Sio kweli kuwa Mnyika ndio amesababisha mahakama kutoa zuio la bomoabomoa Morogoro road

Kwa hiyo huyo ni mumeo mbona umelalamika sana kuwa sio Ke
Bado una rejea kauli zako any kuna Msemo moja ''never argue with a fool , people might not notice the difference'' hivyo nakuacha Kama ulivyo
 
myika wananchi wa kibamba wanataka maendeleo sio maneno, mfano barabara ya kuluvya kwenda hondogo ni mbovu sana!! inahitaji matengenezo, miundombinu ya maji hakuna, hakuna soko nk. hayo mdio wananchi wanataka kuona unayatenda.
 
Tuache malumbano tupambane tupate haki yetu...sio wakati wa kuambiana nani anasaidia au la...wewe kama mwenyekiti ungetoa nafasi kwa waathirika wenginr kuunganishwa na kesi hii kwa kuwapa maelezo kwa sababu na uhakika sio wote wanao uelewa sawa au kuingia mitandaoni...kama nyie...umoja unahitajika sana katika suala hili
 
Huyo Chrizant Kibogoyo , ni Mwanaharakati na mpigaji mzuri tu, ana maslahi makubwa anayapata kwenye hili la bomoabomoa, anafahamika maeneo yote ya Makondeko ambako ndio kwenye nyumba yao ya urithi, kulikuwa na mradi wa maji Kwembe, yeye akiwa kama Mwenyekiti wa mradi wa maji, kwa kushirIkiana na DAWASA/DAWASCO wamekula fedha ya maana mpaka kufikia mradi kishindwa kujiendesha

Kelele zake ni hofu ya kupokwa Maslahi anayoyapata kwenye hizo harakati za kuchangisha fedha za kuendeshea kesi
Asante kwa ufafanuzi, nilihisi toka mwanzo kuwa huyu jamaa ana lake
 
Lusomya......ushauri wako ni mzuri saana.Nilivyomsoma Mwenyekiti in between the lines namuelewa vingine kabisa.Sheria haitojali kama Mnyika kasaidia....hapa ni upanuzi wa barabara hata kama mutamkana Mnyika muda ukifika watabomoa tu.
Muhimu sasa ni kuwekeza katika kudai fidia na munaweza kuwa kama wazee wa EAC.
 
Ahsante kwa kutuelimisha ila naomba utujuze vile vile ni nani kiongozi wa mawakili waliofika mahakamani kuomba na kufanikiwa kupata zuio husika na ni nani alikuwa anaongoza mikakati ya kuelimisha wananchi kudai haki yao kwa njia ya kimahakama na vile vile kulisema hilo swala bungeni.
Vijiji vya ujamaa sawa, vilikuja na vikaondoka na zama zake. Sasa hivi ni hili swala la mita 240 ndiyo mahangaiko ya sasa kwa wananchi wa Kimara, Mbezi na Kiluvya. Yaani inauma sana Mkuu.
Samahani nipo vijijini ambapo network ni shida. Mawakili wetu ni Destiny Law Chambers ambao kupitia kesi kama hii hii Na 80 ya 2005 waliibwaga Wizara ya Ujenzi Na Tanroads; pia wakawawaga tens katika rufaa waliyoomba Na Appl 151 ya 2015.
Kamati yetu ndio imekuwa ikielimisha wananchi kuhusu haki zao kwa mujibu wa sheria. Wanasiasa wanaogopa kujiingiza kikamilifu kutetea suala hili kws sababu tunaonekana wachache lakini athari za ubabe huu zinamwathiri kila mkazi wa eneo la Ubungo hadi Kibaha kwa uwekezaji wao kukosa thamani kwa sababu maeneo prime yamezuiwa kibabe kuendelezwa.
Aidha watumiaji wa barabara ya Morogoro wote wanaathirika kwa kukosa huduma mbalimbali kama vile mabenki, supermarket n.k wanapokuwa wanatumia barabara hii.
Tunatambua kuwa zimepigwa propaganda kuws sisi ndio chanzo chs foleni. Hii sio kweli hats kidogo kwa kuea eneo halali la hifadhi ya barabara la mits 22.85 kila upande toka katikati ya barabara sawa na mita 45.7 ambalo ndilo lililolipiwa fidia mwishoni mwa miaka 1960. Linaweza kuzalisha njia za barabara (lanes) 14 (45.7\3.25=14) kwa mujibu wa ibara 27 ya Kanuni za Sheria mpya ya barabara Na 13 ya 2007 kinachotamka kuwa "njia moja barabara ya lami isipungue mita 3.25". Barabara ya sasa ya Morogiro yenye njia mbili ina upana wa Mita 6.5.
Kwa mantiki hiyo upanuzivwa sasa wa barabata ya Morogoro kuwa ya njia 6 utatumia Mita 19.5 tu na eneo la mita 26.2 kusalia kwa ajili ya miundombinu mingine.
Hapo utagundua kuwa sio kweli sisi ndio chanzo cha foleni. Pia hakuna ulazima wa kuvunja haki za binadamu za watanzania wenzetu kwa kisingizio cha foleni.
 
