“Lukas uwe na safari njema baba ila usisahau kuwa kuna mtu umemuacha huku”
“Sawa mama sitasahau namheshimu sana Sumaya hata na wewe mama siwezi kufanya hivyo”
“Sawa Sumaya Usilie mwanangu utaumwa hiyo ni safari tu atarudi”
Haukupita muda Lukas aliondoka na kuelekea kwenye ndege kwaajili ya safari huku nyuma Sumaya hakuacha kumtizama mpaka anapotea kwenye macho yake, aligeuka na kuambatana na mama yake kurudi nyumbani.
ENDELEA………..
Ilikuwa ni mapema sana simu ya Sumaya iliita na alipoangalia alikuwa ni baba yake ndiye anayempigia.
“Daddy you didn’t sleep until this time?”
“Sumaya umefikia wapi lile jambo letu mama?” Hakujibu swali badala yake na yeye Aliuliza swali lingine
“Daddy sijafikiria kabisa kuhusu jambo hilo”
“Mwanangu baba yako umri unaenda sasa unafikiria ni nani ataendesha biashara zangu Sumaya, nakuomba fanya hivyo tafadhali wewe ni mwanangu wa pekee niliye naye hata ukitaka kwenda nchi yoyote niambie niko tayari kukupeleka popote”
“Labda unipe muda zaidi nifikirie ila sina uhakika juu ya hilo baba”
“Please Sumaya do it…….”
“Daddy I will think about it”
Aliongea hivyo na kukata simu, hakuwa tayari kufanya kile baba yake alimuomba kwani alitaka kuwa mwanamitindo tu hakuna kingine alikiwaza.
**
Huku Tanzania katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Kambarage Nyerere inaonekana familia nzima ya Mrs Costanzo bila kuwasahau Anitha na Halima walikuwa wakimuaga kijana pekee Alvin kwaajili ya safari yake kwenda Marekani kimasomo, Anitha aliumia sana kwani alijua kuwa anamkosa mwanaume ambaye alikuwa akimpenda sana na sio Anitha tu hata Alvin mwenyewe kwani alishaanza kuvutiwa na kumpenda Anitha tokea alipoonjeshwa asali ya mwanamke huyo na kupelekea kumpenda sana.
“I will miss you brother” Ilikuwa ni sauti iliyojaa huzuni na deko ya msichana mdogo Nicole akimuaga kaka yake huyo wa pekee
“Me too Nicole” Alvin alimkumbatia mdogo wake muda huo Mrs Costanzo alikuwa akiwatizama tu wawili hao bila kuongea chochote kwa alikuwa ameshaongea naye vya kutosha mwanaye.
Waliagana na sasa Alvin aliwaacha hapo na yeye akaondoka, familia iliyobaki nayo aliondoka hapo muda huo baada ya Alvin kuwaacha kwakuwa ilikuwa bado asubuhi mapema Mrs Costanzo aliona ni bora wapite kwenye mgahawa ili wapate chai kisha awarudishe nyumbani na yeye aende kazini aliona mambo yatakuwa mengi mpaka warudi nyumbani kuandaa chai.
Walipomaliza Mrs Costanzo aliwarudisha Anitha na Halima nyumbani kisha alimpeleka shuleni Nicole na yeye alielekea kazini kwake.
Mr Hernad alikuwa akijiandaa kwenda kazini mke wake alimfuata na kuketi pembeni akimtizama alipokuwa akijiweka vizuri tai yake shingoni.
“There is something huge?” Aliuliza Mr Hernad akijitazama kwenye kioo kikubwa cha kabati la nguo
“Nothing but nilikuwa nataka tu kukuuliza umefikia wapi kumshawishi Sumaya?”
“Naona kazi imekuwa ngumu mke wangu Sumaya ameshikilia msimamo wake”
“Mmmh sasa itakuwaje? Mi naona tuendelee kumshawishi tu halafu kuna yule mtoto wa dada yangu Erick naona alipokuwa anafanyia kazi kuna shida kidogo kwa sasa yupo hana tu kazi”
“Kasomea fani gani?”
