ram
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 9,329
- 8,513
Maskini Adelina....jina la marehemu wifi yangu piaNA MIMI 3
A Story by Elton Tonny
Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA KUMI NA SABA
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Sikuwahi kudhani maisha yangu yangekuja kugeuka kuwa mabaya kwa ughafla namna hii. Mimi Jayden, sasa nilikuwa nimetekwa na mwanamke mwenye kisasi dhidi yangu, na alitoka kufanya jambo zito mno lililoniondolea hamu ya kutaka kuendelea kuishi kabisa. Kila nilipofumba na kufumbua macho, ni taswira moja pekee iliyokuwa mbele yangu, taswira ya jambo baya alilofanya mwanamke huyo kwa mwanamke niliyempenda sana. Bado sikuamini kama yale yaliyotokea yalikuwa yametokea kweli, lakini kumbukumbu zote zilirejea pale pale na kuendelea kuichoma nafsi yangu kila nilipolazimika kuliona tukio lile akilini mwangu.
Iliendelea kujirudia na kujirudia kichwani kwangu, jinsi ambavyo Miryam alikuwa amefanywa. Kutokea ndani ya lile gari, mpaka alipotupwa mbali kwenye lile bonde. Hakukuwa na hisia mbaya zaidi kwangu kuliko kujua yote hayo yaliyompata yalisababishwa na mimi, na hata kutamani muda urudi nyuma ili mambo yabadilike ilionekana kuwa unafiki wa hali ya juu kutoka kwangu. Hakukuwa na mwingine wa kulaumu isipokuwa mimi mwenyewe. Kama ni jambo la kustahili ambalo nilitakiwa kupata sasa, basi ni adhabu kubwa kuwa chanzo cha mateso na kifo cha mpenzi wangu niliyempenda sana, na nilichohitaji kinipate kilikuwa ni kile kile kilichompata yeye ili hatia yote niliyohisi iambatane naye kwa njia iliyostahili.
Sikujua mahali nilikokuwa, lakini najua ilikuwa imepita siku moja kuelekea ya pili tokea Bertha anifanyie kisa kile mpaka sasa. Nilikuwa ndani ya chumba kilichoonekana kuwa kwenye nyumba moja nzuri, kukiwa na mandhari safi, kitanda, sofa, kabati, na vifaa bora vya chumbani kana kwamba iliikuwa chumba cha hoteli za kupangisha. Mikono yangu na miguu ilifungwa huku nikiwa nimeketishwa sofani, na nakumbuka, kwa masaa kadhaa yaliyopita, mmoja wa vikaragosi wake Bertha alikuja kujaribu kunipa chakula eti, lakini sikutaka kula chochote. Sikuwa nimekula wala kunywa chochote kile kutokea usiku niliokuwa hospitalini na mwanangu.
Alijaribu kunilazimisha kwa kuupiga mwili wangu, nile, lakini sikufungua mdomo na kumwacha akinitukana na kuondoka zake. Yaani niliendelea kubaki nimekaa hapo hapo nikifungwa kama mbuzi anayengojea kuchinjwa, mkojo nilioruhusu unitoke ukiwa umeshakaukia kwenye suruali, nikiwa sina hali. Mwili ulihisika kwa namna ovyo sana, lakini ndiyo jambo nililoona linafaa kwa wakati huu na kusonga mbele. Nilitaka kufa, kwa hiyo kama kunifunga kwao ilikuwa ni ili nisitoroke ama nisijiumize wangejua wao, ningeiruhusu njaa hii iniue taratibu tu ikiwa wangechelewesha kuyaleta mauti kwangu. Ndiyo kilichokuwa kimebaki.
Nimeendelea kukaa hapo hapo tu kwa dakika na masaa na masaa, pumzi zikinitoka kwa uchovu mwingi, na likiwa ni jira nisilotambua hata kidogo, mlango wa chumba hicho ukafunguka na viumbe fulani kusikika wakiingia. Hata kwa hali yangu mbaya ningeweza kuelewa hakuwa mtu mmoja, lakini sikujali. Macho yangu yalielekea chini, nikiwa nimeegamia sofa kama vile nguvu zote zimeniisha, ndipo sauti zikaanza kusikika hapo.
"... yuko hivi hivi tokea jana usiku...."
"Nilikaa kumwangalia, yaani ametulia hivyo hivyo..."