..yes.

..anayetaka kuwabomolea nyumba zenu ni Magu na Mbarawa.

..msisahau hilo mkaanza ku focus kwenye mambo madogo-madogo.
Ndio maana tuko kwenye vyombo vya sheria. Ibara 107 A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatamka " Mahakama ndio itakuwa Na kauli ya mwisho katika utoaji haki hapa nchini" Kumbuka kituo cha mafuta cha Mwanza kilivyobomolewa kwa mbwembwe. Unajua Serikali ililazimika kumlipa fidia mhusika ya Bilioni 4 kutokana makosa ya Waziri wake?
 
..asante.

..nilidhani umesahau kuhusu Magu na Mbarawa
 
Kuelekea mbele watanzania tubadulike kuna wakati tunatoa lawama kwa serikari kwa uzembe wetu wenyewe au kufikiri mambo yatabadiliki kwa maslahi yetu mbeleni.

Ukweli ni kwamba kuna maeneo mengine ya Dar Es Salaam yaliuzwa kimakosa na wafanyakazi wa serikari wasiokuwa na maadili mfano mimi namjua mtu ana eneo alilonunua kihalali lakini kwenye kufuatilia kakuta linaangukia katika sehemu ya makaburi kwa mujibu wa city plan. Japokuwa kwa sasa hakuna kaburi hata moja utaratibu ni kwamba unaenda ardhi kutafuta compensation yako, maajabu ni kwamba kuna watu wamejenga na wengine wanaanza ujenzi kama vile city plan aina tija. Na hawa watu huko mbeleni watajifanya wanaonewa wakati wakuvunjiwa ukifika.

Binafsi nilikuwa na huruma nikidhani ni makosa ya serikari lakini na wananchi saa zingine wanakuwa wakaidi au wavivu wa kufuatilia maana hii nchi nayo kuingizwa mkenge ni dakika moja lakini ukienda ardhi majibu unapata, upande wa serikari wafanyakazi wa ardhi inabidi waache kutoa hati katika maeneo ambayo yana plan zingine baadae.
 
Kwa niaba ya Kamati ya Waathirika wa Bomoabomoa ya barabara ya Morogoro nachukua nafasi hii kuweka kumbukumbu sahihi dhidi ya upotoshaji mkubwa uliofanywa Na kikundi cha "CHADEMA IN BLOOD" kuwa Mhe John Mnyika Mbunge Jimbo ka Kibamba amefanikiwa kuwaokoa waathirika kupitia zuio la Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi.

Ili kuweka kumbukumbu sahihi Kesi husika ilifunguliwa na baadhi ya waathirika wapatao 500 na zaidi kidogo siku nyingi hata kabla ya TANROADS kuanza kutoa notisi za ubomoaji. Mhe Mnyika amekuja kujua kuhusu kufunguliwa kwa shauri hili na tarehe ya kusikilizwa kwa maombi ya walalamikaji baada ya notisi kuanza kutolewa tar 2 Mei 2017. Hivyo sio sahihi hata kidogo kwa MTU mzima mwenye akili zake timamu kutoa madai kuwa Mbunge ndio amewaokoa waathirika hawa.

Hadi sasa waathirika waliofungua kesi wamepambana na changamoto kibao ikiwemo ukosefu wa raslimali za kufungua kesi husika. Lakini hatukuwahi kupata msaada wowote kufanikisha hatua hii ya ufunguaji kesi Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kutoka viongozi wa kuchaguliwa ikiwemo Mbunge, Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa n.k wanaojifagilia kupitia kuwa mitandao ya kijamii kuwa ndio wakombozi.

