Stories of Change - 2022 Competition
Aug 25, 2022
42
71
Takwimu kutoka Shirika la Mfuko wa Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) zinaonyesha kuwa, kila mwezi, takribani wanawake bilioni 1.8 ulimwenguni kote hupata hedhi. Mwanzo wa hedhi kibaiolojia inamaanisha kuwa kuna awamu mpya katika uwezekano wa ongezeko la mwanadamu duniani, yaani upatikanaji wa kiumbe hai (mtoto). Katika mandhari tofauti tofauti, hususani katika nchi zinazoendelea, katika maeneo ya vijijini, swala hili limekuwa likiwarudisha nyuma wasichana wengi wadogo kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi sekondari kwenye mahudhurio.

Wasichana wengi waliobalehe wanakabiliwa na unyanyapaa, kunyanyaswa na kutengwa na jamii wakati wa hedhi, hivyo hupelekea kukosa masomo na kubaki nyumbani kutokana na hedhi, jambo ambalo ni la kawaida lakini kutokana na uwezo mchanga wa uelewa katika maeneo ya vijijini, wengi husababisha mabinti hawa kukosa haki yao ya msingi mara kadhaa kila mwezi ya kuzikomboa fikra zao katika mbio za kuukwepa ujinga, kama adui mmoja wapo nchini kwetu Tanzania kufuatia msisitizo wa mara kadha wa kadha aliokuwa akiusisitizia Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Mbali na hapo, takwimu kutoka jarida la African Educational Journal (AEJ) zinaonyesha kuwa msichana mmoja (1) kati ya wasichana kumi (10) wa shule za kiafrika kila mwaka hukosa au kuacha masomo kabisa, kwasababu ya hedhi. Nchini Tanzania, takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya 28% ya wasichana hukosa siku 35 za mwaka wa masomo (Ripoti ya UNESCO, 2018) kutokana na usimamizi duni katika kipindi hiki pamoja na wasiwasi wa udhalilishwaji.

Hii inaletwa kwasababu mbalimbali zikiwemo uwezo duni wa wazazi wa watoto hawa kuweza kuwanunulia taulo za kike; elimu ndogo ya jinsi ya kuwahudumia wasichana hawa kuweza kujisimamia katika kipindi hiki wanachopitia; Hivyo, hii inaonesha ni kwa jinsi gani changamoto hii inayogusa sekta ya afya na elimu, inavyorudisha nyuma nguvu za serikali katika uboreshwaji wa huduma za kielimu zinazosisitiziwa na kuwekewa mkazo kila kukicha kwasababu ya watoto hawa kupitia vikwazo hivyo.

Miaka miwili iliyopita, Ripoti kutoka shirika moja wapo la Umoja wa Mataifa liitwalo (UNFPA) lilibaini kuwa katika mkoa wa Kigoma nchini Tanzania, kuna baadhi ya wasichana wadogo ambao hutumia hata matambara katika kujisitiri pindi wanapozipitia siku zao kila mwezi, jambo ambalo ni hatari kwa afya kwasababu vitambaa hivyo havijathibitishwa kuwa salama kwa matumizi ya msichana yoyote hususani katika sehemu hizo.

UNI210244.jpg

Chanzo: unicef.org

Tunasikia mara kwa mara kutoka kwa wataalamu wetu kwamba, mfumo hafifu wa usafi na utumiaji mbovu wa taulo za kike unaweza kuwa na athari mbaya kwa afya ya wanawake. Tatizo hilo linaweza kumfanya mwanamke kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya homa ya ini, magonjwa ya mfumo wa mkojo, saratani ya shingo ya kizazi na magonjwa mengine yanayoathiri mfumo wa uzazi. Mapambano dhidi ya unyanyapaaji unaohusishwa na hedhi ni jambo la kulivalia njuga kikamilifu kuanzia serikali ikisaidiana vilivyo na asasi zisizo za kiserikali ili kulipigania jambo hili kupitia zoezi shirikishi baina ya pande zote. Hii itasaidia zaidi katika kuongeza uelewa na kuelimisha umma juu ya swala hili ambalo ni jambo la kawaida linalochukuliwa kwa mtazamo hasi, haswa katika maeneo yaliyo mbali na mji.