"Na hataki kula. Nikamlazimisha, lakini wapi. Nikakiacha hicho hapo mpaka sasa hivi hajakigusa..."
"Angekigusa vipi wakati amefungwa?"
Sauti iliyouliza swali hilo ikatambulika kwangu, na haikuwa ya mwingine isipokuwa Bertha mwenyewe. Leo ndiyo alikuwa amekuja. Ukimya ukafuata baada ya yeye kuuliza hivyo, nami niliendelea kutulia tu nisijali lolote tena. Kisha nikasikia sauti kama ya kiti kuvutwa, kikiletwa karibu nami hapo nilipokaa, halafu nikaona mjongeo mbele yangu ulioonyesha kwamba mtu alikaa hapo. Harufu nzuri iliyoingia puani mwangu ilinijulisha kwamba alikuwa ni Bertha, lakini ilinikera sana. Nikazidi kujihisi vibaya mwilini, nami nikapeleka macho yangu pembeni zaidi kwa kutotaka kumtazama mwanamke huyo.
"Nimefika HB. Pole nimekawia, kuna vitu nilikuwa naweka sawa kwanza. Hope hujani-miss sana," Bertha akaongea hivyo.
Nilimsikia vyema, lakini sikuwa na hisia yoyote ile yenye kunilazimu nijali chochote hapo.
"What is this, nasikia unagoma kula wakati kinatengenezwa chakula poa kabisa? Umeanza lini tabia mbaya?"
Kicheko laini kilisikika kutoka kwa watu wake hapo, akiwa ameniuliza kwa kejeli nyingi.
"Kwa hiyo nini... unataka kujiua HB?" Bertha akauliza hivyo.
Nikaendelea kunyamaza zangu.
"Look at you... hivi wewe... daktari eti, unakataa kula kisa nini? Halafu unajikojolea? Unataka nini, attention?" Bertha akasema hivyo.
Nikabaki kama nilivyokuwa.
"Oooh... hii yote kwa sababu baby mama wako mtarajiwa ameenda kuionja kuzimu eh? Ndiyo maana umesusa? Na uneninunia?"
Kauli yake ikanifanya nifumbe macho baada ya kumbukumbu ya Miryam kunirudi kichwani.
Bertha akabana kicheko laini na kusema, "Usiwe hivyo bwana. Ona... usinune kwa sababu ya hilo, haina maana tena HB. Mimi niko hapa, na ninamleta mtoto wetu ndani ya miezi michache tu. Kwa nini unahuzunika sasa? Unapaswa kuwa na furaha jamani."
Ikiwa ningetaka, ningeweza hata kumtemea mate usoni, na nasema hivyo huku nikijua mate yalikuwa yamekauka, lakini kejeli zake hazikunipa maumivu zaidi ya yale aliyokuwa ameshanipa. Alikuwa akijisumbua tu.
"Ona baby, nimekuletea chakula kizuri. Tena... nimepika mwenyewe, si mmeona nimekipika jamani... nimempikia baby wangu?"
Bertha alisema hivyo kama kuwaambia na wengine waliokuwemo, na nadhani wangempa kichwa kwa kukubali. Njia yake ya kuongea ilionyesha alikuwa anafurahia sana kuanza kunitesa namna hii, na naona hali yangu mbaya ilikuwa inampa mridhiko wa hali ya juu. Ila najua pia hakuwa amemaliza, lakini nilikuwa mbali mno kujali tena alichotaka kunifanyia kwa zamu hii.
"JC..." akaniita.
Nikabaki kimya tu.
"Niangalie," akasema hivyo.
Ni kama alikuwa akiongea na mfu tu hapa.
"Kwa hiyo hutaki kuniangalia?" akauliza.
Kimya.
"Niangalie!" akafoka kwa sauti ya juu.
Sijui nini kilifuata baada ya hapo, lakini sikumwangalia, ila nikahisi hatua zikija karibu nami lakini zikakatishwa.
"No, it's okay. I got this..." Bertha akasema hivyo.
Ni kama alikuwa anamzuia kikaragosi wake mmoja asije kunigusa, labda kunilazimisha nimwangalie madam wake.
"Well... hutaki kuniangalia nikikubembeleza, basi sawa. Ngoja nitumie fimbo," Bertha akasema hivyo.
Kama alitaka kunichapa, basi ningepokea hizo fimbo zote, lakini nisingemwangalia.