Nichukue fursa hii kuwakumbusha wote wanaojifagilia kutusaidia kuwa hili suala ni la kijamii na si la kisiasa. Hivyo tunawaomba wanasiasa wote wasiokuwa na maadili mema wajiweke kando na shughuli zetu kama ambavyo walijiweka kando baada ya Mhe John Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi kumjibu Mhe John Mnyika kuwa "kama anataka barabara iwe na upana wa rula".

Kutokea hapo mbunge wetu alimuogopa Waziri wa Ujenzi Na akaamua kututekekeza waathirika wa bomoabomoa hii licha ya ukweli kwamba alikuwa na muda uwezo wa kutusaidia kupitia nafasi yake ya ubunge.

Niwatake wanasiasa wote wasiokuwa na utu wajiweke pembeni na mchakato huu wetu sasa kwa kuwa tuliwapatia nafasi ya kutosha kulishughulikia na wakashindwa.

Wanachofanya wanasiasa tuliowachagua ni kutumia mafuta yetu kutukaanga ili tutakapoiva washiriki kalamu ya kututafuna katika kualikwa uwekaji majiwe ya msingi, uzinduzi n.k
Sisi waathirika bado tuna imani na mhimili wa mahakama kutupatia haki yetu.

Aidha bado tuna imani Na wadau mbali mbali wenye nia njema ikiwemo vyama vya siasa vilivyoamua kuweka wazi mustakabali wake wa kujisahihisha na kujirekebisha na kuachana na utapeli wa kisiasa kama unaofanyika katika suala hili la bomoa bomo basdhi ya wsnasiada, kutaka kujipatia umaarufu wa kisiasa kupitia maafa, gharika Na shida za waathirika wa bomoa bomoa hii.

Kamati ya waathirika inachukua fursa hii kuwakumbusha wadau wote kuwa katika suala hili zitajitokeza athari kubwa sana za kijamii, kiuchumi n.k. Hivyo wadau wote wenye nia njema kutoa misaada ya ukweli wanaakikwa. Ikiwemo wale wanaojijua kuwa ndio walihusika kutunga na kuiagiza serikaki ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutekekekeza Operesheni Vijiji vya Ujamaa. Operesheni ambayo ndio chanzo cha hii bomoa bomoa.
Basi ni wewe uliyesababisha.Umefurahi ee?!
 
Tuache malumbano tupambane tupate haki yetu...sio wakati wa kuambiana nani anasaidia au la...wewe kama mwenyekiti ungetoa nafasi kwa waathirika wenginr kuunganishwa na kesi hii kwa kuwapa maelezo kwa sababu na uhakika sio wote wanao uelewa sawa au kuingia mitandaoni...kama nyie...umoja unahitajika sana katika suala hili
Lusomya nakubaliana nawe kwa 100% Na ndio lilikuwa tarajio letu kumshirikisha Mbunge kikamilifu alipotutafuta kujua tumefika wapi katika kuguatilia haki zetu. Kamati imelazimika kuweka kumbukumbu sahihi kwa nia ifuatayo:-
a) kurekebisha upotoshaji ukiofanyika kupitia mitandao ya kijamii kuwa Mbunge kafanikisha upatikanaji wa zuio la mahakama. Wasio Na uelewa mpana watachukulia kuwa zuio hilo linamhusu kila aliyepewa notisi na kuwekewa alama ya X.
b) Kurekebisha madhara yaliyotokana na Mbunge kutumia vibaya taariga nyeti alizozipata kutokana na wadhifa wake kwa malengo ya kujitafutia umaarufu wa kiasiasa pasipo kuzingatia athari xa kitendo hicho.
c) Kurejesha imani za waathirika kwa Kamati yao Na viongozi wake kuwa haina/hawana malengo yoyote ya kisiasa kama ambavyo ilianza kuonekana kutokana vitendo vys ukodefu wa maadili wa Mbunge na timu yake.
d) Kudumisha utamaduni wa kukosoana kwa uwazi na ukweli vinapojitokeza vitendo vyovyote vya ukosefu wa maadili ya uongizi.
Nikubaliane tena na wewe kuwa mshikamano unahitajika sana ktk kipindi hiki. Lakini pasipokuwa Na maadili hats huo mshikamano hauwexi kujengeka
 
Kwa niaba ya Kamati ya Waathirika wa Bomoabomoa ya barabara ya Morogoro nachukua nafasi hii kuweka kumbukumbu sahihi dhidi ya upotoshaji mkubwa uliofanywa Na kikundi cha "CHADEMA IN BLOOD" kuwa Mhe John Mnyika Mbunge Jimbo ka Kibamba amefanikiwa kuwaokoa waathirika kupitia zuio la Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi.