Kama wanaharakati wa kupigania haki za wenzetu wanaoishi katika mazingira ambayo si rafiki kupata huduma bora na ambao ni ngumu kwa wao kupata mtu wa kuwasemea changamoto zao mmoja mmoja, licha ya kuwepo kwa wabunge na viongozi mbalimbali ambao wanahusika moja kwa moja kutatua changamoto za jamii kiujumla kama miundombinu na huduma nyinginezo; yatupasa kupaza sauti zetu kikamilifu kadiri ya uwezo wetu, ili tuweze kuona ni njia gani bora tunaweza kuitumia kuwapunguzia uzito wa changamoto hizo au kuwakomboa wasichana hawa wanaopitia vikwazo hivi, kwani hedhi si ugonjwa bali ni hali tu ya kawaida ambayo msichana yoyote ambaye anaweza kushika ujauzito anaipitia mara kadhaa wa kadhaa, kila mwezi ili kukamilisha mzunguko wake.

Kufuatia changamoto hii inayowakumba wasichana hawa wadogo, inayowapelekea muda mwingine kukosa baadhi ya vipindi muhimu mashuleni, na kunyanyapaliwa katika jamii zao napendekeza mambo yafuatayo yafanyike ili kupunguza uzito wa hili jambo kama sio kulitokomeza kabisa:

  • Serikali kupitia Wizara zake ambazo moja kwa moja zinaguswa na changamoto hii mfano Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu pamoja na Wizara ya TAMISEMI waunde mfumo maalum ambao utawawezesha wanafunzi hasa watoto wa kike wanaosoma katika maeneo mbalimbali kupata elimu hii ya afya ya hedhi (Menstrual hygiene) kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi sekondari. Tunafahamu vipindi vya kawaida ni Jumatatu hadi Ijumaa; Muda maalum unaweza tengwa kwa ajili ya kuwaelimisha watoto hawa haswa mwishoni mwa wiki, ili waanze kupata ufahamu wa jinsi ya kujisimamia kikamilifu pindi wanapoanza kuzipitia siku zao. Naamini kuna walimu wa kike mashuleni ambao wana ufahamu mzuri juu ya maswala haya, hivyo mfumo mzuri ukiwekwa katika ratiba za mashuleni katika utoaji wa elimu hii ya kiafya ikiambatanishwa na motisha kwa watoaji elimu hao, itasaidia kuikomboa jamii ya watoto wengi wa kike ambao hukosa masomo kwa zaidi ya siku 35 kwa mwaka mzima wa masomo, kama takwimu kutoka UNESCO zilivotuonyesha hapo awali.