"Sihitaji kukupa motivation kubwa sana ili unipe nachotaka, but with you nimeshagundua huwa hautembei mpaka usukumwe. Hope this will do the trick..." akasema kwa sauti tulivu.
Alikuwa na maana ya kutaka kuniumiza ili nimpe alichotaka, lakini mimi hapo ndiyo nilihitaji aniumize alivyotaka na nisingejali. Sema, maumivu aliyotaka kuyaleta kwangu yangekuja kwa njia ambayo nisingetarajia kabisa, kwa sababu sikujua aliwaza nini. Nikiwa nimekaa namna hiyo hiyo, Bertha akaanza kuweka vitu fulani vilivyoonekana kuwa karatasi kwenye mapaja yangu, akiwa kama anavibandika kwa nguvu, mara nne, na macho yangu yalipofanikiwa kuona kilichokuwepo hapo, yakatanuka kiasi. Zilikuwa ni picha, na ni picha ambazo nilipoelewa zilimaanisha nini, nikajikuta nameza mate ndani ya koo langu kavu kwa hisia mpya ya msisimko iliyoniingia. Msisimko mbaya.
Picha ya kwanza ilionyesha kichwa cha mtu kilichokatwa, mwanaume, na huyo alikuwa ni Bobo! Picha ya pili ilionyesha mwanamke mmoja asiyekuwa na nguo mwilini, akiwa ameshikiliwa na wanaume watano walio uchi pia, na picha ya tatu ilionyesha wanaume hao wakiendelea kumshikilia mikono na miguu, mmoja akimwingilia kimwili kupitia kitoweo chake, mwingine nyuma yake, na mwingine mdomoni mwake, halafu ya nne ikaonyesha mwanamke huyo akiwa ametundikwa kwa kunyongwa huku mwili wake ukionekana kutapakaa damu, ndani kwake, na huyo alikuwa ni Adelina!
Nilihisi pigo zito sana moyoni. Nilishtuka! Macho yangu yakakaza hapo zaidi, nikiwa nimeganda tu kutazama picha iliyomwonyesha Adelina akiwa amenyongwa, na aisee! Nguvu zikaniishia. Sikuwa hata na muda wa kufikiria nini wala nini, yaani kile nilichokiona kilipita unyama wowote ambao nilidhani Bertha angenifanyia. Nilichoka mno. Eh Mungu wangu!
Nikasikia Bertha anasafisha pua yake, kisha akasema, "Niangalie."
Macho yangu hayakuwa na budi sasa kupanda na kumwangalia mwanamke huyu, na nilikutana na uso wake usiokuwa na aina yoyote ya hisia za majuto, wala hofu, wala huruma, bali ni kuridhika kabisa na kile alichotoka kunionyesha.
"Sasa je? Kama mtoto mzuri," akasema hivyo.
Niliingiwa na huzuni zaidi sasa, nikibaki kumtazama kwa mkazo huku midomo yangu ikitetema. Kulikuwa na watu kama wawili waliosimama nyuma yake.
"Umeonaje chakula nilichokuletea?" Bertha akauliza hivyo.
Nikaendelea kumtazama kwa hisia za maumivu.
"Oh, lazima umeona ni kitamu, maana mwanzoni ulikuwa hutaki kuniangalia, ila nilipokusogezea ndo' motivation ikakuingia hahahah..." akaongea hivyo kwa sifa na kucheka.
Wenzake wakacheka pia, na mimi nikiwa nimekabwa na huzuni, nikafumba macho na kufumbua, machozi yakianza kunijaa.
Bertha akaweka uso makini, naye akasema, "Najua unawaza 'kwa nini unafanya hivi Bertha?' 'Kwa nini umeamua kufanya hivi?' 'Why?' 'ohohooouu...' Ahahahah... ni kwa sababu yako, JC! COME ON!!"
Aliiongea kwa kejeli na mkazo mwingi, nami nikaendelea kumtazama kwa umakini.
Akanyanyua kidole na kuonekana kutaka kusema kitu fulani, lakini akaishia kushusha pumzi na kufumba macho yake, kisha ndiyo akasema, "Sitaongea sana. Najua una njaa, so nimekuja kukupa option mbili leo."
