Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Klabu ya soka ya Singida United imetangaza kuwasajili wachezaji wapya watatu, akiwemo mshambuliaji kutoka Ivory Coast na mwingine kutoka Brazil
Mkurugenzi Singida United, Festo Sanga amewataja wachezaji hao kuwa ni Amara Diaby(Ivory Coast) kutoka klabu ya ASEC Mimosas, John Tibar kutoka Ndanda FC na mshambuliaji wa Felipe Dos Santos kutoka Brazil
Mchezaji Amara Diaby ametia saini mkataba wa miaka miwili huku Tiba John kutoka Ndanda FC akisaini kandarasi ya miaka mitatu
Aidha aliyekuwa kocha wa Singida United, Hans Van Pluijm atajiunga na klabu ya Azam FC katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara