Simike, Mbeya: Ajali ya Lori na Coaster yasababisha vifo zaidi ya Watu 16 na kujeruhi wengine 18

pmwasyoke

JF-Expert Member
May 27, 2010
4,724
3,240
Kuna taarifa ya ajali ambapo inasemekana lori limeigonga Coaster iliyotokea Tunduma kuja Mbeya eneo la Simike. Mchana huu.

Inasemekana kuna vifo kadhaa.

----===========

Hii ajali imetokea leo mlima wa Simike Mbembela mkoani Mbeya na kuuwa watu 13 na kujeruhi watu 18, Chanzo cha ajali ni baada ya Lori kufeli breki kwenda kugonga Costa, guta, bajaji na pikipiki na kusababisha vifo na majeruhi.

RPC Mbeya amethibitisha.

s1.jpg

Screenshot 2024-06-06 100353.jpg

Screenshot 2024-06-06 100332.jpg

================

UPDATES...
Taarifa zinazoendelea kuripotiwa kuhusu ajali ya gari aina ya Coaster Jijini Mbeya hapo jana Juni 05, 2024 katika mteremko wa Simike vifo vimeongezeka kutoka 14 mpaka hivi sasa watu 16 wamefariki Dunia.

Taarifa hizi zimethibitishwa na Dkt Godlove Mbwanji ambaye ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.
 
Ndugu zangu watanzania,

Ajali Mbaya sana imetokea mkoani Mbeya na kuuwa watu na majeruhi zaidi ya 17. Ni ajali Mbaya sana iliyotokea eneo la Nzovwe baada ya Loli kuonekana kufeli breki na kupoteza muelekeo na hivyo kugonga gari ya abiria aina ya Costa inayosemekana ilikuwa inatokea Mkoani Songwe.

Mungu atusaidie tu maana ajali zinachukua maisha ya watu wengi sana na kuacha simanzi kwa familia.ni machozi matupu na huzuni kwa wana Mbeya.
 
ni kwamba madereva wengi hawana mafunzo? breki zikifeli kuna namna wanaelekezwa kuminya emergency brake pindi breki za kawaida zinapofeli.
 
Kuna taarifa ya ajali ambapo inasemekana lori limeigonga Coaster iliyotokea Tunduma kuja Mbeya eneo la Simike. Mchana huu.

Inasemekana kuna vifo kadhaa.
----
Hii ajali imetokea leo mlima wa Simike Mbembela mkoani Mbeya na kuuwa watu 13 na kujeruhi watu 18, Chanzo cha ajali ni baada ya Lori kufeli breki kwenda kugonga Costa, guta, bajaji na pikipiki na kusababisha vifo na majeruhi.

RPC Mbeya amethibitisha.

View attachment 3009467View attachment 3009466
Impact inaonekana ilikuwa kubwa mno coster haifai kabisa. Mungu arehemu nafsi zao
 
Bongo kila uzembe dereva anasingizia kufeli breki na kweli anaachwa eti kisa breki ilifeli. Mambo ya hovyo sana.
Mwaka Juzi dereva mmoja Marekani aliua watu 4 kwa kusingizia brake failure, akajikuta anakula miaka 110.

Wenzetu wana watu wa machanics wanapeleka gari gereji inapimwa kuonyesha kama kweli kulikua na brake failure. Bongo watu wanaua watu na waanchiwa kwa kisingizio cha brake failure.

Back
Top Bottom