Alizungumza kwa njia yake makini wakati huu, na mimi hapo kusema kweli nilikuwa nimeshauelewa mchezo wake wote aliotaka kuufanya, hata ingawa sikuyajua makali yake. Akafanya kuelekeza kiganja chake kwa mmoja wa watu wake hapo, na ikiwa ni mwanaume, akampatia vitu vilivyoonekana kuwa picha zingine. Sikuweza kuzuia hisia zangu kupandisha hofu zaidi kwa kuwa najua angenionyesha vitu vibovu zaidi, na kweli ikawa hivyo, lakini kwa njia tofauti.
Bertha akanionyesha picha ya kwanza, nami nikaiangalia na kutambua mtu aliyekuwepo hapo kuwa mama yangu. Akaitupa na kunionyesha ya pili, nayo ilimbeba Jasmine. Ya tatu, ikawa ni Mariam, ya nne ikawa ni Tesha, ya tano ikawa ni Nuru, na ya mwisho, ikawa ni Evelyn. Zote zilikuwa picha safi, yaani, hakukuwa na mambo yoyote mabaya yaliyoonekana hapo kama kwenye picha za Bobo na Adelina, nami nikajikuta nadondosha machozi nikiwa naiangalia picha ya mwanangu iliyoendelea kushikiliwa vidoleni kwa mwanamke huyu mkatili.
Bertha akasema, "Two things. Moja, ufate KILA kitu nitakachokwambia ufanye kuanzia sasa, au mbili, kataa kufanya hivyo, na hawa wote uliowaona wanakenua hapa nitawageuza kuwa vyakula vya mbwa kama hao machangudoa wako wawili, na... sijui kama Bobo alikuwa ni swahiba wako kabisa, ila... you get it. Nitawaua wote."
Nikafumba macho na kuinamisha uso kwa kuhisi maumivu mengi moyoni. Nilichokuwa najitakia mwenyewe kutokea hapa killionekana kutonitaka mimi, yaani Bertha aliamua kuninyima hata haki ya kutaka kufa. Alitaka niendelee kuishi ili kila siku anifanye nihisi ni namna gani aliniweka kuwa mwanasesere wake chini ya kiganja chake.
"Kwa hiyo utachagua nini... handsome?" Bertha akauliza hivyo.
Nilihisi unyonge wa hali ya juu, na hisia za kustahili haya yote zilinilemea, lakini siyo kwa namna aliyoileta Bertha kwangu. Ilikuwa na ulazima gani kumuua mtu ambaye hakumkosea lolote, kumfanyia unyama mwanamke ambaye hata hakumjua ili tu anilipizie kisasi mimi, na kisha kumuua pia? Kwa nini isiwe mimi ndiye ambaye angenifanyia mambo hayo? Iliniuma sana.
Vifo vya watu hao niliowapenda na kuwajali vilikuwa ni makosa yangu, na sasa kama sikutaka vingine viongezeke kwa wengine, ingenibidi nikubali kufanya aliyotaka mnyama huyu ili kuwaokoa wasiokuwa na hatia. Najua hakutaka nikatize uhai wangu upesi ili aendelee kufurahia kuona nilivyoteseka, na kutokea hapa sikuwa na njia nyingine ya kukataa alichokitaka kutoka kwangu. Kama kuwa mtumwa kwa mateso, ningekuwa mtumwa wake tu. Hakukuwa na namna.
Alikuwa bado ameishikilia picha ya Evelyn, mimi nikiwa sijatoa jibu kwa swali lake, naye akasema, "Okay. Kama unahitaji muda zaidi wa kufikiria, nitakuacha ufikirie. Labda... hao wawili hawajatosha..."
Nikamwangalia machoni baada ya yeye kusema hivyo.
Akawa anaiangalia picha ya Evelyn kiufikirio, kisha akasema, "Niongeze mmoja, au wawili hivi ili nikupe motivation zaidi ya kutoa jibu. Nitaanza na huyu."
Aliongea hivyo huku akinionyeshea picha hiyo ya Evelyn, nami nikajipa nguvu kiasi na kujivuta, nikiuweka mwili wangu sawa ili nimtazame kwa namna makini zaidi. Alibaki akiniangalia kwa namna ya kutojali kabisa, mimi hapo machozi bado yakinitoka kama mtoto bila sauti ya kilio.
Nikafumbia mdomo, Bertha akionyesha subira ya kunisikia naongea, nami nikasema, "Unataka nini?"
