Sio Tanzania tu, hakuna nchi yoyote Afrika yenye uwezo wa kupambana na Magharibi

Mi mi

JF-Expert Member
Jul 14, 2024
1,648
3,547
Niweke ukweli ili hata wenye tuakili tudogo wajue sio tu Tanzania hapa Africa nzima hakuna nchi yenye uchumi stable wa kuweza kupambana na kutingishana na magharibi.

Bila hata vita za silaha hakuna nchi Africa ya kuweza kupambana na ulimwengu wa magharibi.

Ulimwengu wa magharibi ukiamua nchi fulani sio mshirika wetu kazi ipo kwa hiyo nchi tena kazi nzito haswa.

Naposema ulimwengu wa magharibi namaanisha marekani na washirika wake, ulimwengu wa magharibi ulishinda vita dhidi ya almighty Soviet Union ikafa kifo kibaya sembuse kinchi cha ajabu kiitwacho Tanzania.

Moto wa nchi za magharibi Nyerere aliufahamu vizuri sio tu Nyerere mpaka baba zake Nyerere wa falsafa China na Soviet walijua ukubwa wa ulimwengu wa magharibi haswa.

China ya Mao sio mjinga kuanza kurudisha taratibu uhusiano wake na marekani na ulimwengu mzima wa magharibi Mao aliona hapa kazi ipo ni kuwa mpole na kujua namna ya kula na kipofu.

Napomaanisha ulimwengu wa magharibi ni mifumo yote ya kiutawala na kiuchumi ya kidunia kwa asilimia kubwa imejishikiza wapi ? Ni kwao sio mabank, sio fedha, sio mikopo, sio mifumo ya malipo, sio manunuzi n.k


Leo tukipigwa pin tuna huo uwezo wa kusurvive kwa kipindi kirefu ? Korea kaskazini inaishi kwa support kubwa ya China na hii ni kwa sababu North Korea ana umuhimu sana kwa usalama wa nchi ya China kutokana kwa walivyo pakana na siasa za ukanda ule.

Je, tunaya fahamu maumivu anayo pitia Russia sasa na yeye ni taifa kubwa lenye nguvu na uwezo katika maeneo mbalimbali ?

Je, Iran inapenda kuendelea kuishi chini ya vikwazo na vina madhara gani katika ukuaji wake ?

Hao Iran, North Korea, Russia, China ni washirika walio shibana haswa kwa sababu kila mmoja ana mpatia mwenzake kitu cha muhimu sisi tuna washirika gani tulio shibana nao haswa ? Kwamba tukianza kufungiwa milango tunaweza kubebwa pia tukumbuke anabebwa anaye bebeka.

Hao Wachina, warusi, wairan, wakorea wote wana akili balaa sisi akili sifuri sasa hata huyo atakayetaka kutubeba si atachoka mwenyewe kubeba kundi la wajinga.

Viongozi ni rahisi kuropoka kwa sababu yeye na familia yake maumivu hatoyapata hivyo ndivyo ilivyo kuwa hata kwa mugabe ila wazimbabwe wa kawaida joto la jua waliliona.

Viongozi punguzeni mihemko sisi bado wadogo sana hatuna teknolojia,elimu bora, uchumi bora, afya, uongozi bora hatuna chochote bora cha kuweza kuvimbiana na magharibi.
 
Duniani ni nchi chache sana za kuweza kupambana na magharibi tena zinahesabika sawa na vidole vya kiganja cha mkono mmoja.
 
Fact!

Hata hao tunaowategemea kwamba wanaweza kutusaidia na wao pia wanadhibitiwa na nchi za Magharibi. Nchi ya China, Urusi, Iran, Saudi Arabia, UAE, n.k Wana maslahi makubwa zaidi nchini Marekani kuliko Tanzania au Afrika kwa ujumla.
 
Hatuwezi kufa njaa ila pesa tutakosa ....Maana wale hadzabe hata Rais hawamjui ila wanaishi kwa kula na kulala.
 
Uwezo upo tukitumia akili zetu vizuri.
 
Hana ubavu huo, aliyoyaongea eidha yana baraka zao au keshawapigia goti kuomba msamaha.

Sio kilaza kiasi hicho kwamba awang'ong'e afu USAID zipotee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…