  • Wajasiriamali wadogo wadogo wenye nia madhubuti ya kuwasaidia watoto hawa kupitia utengenezaji wa taulo za kike (pedi) ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja (re-usable sanitary pads) wapewe vipaumbele na mazingira wezeshi ili kuweza kulifanya jambo hili kwa ukubwa zaidi. Serikali inaweza kuwasaidia wajasiriamali hawa kwa kuwapunguzia kodi kwa kiasi kikubwa, kwani huduma wanayotoa inagusa maisha ya wasichana moja kwa moja katika kushiriki masomo yao kikamilifu na kwa amani; kuwapa mikopo ili kuboresha miundombinu ya vitendea kazi ili waweze kuzitengeneza pedi hizi kwa ubora zaidi na kwa ukubwa zaidi; vilevile kuwapa mafunzo watu wenye nia ya kulifanya jambo hili kwenye jamii nyingine nyingi zinazopitia changamoto hii. Ili kuweza kuzikomboa jamii nyingi iwezekanavyo kutoka maeneo mbalimbali nchini.
    Christina Tailosi and Ruth Makina display the pads3_0.jpg
Chanzo: unicef.org
Taulo za kike ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja, zina faida zifuatao:
  • Zinapunguza kiwango cha uzalishaji taka
  • Zinasifika kuwa ni bora na nzuri kwa afya, endapo zikitumika kwa usahihi
  • Zinapunguza gharama za matumizi. Mfano pakiti moja ya Elea pads, inauzwa shilingi Tsh 5000, ambayo ina pedi zaidi ya nne (4) zimethibitishwa kuweza kutumika kwa zaidi ya mwaka mmoja (1)
  • Hazina kemikali yoyote ambayo inaweza kuziathiri sehemu za chini za mwanamke
  • Tafiti nyingi zinaonesha kuwa zinamfanya msichana ajisikie huru zaidi ukilinganisha na pedi ambazo ni za kutumika mara moja na kutupa

  • Wanajamii wa eneo husika pamoja na serikali ijihakikishie inawapa nafasi viongozi wenye utashi na uelewa wa kuchanganua mambo kupitia weledi waliokuwa nao. Haipendezi kuwa na kiongozi hata katika ngazi ya chini kabisa kijijini au mtaani, ambaye anashabikia tamaduni potofu, kama vile mtoto wa kike haruhusiwi kupika, kufua nguo zake au za wazazi wake, kujishughulisha na kazi za kijamii, kipindi yupo katika siku zake (hedhi) kwa kuamini kuwa ataleta nuksi au mkosi katika kutimiza majukumu hayo. Hivi ni vitu vya aibu na sio vya kufumbiwa macho, kwani italeta picha ya kwamba elimu inayotiliwa mkazo kwa nguvu zote na serikali bado haijaikomboa jamii na ujinga au mawazo potofu kabisa. Hivyo, wanajamii kwa nafasi yao, na serikali kwa nafasi yao, wahakikishe wanawapa mamlaka viongozi wenye weledi madhubuti, ambao wanakwenda kupigania na kusimamia haki kwa wote na kukemea vitu ambavyo havina umuhimu wowote na manufaa yoyote katika jamii na taifa zima kwa ujumla.

  • Serikali ihakikishe kuwa mashuleni na sehemu nyinginezo za utoaji wa huduma haswa vijijini kuna mazingira safi, salama na wezeshi kwa watoto wa kike, ili kuweza kujihudumia vizuri kipindi wanapitia mizunguko yao. Upatikanaji wa maji safi na salama, vyoo safi na salama, kuwepo kwa vihifadhi taka (dustbins) vikubwa vya kuhifadhi taulo hizo za kike ambazo zimekwisha tumika; ni vitu muhimu vya kupewa kipaumbele katika harakati hizi kukomboa kizazi hiki ambacho kimesahaulika kutokana na kufumbiwa macho kwa hii changamoto.

  • Ikiwezekana, Serikali inaweza kuanza kampeni ya utoaji na usambazaji wa taulo za kike bure kwa wanajamii wanaoishi katika mazingira magumu. Tumeshuhudia miezi kadhaa iliyopita nchi ya Scotland barani ulaya, imetangaza zoezi la upatikanaji wa taulo za kike bure kwa wanajamii wake ambao wanashindwa kukidhi uwezo wa kununua nyenzo hizo muhimu. Hivyo, kama inawezekana basi, kwa kiasi chake, serikali ianze mbio hizi au kampeni hizi, ninaamini asasi nyingine zisizo za kiserikali na mashirika makubwa ya kimataifa kama USAID, UKAID, KOICA, UNESCO na mengine mengi, yanaweza kuunga mkono na kufadhili mbio hizi zitakazoweza kuzikomboa jamii nyingi za Tanzania zinazopitia vikwazo hivi.