Sauti yangu ilikuwa ya chini sana, na sasa nilikuwa nimejipa nguvu kidogo tu ya kumwonyesha kwamba nilichagua jambo la kwanza alilonipa nichague kati ya yale mawili. Sikupatwa na hisia yoyote zaidi ya maumivu kwa kila kitu nilichowazia kimetendeka na ambacho kingefanyika baada ya hapo lakini nilikuwa tayari kwa mengine yote isipokuwa watu niliowapenda kuumizwa kwa sababu yangu.
Bertha akatabasamu kiasi, kisha akaanza kucheka kwa namna iliyoonyesha furaha tele. Akaiangalia picha ya Evelyn tena na kusema, "Men are so weak. Uko tayari nikuue wewe, lakini paka wako akinyooshewa panga unanywea. That's so f***** gross."
Nikaangalia chini na kusema, "Niambie. Unataka nini? Nitafanya..."
Bertha akauliza, "Sure?"
Nikajitahidi kutikisa kichwa na kusema, "Ndiyo."
Akatulia kwanza akiniangalia kwa hisia makini, kisha akatikisa kichwa kukataa na kusema, "Naah. Haujanishawishi. Ahah... bado nahisi kama napaswa kukuongezea moti...."
Nikajivuta zaidi kujitoa sofani hapo, nikiwa na nia ya kutaka kupiga magoti ili nimwombe nikiwa chini yake, nami nikaangukia sakafuni nikiwa sijiwezi vizuri kutokana na uchovu na maumivu ya mwili. Nilianguka chini hapo na kuzilalia picha alizokuwa ametupa, mikono na miguu ikiwa imefungwa bado, na katika hali yangu mbovu nikaanza kujitahidi kuunyanyua mwili ili hayo magoti yapigwe. Najua ilimpa raha sana Bertha kuniona nilivyosumbuka hapo chini kujigeuza na kujigeuza hadi nilipoweza kupiga magoti kwa upande, nikiegamia mikono kwa chini na kumtazama kwa njia iliyoonyesha kweli nilitaka kumfanya ahisi ninamshawishi.
Hapa hakukuwa na nafasi ya kuweka ujeuri wa aina yoyote. Nilikuwa sitaki kumwacha aendelee kujipa kichwa zaidi maana tayari nilielewa alichokuwa akikitaka, kwa sababu nilimjua vizuri sana. Yote aliyokuwa amefanya, yalikuwa kuniumiza si kwa sababu tu ya niliyomtendea kipindi kile, ila kwa sababu alikuwa ananipenda. Upendo uliochochea chuki kubwa kunielekea. Kwa hiyo, ningefanya kila alichotaka kuhakikisha anawaacha kabisa wapendwa wangu. Na sijui kihalisi alitaka nini, ila JC nilikuwa tayari kumpa. Sikuwa na namna tena. Miryam alitoweka, Adelina dada wa watu alitendewa vibaya sana na kuuliwa pia, Bobo... yaani! Ilitosha.
Nikafungua kinywa changu tena na kusema, "Fanya lolote unalotak... hh.. hhh... juu yangu... mimi. Usiumize mtu m-mwingine... hh.. zaidi. Nakuomba... hhh... nitafanya yote unayotaka."
Bertha akabaki kunitazama kwa hisia makini, kisha akasema, "Natamani ingekuwa rahisi."
"Bertha..." nikaishia kutaja jina lake.
Akaangalia pembeni.
"Nachagua kufanya kila kitu... utakachotaka. Kila kitu. Nitafanya. Tafadhali... usiwaumize wengine... hhh... nakuomba..." nikaongea kwa hisia sana, machozi yakinitoka.
Bertha akarudi kuniangalia na kunikazia macho yake, akionyesha aina fulani hivi ya hasira kali, na kwa sauti ya chini akasema, "Tusingefikishana huku JC, kama tu ungekuwa halisi na mimi. Nilikuwa tayari kukupa kila kitu. Everything. Why? Kwa nini ulinifanyia vile? Huh?"
Nikaendelea kumtazama kwa hisia za huzuni.
Akatikisa kichwa kwa njia iliyoonyesha kukerwa sana, naye akasema, "Sawa. Unachagua kufata kila nitakachokwambia ufanye, si ndiyo?"
Nikatikisa kichwa kukubali.
Akasema, "Okay. Kuanzia sasa... wewe utakuwa mbwa wangu. Unanisikia? Nani?"
Nikaangalia chini na kusema, "Mbwa wako."
"Sikusikii..." akasisitiza.
Nikamwangalia machoni na kusema, "M-mbwa wako."
"Yeah. Wewe ukiwa mbwa wangu, utapaswa ufanye nini?" akaniuliza.