Ili kuweka kumbukumbu sahihi Kesi husika ilifunguliwa na baadhi ya waathirika wapatao 500 na zaidi kidogo siku nyingi hata kabla ya TANROADS kuanza kutoa notisi za ubomoaji. Mhe Mnyika amekuja kujua kuhusu kufunguliwa kwa shauri hili na tarehe ya kusikilizwa kwa maombi ya walalamikaji baada ya notisi kuanza kutolewa tar 2 Mei 2017. Hivyo sio sahihi hata kidogo kwa MTU mzima mwenye akili zake timamu kutoa madai kuwa Mbunge ndio amewaokoa waathirika hawa.

Hadi sasa waathirika waliofungua kesi wamepambana na changamoto kibao ikiwemo ukosefu wa raslimali za kufungua kesi husika. Lakini hatukuwahi kupata msaada wowote kufanikisha hatua hii ya ufunguaji kesi Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kutoka viongozi wa kuchaguliwa ikiwemo Mbunge, Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa n.k wanaojifagilia kupitia kuwa mitandao ya kijamii kuwa ndio wakombozi.

Nichukue fursa hii kuwakumbusha wote wanaojifagilia kutusaidia kuwa hili suala ni la kijamii na si la kisiasa. Hivyo tunawaomba wanasiasa wote wasiokuwa na maadili mema wajiweke kando na shughuli zetu kama ambavyo walijiweka kando baada ya Mhe John Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi kumjibu Mhe John Mnyika kuwa "kama anataka barabara iwe na upana wa rula".

Kutokea hapo mbunge wetu alimuogopa Waziri wa Ujenzi Na akaamua kututekekeza waathirika wa bomoabomoa hii licha ya ukweli kwamba alikuwa na muda uwezo wa kutusaidia kupitia nafasi yake ya ubunge.

Niwatake wanasiasa wote wasiokuwa na utu wajiweke pembeni na mchakato huu wetu sasa kwa kuwa tuliwapatia nafasi ya kutosha kulishughulikia na wakashindwa.

Wanachofanya wanasiasa tuliowachagua ni kutumia mafuta yetu kutukaanga ili tutakapoiva washiriki kalamu ya kututafuna katika kualikwa uwekaji majiwe ya msingi, uzinduzi n.k
Sisi waathirika bado tuna imani na mhimili wa mahakama kutupatia haki yetu.

Aidha bado tuna imani Na wadau mbali mbali wenye nia njema ikiwemo vyama vya siasa vilivyoamua kuweka wazi mustakabali wake wa kujisahihisha na kujirekebisha na kuachana na utapeli wa kisiasa kama unaofanyika katika suala hili la bomoa bomo basdhi ya wsnasiada, kutaka kujipatia umaarufu wa kisiasa kupitia maafa, gharika Na shida za waathirika wa bomoa bomoa hii.

Kamati ya waathirika inachukua fursa hii kuwakumbusha wadau wote kuwa katika suala hili zitajitokeza athari kubwa sana za kijamii, kiuchumi n.k. Hivyo wadau wote wenye nia njema kutoa misaada ya ukweli wanaakikwa. Ikiwemo wale wanaojijua kuwa ndio walihusika kutunga na kuiagiza serikaki ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutekekekeza Operesheni Vijiji vya Ujamaa. Operesheni ambayo ndio chanzo cha hii bomoa bomoa.
Jamani kwani mnyika akiongeza nguvu kunashida? Unaonaje utawalahuu unatiswa na Mahakama? Nafikiri muhimu Ni kumuomba Mungu wakati wote watu wanabomolewa kukiwa na zuio.
 
Hapo kwenye bold ndio nimejua wewe si muathirika wa bomoa bomoa!
 
Back
Top Bottom