  • Maboresho yafanyike kwenye mitaala inayotumika kuwapa wanafunzi elimu mashuleni. Nashauri, Serikali iratibu upatikanaji wa elimu kuhusiana na maswala ya afya ya mwili na ya akili. Licha ya wanafunzi kusoma masomo mbalimbali kulingana na taaluma wanazopendelea, serikali ijikite pia katika kutoa mafunzo kwa wanafunzi hawa hata kwenye muda wa ziada, ili iweze kuwaanda kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii kwenye masuala ya kiafya na kiutamaduni ili waweze kuzitambua na kusimamia haki zao kikamilifu.

Hitimisho:
Napenda kuchukua fursa hii, kutoa wito kwa viongozi katika ngazi mbalimbali serikalini, watunga sheria na sera za nchi, wasijikite kwenye kutatua changamoto za kiujumla katika jamii tu, bali wajitahidi kufika hata katika ngazi za chini kabisa kwenye baadhi ya maeneo yenye uhitaji kweli kweli, ili kutatua vyanzo vya changamoto hizo. Hii itasaidia kukata mizizi kutoka kwenye shina la matatizo hayo yanayozikumba jamii zetu; kwani wengi tunajikita kutatua changamoto zinazojulikana, lakini tunasahau kutatua vyanzo vyake; tukiweza kutatua vyanzo vya changamoto mbalimbali, hakika tutaweza kuvuka viunzi vingi vilivyokuwa vikitushikilia kusonga mbele kwa namna moja au nyingine.
 
Takwimu kutoka Shirika la Mfuko wa Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) zinaonyesha kuwa, kila mwezi, takribani wanawake bilioni 1.8 ulimwenguni kote hupata hedhi. Mwanzo wa hedhi kibaiolojia inamaanisha kuwa kuna awamu mpya katika uwezekano wa ongezeko la mwanadamu duniani, yaani upatikanaji wa kiumbe hai (mtoto). Katika mandhari tofauti tofauti, hususani katika nchi zinazoendelea, katika maeneo ya vijijini, swala hili limekuwa likiwarudisha nyuma wasichana wengi wadogo kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi sekondari kwenye mahudhurio.

Wasichana wengi waliobalehe wanakabiliwa na unyanyapaa, kunyanyaswa na kutengwa na jamii wakati wa hedhi, hivyo hupelekea kukosa masomo na kubaki nyumbani kutokana na hedhi, jambo ambalo ni la kawaida lakini kutokana na uwezo mchanga wa uelewa katika maeneo ya vijijini, wengi husababisha mabinti hawa kukosa haki yao ya msingi mara kadhaa kila mwezi ya kuzikomboa fikra zao katika mbio za kuukwepa ujinga, kama adui mmoja wapo nchini kwetu Tanzania kufuatia msisitizo wa mara kadha wa kadha aliokuwa akiusisitizia Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Mbali na hapo, takwimu kutoka jarida la African Educational Journal (AEJ) zinaonyesha kuwa msichana mmoja (1) kati ya wasichana kumi (10) wa shule za kiafrika kila mwaka hukosa au kuacha masomo kabisa, kwasababu ya hedhi. Nchini Tanzania, takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya 28% ya wasichana hukosa siku 35 za mwaka wa masomo (Ripoti ya UNESCO, 2018) kutokana na usimamizi duni katika kipindi hiki pamoja na wasiwasi wa udhalilishwaji.

Hii inaletwa kwasababu mbalimbali zikiwemo uwezo duni wa wazazi wa watoto hawa kuweza kuwanunulia taulo za kike; elimu ndogo ya jinsi ya kuwahudumia wasichana hawa kuweza kujisimamia katika kipindi hiki wanachopitia; Hivyo, hii inaonesha ni kwa jinsi gani changamoto hii inayogusa sekta ya afya na elimu, inavyorudisha nyuma nguvu za serikali katika uboreshwaji wa huduma za kielimu zinazosisitiziwa na kuwekewa mkazo kila kukicha kwasababu ya watoto hawa kupitia vikwazo hivyo.