“Procurement yupo vizuri sana”
“Okay haina shida mwambie ajiandae akiwa tayari aje ofisini na vitu vyote vya muhimu nitaangalia anafit kwenye nafasi gani”
“Asante sana mume wangu utakuwa umemsaidia sana”
“Usijali Erick naye ni mwanangu na ni wajibu wangu kumsaidia” Alibeba begi lake kisha akaaga na kuondoka, huku mke wake alichukua simu yake na kumpigia Erick kumpa taarifa kutoka kwa Mr Hernad alipomaliza kuongea naye alimpigia Sumaya.
“Shikamoo mama”
“Marahaba mwanangu….. kwema huko?”
“Kwema mama mnaendeleaje?”
“Sisi ni wazima, nimesikia umemkatalia baba yako kuhusu lile jambo?”
“Aah mama tatizo sio kitu ambacho nilitaka nikasome ila hata hivyo nilimuambia nitalifikiria”
“Ila usijali mwanangu we somea kitu ambacho unakipenda haya mengine ni machaguzi tu lakini kaka yako atakuwakulisha maana Sio muda mrefu baba yako atampa kazi pale”
“Ooh unasema kweli mama? Basi ni jambo jema”
“Sawa, baadae basi nami niendelee na shughuli nyingine”
“Sawa mama Nakupenda”
“Nakupenda pia mwanangu” Alikata simu na kuiweka pembeni huku akionekana kutabasamu.
**********
Mwanzoni mawasiliano kati ya Lukas yalikuwa mazuri bila shida yoyote muda mwingi walikuwa wakiongea kwa njia ya video call au hata kwa sauti na furaha kwenye penzi lao ilizidi kuongezeka japokuwa walikuwa mbali.
Ilikuwa haipiti siku hawajawasiliana na hiyo ndio ilikuwa kawaida yao na wakazoea hivyo hata penzi lao lipi endelea kukua zaidi na zaidi.
Huku Zuleya na Carlos walizidi kuzama kwenye huba zito kadri siku zilivyozidi kwenda huku Carlos akimueleza Zuleya nia yake ya kuuza vitu vyake vyote na mali zote alizonazo Jamaica na kutaka kurudi Kenya.
“Kwahiyo lini unaondoka?” Aliuliza Zuleya huzuni
“Kila kitu kikiwa Sawa nitaondoka but sitaki kuondoka mwenyewe Zuleya”
“Carlos…..”
“Najua najua nita arrange kila kitu usijali, au.. au haunipendi Zuleya…….”
“Carlos….. aaah hayo yanatoka wapi I’m just worried about my daughter”
“Najua na ndio maana nikakuambia Nita arrange kila kitu hata akisoma huku then kila likizo atakuwa anaenda Kenya”
“Ni wazo zuri pia”
“Nimeshanunua nyumba na tayari nina mgahawa mkubwa kuliko wa huku hivyo maisha yetu hayatakuwa mabaya sana mpenzi”
Alimtizama Zuleya ambaye alikuwa anatabasamu kuonesha kuwa alifurahishwa na maamuzi ya Carlos, alimkumbatia taratibu na kujituliza kwenye kifua cha mwanaume.
“Utakula nini mpenzi” Aliuliza Carlos kwa sauti ya chini
“Carlos hapa ni kama kwangu usiwaze ngoja niingie jikoni nikapike tule” Zuleya alipoongea hivyo Carlos alionekana kuzama kwenye mawazo mazito sana ni kama kuna jambo alilikumbuka
“Carlos……”
“Aaah….. Zuleya twende jikoni pamoja” Alimshika mkono na kuongozana pamoja mpaka jikoni.
Wakati Zuleya akiendelea kupika Carlos alimsogelea na kumkumbatia Zuleya kwa nyuma.
“Mbona unaonekana haupo Sawa ni ghafla tu umebadilika?”
“Hamna nimekumbuka tu kitu fulani cha nyuma”
“Can you tell me if you don’t mind?”
“Sio muhimu sana ila ni kuhusu Mpenzi wangu wa zamani the way unavyoni care ni kama wewe hakuna tofauti inanipa wakati mgumu sometimes” Aliongea kwa huzuni na kumfanya Zuleya amuhurumie
“Yupo wapi?”
