SIMIYU: Mkuu wa Mkoa amfuta kazi Mhandisi wa Mkoa

Mpaka wajitambue washafukuzwa wengi. Watumishi wengi bado wanaishi "jana"
 
Ila swali ninalojiuliza mie, ina maana huyo Makonda wa mkoa wa Simiyu huwa hakagui hiyo miradi ya mkoani kwake mara kwa mara mpaka Mtukufu aje huko kukagua..?
 
Dili lilikuwa LA wote . Kimenuka inabidi kondoo was kafara apatikane. Pole yake
 
Huu ni uonezi mkubwa sana ,,Raisi asinge kuja hapo hii habari isngekuwepo.. kweli Raisi unakazi ngumu kama wasaidizi wako ndo hawa.
 
Kwa uelewa wangu kidogo RC hawezi kumfukuza kazi mtumishi yeyote siyo mamlaka yake ya nidhamu, RAS ndiyo mamlaka ya nidhamu, kabla ya kuandika tuwe tunafanya utafiti kidogo, kuna vijana wa sekondari humu ndani tutakuwa hatuwasaidii kwenye civics.
Hajamfukuza kamsimamisha tu
 
Let me put this thing clear;

Huyo Muandisi anaweza kushinda hii kesi kwa in a simple way kabisa; na hii ni kama ifuatavyo;

1. Kisheria kabisa muandisi(Engineer) hapaswi kuaandaa makaadirio ya ujenzi..this is out of his professional..

Makadirio ya ujenzi yanafanywa na Quantity Surveyor(Qs), huwezi kumpa kazi Structural Engineer akaandae BOQ wakati hana skill ya estimating, hana skills za kutake-off.

Sasa utakuta hiyo Str.Engineer ndo kama Architect, yeye kawa Qs, yeye kawa Service engineer, yeye kawa Structural engineer, yeye kawa Geotechnical Engineer..

Lazima angekosea tuuu! No way..

2.Pili, kuhusu kudesign..Structural engineer ni expert kwenye structural na sio Architectural design..hiyo ishu ya 3D( yaani Three dimension) ya kazi ya msanifu wa Jengo (Architect) . Huwezi kumhold liable wakati amepewa kazi ambazo sio zake lazima angekosea tuu...

Ni sawa , kumpeleka mgonjwa wa jino kwa daktari ngozi..! Dkt. Wa ngozi anaweza akavunja jino badala ya kuling'oa

Na pia:
To my experience, Halmashauri zetu hazina Architects ,hazina Quantity Surveyors wala service Engineer...utakuta kuna Structural Engineer na Technicians basi na kazi zinatakiwa ziendelee...! Huu ni ujinga..


Huyo Engineer atafute tuu watu wanaolewa namna hizi construction discpline zinavyofanya kazi...anarudi kazi kama kawaida..
 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amsimamisha kazi mhandisi wa mkoa baada ya kunabainika alimdanganya Rais kuhusu ujenzi wa Hospitali.


=====
Mhandisi wa Ujenzi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu, Deusdedit Mshuga amesimamishwa kazi kwa kukabiliwa na mashtaka matatu.

Akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa, Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini amesema Mhandisi huyo anashtakiwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu aliyopewakwa kiwango cha kuridhisha.

Alisema akiwa mtumishi wa umma kinyume na kipengele cha 8 cha sehemu"A" ya jedwali la kwanza la kanuni za Utumishi wa Umma, Tangazo la Serikali Na.168/2003; mtumishi huyo alishindwa
kuandaa makadirio ya gharama za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa yenye uhalisia.

Aliandaa makadirio ya Tsh46,1 yaliyosomwa mbele ya Mhe. Rais tarehe 11 Januari,2017 ambayo ni juu kuliko uhalisia.

Shtaka la pili ni kufanya uzembe mkubwa wakati wa utekelezaji wa majukumu ya kazi iliyopewa kinyume na kipengele cha 13 cha sehemu "A" ya jedwali la kwanza la Kanuni za Utumishi wa Umma,Tangazo la Serikali na 168/2003;

Alitaja (1) kuandaa makadirio ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa Tshs.46,106,456,000 hali iliyosababisha Mhe Rais kusomewa taarifa ya gharama zisizo na uhalisia na(2) Kuandaa michoro ya taswira (3 D)isiyoendana na michoro halisi ya Hospitali ya Mkoa iliyooneshwa mbele ya Mhe.Rais

Shtaka la tatu ni kufanya kazi kwa kukiuka maadili ya taaluma yake wakati wa utekelezaji ya kazi aliyopewa kinyume na kipengele cha 14 cha Sehemu "A" ya Jedwali la kwanza la Kanuni za Utumishi wa Umma, Tangazo la Serikali Na.168/2003:- kwa (1) Kuandaa makadirio ya shilingi 46,106,456,000 ya gharama za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa bila kuzingatia mita za mraba za eneo, michoro na kusababisha gharama kubwa zisizo na uhalisia
(2) Kuandaa makadirio ya shilingi 3,009,640,000 yasiyo na uhalisia ili kugharamia ujenzi wa majengo ya msingi kuwezesha Hospitali kuwa "functional" kwa kupiga simu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Pichani ni Katibu Tawala Mkoa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini (mwenye koti jeusi) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka mwenye tai wakizungumza na viongozi na watumishi wa Sekretatieti ya Mkoa wa Simiyu katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.


Zengwe kama hili hili Lipo Hospitali inayojengwa pale Shinyanga Mjini.

Yaani hawa wahandisi wanafaa kuning'inizwa.

Yaaani ni sheeeedah.
Nalitafuta gepu siku moja nifyatuke mbele ya JPM
 
Huyo mkuu wa mkoa alikuwa wapi kabla ya safari ya raisi?
Hakukuwa na maandalizi ya nini kitakuwa presented kwa mkuu wa nchi?
Huyo RC hakupitia taarifa hiyo kabla haijasomwa?
Kwa nini raisi asianze na RC kwanza?
Taarifa ya uongo imetolewa kwa raisi RC ukiwepo halafu unaanza sanaa...collective responsibility hivi inakuwaje?
Utumishi wa umma sasa umekuwa mgumu
 
Back
Top Bottom