulikukosea nini na wapi tuliteleza Mungu wetu wa Mbinguni... Kwanini mtu unataka madaraka kwa nguvu then hujui cha kufanya.. Ni nini hiki
Tena unaweza ukaulizwa kwanini nchi yako maskini unasema sijui... Hujui.. Madaraka unataka ya nini.. Uongozi wa nchi si sawa na kuchunga mbuzi... Ni wito wa juu kabisa na kitu cha mwisho kwa mtu mwerevu kukifikiria.. Pale Ikulu wanatakiwa watu wenye personal mission na vision.
Si ni Singapore inalishwa na kujengwa na Bandari tu Jamani...... Kwani Rwanda wana Resources gani hadi wapo juu ivo.
Mheshimiwa Rais John Joseph Pombe Magufuli namuomba Akubariki na Akulinde Mabaya yaliyokuwa au yatakayokuwa yakupate yarudi direct kwa wale waliofanya nchi hii pango la wezi...
Uwe na afya njema na MIMI BINAFSI NI OPPOSITION ILA nakubariki uwe DICTATOR. Please changanya element za Hitler+Ghadafi+Lee Kuan Yew+Kagame= SUPER MAGUFULI.
Kaza uso hasa Rais wetu. Hapo ni Bandari tu.... Je?
1. Tanapa
2. Migodini kule
3. Misitu
4. Ukusanyaji mapato kwenye halimashauri zetu.
5. Gesi iliuzwaje na tunafaidikaje.
6. Na kadhalika na kadhalika na kadhalika.