Miaka miwili iliyopita, Ripoti kutoka shirika moja wapo la Umoja wa Mataifa liitwalo (UNFPA) lilibaini kuwa katika mkoa wa Kigoma nchini Tanzania, kuna baadhi ya wasichana wadogo ambao hutumia hata matambara katika kujisitiri pindi wanapozipitia siku zao kila mwezi, jambo ambalo ni hatari kwa afya kwasababu vitambaa hivyo havijathibitishwa kuwa salama kwa matumizi ya msichana yoyote hususani katika sehemu hizo.

View attachment 2336823
Chanzo: unicef.org

Tunasikia mara kwa mara kutoka kwa wataalamu wetu kwamba, mfumo hafifu wa usafi na utumiaji mbovu wa taulo za kike unaweza kuwa na athari mbaya kwa afya ya wanawake. Tatizo hilo linaweza kumfanya mwanamke kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya homa ya ini, magonjwa ya mfumo wa mkojo, saratani ya shingo ya kizazi na magonjwa mengine yanayoathiri mfumo wa uzazi. Mapambano dhidi ya unyanyapaaji unaohusishwa na hedhi ni jambo la kulivalia njuga kikamilifu kuanzia serikali ikisaidiana vilivyo na asasi zisizo za kiserikali ili kulipigania jambo hili kupitia zoezi shirikishi baina ya pande zote. Hii itasaidia zaidi katika kuongeza uelewa na kuelimisha umma juu ya swala hili ambalo ni jambo la kawaida linalochukuliwa kwa mtazamo hasi, haswa katika maeneo yaliyo mbali na mji.

Kama wanaharakati wa kupigania haki za wenzetu wanaoishi katika mazingira ambayo si rafiki kupata huduma bora na ambao ni ngumu kwa wao kupata mtu wa kuwasemea changamoto zao mmoja mmoja, licha ya kuwepo kwa wabunge na viongozi mbalimbali ambao wanahusika moja kwa moja kutatua changamoto za jamii kiujumla kama miundombinu na huduma nyinginezo; yatupasa kupaza sauti zetu kikamilifu kadiri ya uwezo wetu, ili tuweze kuona ni njia gani bora tunaweza kuitumia kuwapunguzia uzito wa changamoto hizo au kuwakomboa wasichana hawa wanaopitia vikwazo hivi, kwani hedhi si ugonjwa bali ni hali tu ya kawaida ambayo msichana yoyote ambaye anaweza kushika ujauzito anaipitia mara kadhaa wa kadhaa, kila mwezi ili kukamilisha mzunguko wake.

Kufuatia changamoto hii inayowakumba wasichana hawa wadogo, inayowapelekea muda mwingine kukosa baadhi ya vipindi muhimu mashuleni, na kunyanyapaliwa katika jamii zao napendekeza mambo yafuatayo yafanyike ili kupunguza uzito wa hili jambo kama sio kulitokomeza kabisa:

  • Serikali kupitia Wizara zake ambazo moja kwa moja zinaguswa na changamoto hii mfano Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu pamoja na Wizara ya TAMISEMI waunde mfumo maalum ambao utawawezesha wanafunzi hasa watoto wa kike wanaosoma katika maeneo mbalimbali kupata elimu hii ya afya ya hedhi (Menstrual hygiene) kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi sekondari. Tunafahamu vipindi vya kawaida ni Jumatatu hadi Ijumaa; Muda maalum unaweza tengwa kwa ajili ya kuwaelimisha watoto hawa haswa mwishoni mwa wiki, ili waanze kupata ufahamu wa jinsi ya kujisimamia kikamilifu pindi wanapoanza kuzipitia siku zao. Naamini kuna walimu wa kike mashuleni ambao wana ufahamu mzuri juu ya maswala haya, hivyo mfumo mzuri ukiwekwa katika ratiba za mashuleni katika utoaji wa elimu hii ya kiafya ikiambatanishwa na motisha kwa watoaji elimu hao, itasaidia kuikomboa jamii ya watoto wengi wa kike ambao hukosa masomo kwa zaidi ya siku 35 kwa mwaka mzima wa masomo, kama takwimu kutoka UNESCO zilivotuonyesha hapo awali.