“She is de……” Alishindwa kumalizia sentensi yake na kujitoa kwa Zuleya kisha akaenda kujiinamia sehemu nyingine, Zuleya alijisikia vibaya sana aliacha kupika na kumfuata Carlos na kumkumbatia akijaribu kumfariji.
“Inatosha Carlos jitulize please mpenzi jitahidi sipendi kukuona katika hali kama hii”
Carlos alimgeukia Zuleya na kumtizama kisha akamwambia
“Zuleya ni siku ambayo siwezi kuisahau kwenye maisha yangu nikiwa Uganda baada ya kupata ajali mbaya ya gari na nikashuhudia akiniacha mbele ya macho yangu huku nami nikiwa sina hata nguvu ya kumshika angalau mkono wake tu nilipoteza fahamu hapo hapo”
Ni simulizi ya kusukitisha sana Zuleya alijikuta akimuhurumia sana Carlos kiasi cha kutoa machozi, alishindwa kujizuia kabisa kulia kwani hata Carlos hakuwa kwenye hali nzuri alionekana kupitia mambo mengi magumu lakini hakuwa akijionesha.
Ni wakati ambao Carlos alikuwa akimalizia hatua za mwisho kwaajili ya kwenda Kenya na Sumaya alishaamua kubaki Jamaica kwaajili ya masomo kwani alishapata chuo cha kusoma huko, Zuleya alimueleza ukweli shemeji ya ke Mr Hernad kuhusu mipango yote na Carlos hakumficha jambo lolote na kumueleza kuhusu nia yao ya kutaka kufunga ndoa akikamilisha hatua zote, lilikuwa ni jambo la furaha sana kwa upande wa Mr Hernad kusikia hivyo maana Zuleya umri ulikuwa ukienda mbio sana alikubali juu ya jambo hilo na kuahidi kuwa watampa ushirikiano wa kutosha juu ya hilo.
Tofauti na ilivyokuwa mwanzoni baada ya miezi michache kupita mawasiliano kati ya Sumaya na Lukas yalianza kupungua kidogo kidogo kwa siku walikuwa wakiongea mara moja tena kwa sauti tu sio kama Mwanzoni kila muda tena kwa video call hali hiyo ilimuacha katika wakati mgumu sana Sumaya, na hapo taratibu mawasiliano yao yalizidi kupungua na hata inapita wiki bila kuongea, Sumaya alizidi kupata hali ya simanzi sana na Zuleya alijitahidi sana kumuweka sawa mwanaye lakini haikuwa rahisi kwani kadri siku zilivyozidi kwenda hata mwezi ulikatika bila mawasiliano yoyote baina ya wawili hao, Sumaya alishindwa kuelewa shida ilikuwa nini na hata masomo yake hakuyazingatia ipasavyo kutokana na kuzongwa na mawazo kila kukicha na wakati huo hawakuwa na mawasiliano kabisa licha ya Sumaya kumtafuta Lukas kila siku bila mafanikio yoyote yale.
Ilimbidi Kufanya maamuzi magumu ambayo hakuwahi kuwaza kuyafanya alimpigia simu baba yake.
“Daddy……”
“Sumaya Mbona kama haupo sawa?”
“I’m okay daddy ni uchovu tu,nina habari njema kwako nimekubali kwenda Marekani baba”
“Really?? Sumaya Una maanisha au?”
“Ndio baba we nifanyie mpango tu m nipo tayari kwenda”
“Okay ndani ya wiki hii kila kitu kitakuwa tayari mwanangu”
“Sawa baba, i love you”
“Love you too Princess”
Alikata simu na kuanza kufikiria mengi juu ya kwenda kusoma nchi nyingine na yote ni kwa sababu tu ya mapenzi alihisi kwenda huko labda angeonana na Lukas au mawasiliano yangekuwa rahisi zaidi aliongea na mama yake naye hakuona cha kumshauri zaidi ya kumuacha afanye kile ambacho anaona ni Sawa kwake na hata hivyo zilibaki siku chache waondoke na Carlos kwenda Kenya.Hata hivyo alimshauri asiache kufanya kile anachokipenda Hata kama anaenda kusomea kitu kingine maana Ndio ndoto zake.