Nikasema, "Nitafanya kila kitu unachotaka."
"Ahahaha... 'nitafanya kilo kitu unachotakoh' huna hata aibu?" Bertha akaongea kwa kejeli.
Nikaangalia chini kwa kufadhaika.
"Well, kama utafanya kila kitu ninachotaka... anza kuthibitisha hilo. Sasa hivi," akaniambia hivyo.
Nikamtazama machoni tena, nikiwa naelewa angetaka nifanye jambo fulani lenye kumpendeza, lakini sikujua la kumfanyia. Ila yeye tayari alikuwa na wazo. Hapo hapo akamtikisia kichwa mmoja wa watu wake pembeni, na ndiyo kumwangalia mwanaume huyo nikaona alikuwa ameshika kitu kama hotpot ndogo mikononi mwake. Akasogea upande wangu na chombo hicho, kisha akakiweka chini karibu nami na kutoa kisu kidogo kutoka kwenye mkanda nyuma ya kiuno chake. Akaivuta mikono yangu na kuzikata kamba ngumu nilizofungwa, akiipa mikono uhuru sasa, kisha akasimama na kurudi nyuma yake Bertha. Nikamtazama mwanamke huyo usoni na kumwona amenikazia macho tu, na eti hilo ndiyo likawa jambo la kwanza alilotaka nifanye. Nile.
Hisia mbaya zaidi ziliniingia, kwa kuwa chombo hicho hakikufunuliwa, hivyo najua Bertha alitaka mimi mwenyewe nifunue ili nikutane na ishu fulani mbovu sana ambayo ingepima kama kweli nilimaanisha kile nilichomwambia. Kama hakikuwa chakula cha kawaida basi ni lazima niliwekewa uchafu wa aina fulani humo kabisa, lakini kwa jinsi mambo yalivyokuwa, nisingeacha kufanya alichotaka hata kama ingenigharimu vipi. Yote yangekuwa kwa yote. Huku mwanzo wa viganja kukiwa na maumivu ya kamba zilizoondolewa, nikanyoosha mkono kuushika mfuniko wa hotpot hiyo, kisha nikauondoa hapo na kubaki nimekitazama chakula kilichokuwepo humo. Wali, nyama, na hata ndizi mbivu.
Nikamwangalia Bertha usoni, naye ndiyo akasema, "Kula. Ama vipi? Unafikiri kuna sumu? Au ulidhani ni nyoka?"
Nikaendelea kumtazama tu.
"Ule. Umalize. Ndiyo tutaanza kuongea kuhusu nini nataka," akasema hivyo.
Hapo alionekana kuweka kituo kikubwa kabisa, na bila kungoja lolote, akasimama mbele yangu na kutumia sekunde chache akiniangalia kwa umakini. Nikashindwa kuacha kumtazama yeye alipoendelea kusimama tu namna hiyo, na ile ameangalia pembeni kwa namna iliyoonyesha kukosa subira, nikakivuta chombo karibu nami na kuanza kujilazimisha kula chakula alichokuwa amenipatia, viganja vikitetemeka haswa. Nilikula upesi, nikijaza mdomo na kutafuna huku narudisha macho yangu kumtazama yeye, kumwonyesha kwamba nilikuwa nimeanza kufanya aliyoyataka, naye Bertha akaniangalia kwa njia iliyoonyesha dharau sana na kisha kuanza kuondoka sehemu hiyo; akifuatwa na wanaume waliompa ulinzi.
Ni baada tu ya wote kutokomea ndiyo hisia zikanilemea zaidi, nami nikaanza kulia kwa kuhisi hatia nyingi moyoni. Picha ambazo Bertha alinionyesha zilikuwa hapo chini sasa, na nilipoangalia zile zilizoonyesha ukatili aliokuwa ameufanya, nikashindwa kuendelea kula na kubaki nalia kwa maumivu tu. Nikahisi mtetemo mwilini uliofanya nilegee zaidi na kujilaza chini hapo, nikiishika picha ya Adelina na kuikaza karibu sana na moyo wangu. Mwanaume mtu mzima lakini nililia haswa. Kwa nini maisha yangu yalikuja kuwa hivi? Mbona ni kama nilikuwa ndani ya sinema? Na haya yote yangekuja kuisha namna gani? Nilikata tamaa kabisa.
★★★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★★★
Whatsapp +255 678 017 280