  • Wajasiriamali wadogo wadogo wenye nia madhubuti ya kuwasaidia watoto hawa kupitia utengenezaji wa taulo za kike (pedi) ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja (re-usable sanitary pads) wapewe vipaumbele na mazingira wezeshi ili kuweza kulifanya jambo hili kwa ukubwa zaidi. Serikali inaweza kuwasaidia wajasiriamali hawa kwa kuwapunguzia kodi kwa kiasi kikubwa, kwani huduma wanayotoa inagusa maisha ya wasichana moja kwa moja katika kushiriki masomo yao kikamilifu na kwa amani; kuwapa mikopo ili kuboresha miundombinu ya vitendea kazi ili waweze kuzitengeneza pedi hizi kwa ubora zaidi na kwa ukubwa zaidi; vilevile kuwapa mafunzo watu wenye nia ya kulifanya jambo hili kwenye jamii nyingine nyingi zinazopitia changamoto hii. Ili kuweza kuzikomboa jamii nyingi iwezekanavyo kutoka maeneo mbalimbali nchini. View attachment 2336829
Chanzo: unicef.org
Taulo za kike ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja, zina faida zifuatao:
  • Zinapunguza kiwango cha uzalishaji taka
  • Zinasifika kuwa ni bora na nzuri kwa afya, endapo zikitumika kwa usahihi
  • Zinapunguza gharama za matumizi. Mfano pakiti moja ya Elea pads, inauzwa shilingi Tsh 5000, ambayo ina pedi zaidi ya nne (4) zimethibitishwa kuweza kutumika kwa zaidi ya mwaka mmoja (1)
  • Hazina kemikali yoyote ambayo inaweza kuziathiri sehemu za chini za mwanamke
  • Tafiti nyingi zinaonesha kuwa zinamfanya msichana ajisikie huru zaidi ukilinganisha na pedi ambazo ni za kutumika mara moja na kutupa

  • Wanajamii wa eneo husika pamoja na serikali ijihakikishie inawapa nafasi viongozi wenye utashi na uelewa wa kuchanganua mambo kupitia weledi waliokuwa nao. Haipendezi kuwa na kiongozi hata katika ngazi ya chini kabisa kijijini au mtaani, ambaye anashabikia tamaduni potofu, kama vile mtoto wa kike haruhusiwi kupika, kufua nguo zake au za wazazi wake, kujishughulisha na kazi za kijamii, kipindi yupo katika siku zake (hedhi) kwa kuamini kuwa ataleta nuksi au mkosi katika kutimiza majukumu hayo. Hivi ni vitu vya aibu na sio vya kufumbiwa macho, kwani italeta picha ya kwamba elimu inayotiliwa mkazo kwa nguvu zote na serikali bado haijaikomboa jamii na ujinga au mawazo potofu kabisa. Hivyo, wanajamii kwa nafasi yao, na serikali kwa nafasi yao, wahakikishe wanawapa mamlaka viongozi wenye weledi madhubuti, ambao wanakwenda kupigania na kusimamia haki kwa wote na kukemea vitu ambavyo havina umuhimu wowote na manufaa yoyote katika jamii na taifa zima kwa ujumla.