Mr Hernad alikuwa na furaha sana baada ya maamuzi ya Sumaya kwenda kusoma kitu ambacho siku zote alipenda mwanaye akasome ili asimamie biashara zake zote kwa sababu hakuona mwingine wa kumuamini zaidi ya mwanaye na pia aliamini anaweza kusimamia vizuri kuliko hata yeye alivyosimamia.
Hakutaka kupoteza muda alifanya mipango yote na hatimaye Sumaya aliondoka nchini Jamaica, hata Carlos na Zuleya baada ya Sumaya kuondoka hawakukaa sana huko nao walielekea nchini Kenya kuyaanza maisha yao mapya.
****************
Sumaya ndani ya nchi nyingine kabisa, Stanford university Ndio chuo ambacho baba yake alimchagulia na aliona kinamfaa mwanaye kwa kipindi chote cha masomo.
Haikuwa ngumu kwa upande wa Sumaya kuzoea kwa haraka mazingira kwani alikuwa ni mtu wa kuchangamana sana na watu japo mwanzoni ilimpa shida kidogo.Baada ya kukamilisha taratibu zote sasa alisajiliwa ndani ya chuo hiko.Kulikuwa na waliotoka mataifa mbalimbali ya Afrika japo hakukuwa na idadi kubwa sana ya waafrika kama ilivyokuwa kwa wazungu.
Alvin naye alikuwa tayari chuoni hapo kwa muda mrefu, tofauti na watu wengine Alvin hakuwa mtu wa kujichanganya sana na watu muda mwingi alikuwa bize na mambo yake licha ya kutopenda kampani ya watu weupe.
Aliketi sehemu akiangalia movie kupitia laptop yake ndogo ya kampuni ya hp, muda huo Sumaya alikuwa na marafiki zake ambao ni Lucia na Lily Walikuwa ni mapacha kutoka Ghana, Fanie alikuwa ni mzungu na Rose kutoka Tanzania.Lilikamilika kundi la watu watano na wote walikuwa sio haba kila walipopita watu hawakuacha kuwatazama hasa wanaume walikuwa wachangamfu na wasio na makuu licha ya kuwa warembo na pia watoto wa vigogo(watu wakubwa) walikozaliwa, waliketi jirani na alipo Alvin.
“Hiiii!” Wote walisalimiana kwa pamoja na hiyo ndio tabia yao, baada ya kusalimiwa Alvin aliinuka na kujibu salamu
“Hi girls!” Alianza kuwaangalia mmoja baada ya mwingine kisha macho yake yalitulia kwa Sumaya kwa sekunde kama tano hivi na ndipo alipoigeukia laptop yake kuendelea kuangalia movie.
“Wow!! He is so handsome!” Aliropoka Lucia ambaye alikuwa na lafudhi ya kighana kabisa na wenzake waligeuka na kumuangalia Kwani alishindwa kujizuia kwa mvuto alionao kijana Alvin.
“Lucia just shut up, unajua atatusikia et, acha tusome kwanza si mnajua tuna mitihani next week” Aliongea Lily kwa kusisitiza na kila mmoja aliinamia laptop yake,
Muda huo akili ya Sumaya haikuwa kwenye kusoma aliwaza mbali sana huku akiangalia picha za Lukas akikumbuka mambo mengi waliyofanya walipokuwa pamoja.
“Maya.. Maya are you okay?” Rose alimuuliza Sumaya kama yuko sawa.
Hapo Sumaya aliinuka na kuondoka bila kusema chochote naye Rose alimfuata nyuma.
THE OATH Sehemu ya kwanza Katikati ya msitu mnene, giza zito likiwa limetanda kila kona ya msitu huo alionekana kijana akikimbia huku jasho likimtoka ni dhahiri alikuwa amekimbia kwa muda mrefu sana na alikuwa na hofu iliyopitiliza huku nyuma sauti tofauti tofauti...
www.jamiiforums.com
Pia mnaweza kufuatilia simulizi yangu mpya nitaipost pia hapa jf
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.