  • Serikali ihakikishe kuwa mashuleni na sehemu nyinginezo za utoaji wa huduma haswa vijijini kuna mazingira safi, salama na wezeshi kwa watoto wa kike, ili kuweza kujihudumia vizuri kipindi wanapitia mizunguko yao. Upatikanaji wa maji safi na salama, vyoo safi na salama, kuwepo kwa vihifadhi taka (dustbins) vikubwa vya kuhifadhi taulo hizo za kike ambazo zimekwisha tumika; ni vitu muhimu vya kupewa kipaumbele katika harakati hizi kukomboa kizazi hiki ambacho kimesahaulika kutokana na kufumbiwa macho kwa hii changamoto.

  • Ikiwezekana, Serikali inaweza kuanza kampeni ya utoaji na usambazaji wa taulo za kike bure kwa wanajamii wanaoishi katika mazingira magumu. Tumeshuhudia miezi kadhaa iliyopita nchi ya Scotland barani ulaya, imetangaza zoezi la upatikanaji wa taulo za kike bure kwa wanajamii wake ambao wanashindwa kukidhi uwezo wa kununua nyenzo hizo muhimu. Hivyo, kama inawezekana basi, kwa kiasi chake, serikali ianze mbio hizi au kampeni hizi, ninaamini asasi nyingine zisizo za kiserikali na mashirika makubwa ya kimataifa kama USAID, UKAID, KOICA, UNESCO na mengine mengi, yanaweza kuunga mkono na kufadhili mbio hizi zitakazoweza kuzikomboa jamii nyingi za Tanzania zinazopitia vikwazo hivi.

  • Maboresho yafanyike kwenye mitaala inayotumika kuwapa wanafunzi elimu mashuleni. Nashauri, Serikali iratibu upatikanaji wa elimu kuhusiana na maswala ya afya ya mwili na ya akili. Licha ya wanafunzi kusoma masomo mbalimbali kulingana na taaluma wanazopendelea, serikali ijikite pia katika kutoa mafunzo kwa wanafunzi hawa hata kwenye muda wa ziada, ili iweze kuwaanda kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii kwenye masuala ya kiafya na kiutamaduni ili waweze kuzitambua na kusimamia haki zao kikamilifu.

Hitimisho:
Napenda kuchukua fursa hii, kutoa wito kwa viongozi katika ngazi mbalimbali serikalini, watunga sheria na sera za nchi, wasijikite kwenye kutatua changamoto za kiujumla katika jamii tu, bali wajitahidi kufika hata katika ngazi za chini kabisa kwenye baadhi ya maeneo yenye uhitaji kweli kweli, ili kutatua vyanzo vya changamoto hizo. Hii itasaidia kukata mizizi kutoka kwenye shina la matatizo hayo yanayozikumba jamii zetu; kwani wengi tunajikita kutatua changamoto zinazojulikana, lakini tunasahau kutatua vyanzo vyake; tukiweza kutatua vyanzo vya changamoto mbalimbali, hakika tutaweza kuvuka viunzi vingi vilivyokuwa vikitushikilia kusonga mbele kwa namna moja au nyingine.
Kaka Andrew

Nimekupigia Kura Naomba na Mimi unipigie Kura kupitia SoC 2022 - Tufuge nyuki kwa maendeleo endelevu na tuwalinde kwa wivu mkubwa
 
Excellent👏 Ni muhimu kutatua vyanzo vya matatizo kuliko kusubiri kutatua matatizo yenyewe!
Hakika kabisa kaka, tukiendelea kutatua changamoto na kusahau mizizi ya yanapoanzia tutashindwa kushughulikia jambo hilo kikamilifu. Tukiweza kumudu chanzo, hakika tutatoa masuluhisho ya changamoto hizi na nyingine nyingi hususani katika nchi zinazoendelea
 
Big up brother nkuona mbali mno may lord bless you fact kwamba serikali inabidi iratibu elimu ya afya ya mwili na akili kuliko masomo ambayo wanafunzi wanayopendelea hii pia itasaidia sana mwanfunzi kukabiliana na changamoto mbali mbali katika jamii
 
Back
Top Bottom