Simba SC yailaza Ruvu Shooting, yabaki kileleni kwa tofauti ya alama nne

Sisi tunajua wapi atakwama simba kanda ya ziwa toto ipo bado ligi kuu halafu kuna simba na yanga halafu simba na azam simba na mbao
Yanga hachezi na Simba, wala hatacheza na Mbao wala hatacheza mechi yoyote mkoani, na atashinda mechi zake zote
 
Sisi tunajua wapi atakwama simba kanda ya ziwa toto ipo bado ligi kuu halafu kuna simba na yanga halafu simba na azam simba na mbao
Simba ya mwaka huu haina ugenini.. popote ni nyumbani.. Sijui Baba na Mwana, Ndala na Toto, Mbao, Azam n.k.. Lazma tuwaadabishe, haijalishi tutachezea wapi
 
Hivi hizo timu ulizozitaja timu ipi iliifunga Simba raundi ya kwanza?Hizo ngonjera ohh watakwama mikoani tumeshazoea. Njoo na umbea mwingine.

Hakuna hata moja Mkuu.. Cha zaidi ni mmoja tu hapo aliambulia sare baada ya muamala kuthibitishwa.
 
Uwezo wa kufikiria wa Waafrika ni mdogo mno. Ebu tujiulize umuhimu wa Simba kumbakisha Blagnon ni nini hasa? Au kuna sehemu imeandikwa lazima uwe na wachezaji 7 wa nje? Kwani ukiwa nao 5 au 6 kuna faini toyote? Eti unamlipa Blagnon au Mavugo pesa kibao unaogopa kumpa hata nusu ya pesa zao mchezaji kama Victor Hangaya au Mandawa? Waafrika tuna matatizo makubwa sana
 
Mkuu kama nia yako ni kujenga nitakuwa nimekuelewa.Kuna wachezaji inatake time kuzoea timu na mpira unaochezwa. Blagnon sio mchezaji mbaya na anapewa muda kuonyesha umahiri wake. Mavugo hajalipwa pesa nyingi unazodai. Mandawa Simba ilijaribu kumsajili lakini Mtibwa wakakataa kata kata kwani ndio msimu huu amesaini na ana mkataba wa muda mrefu.Mara zote huwezi ukapata wachezaji unaowataka. Hata timu kubwa huwa zinapata matatizo hayo.
 
Pastory Athanasi bado hajafit kwenye mfumo.Kuna haja ya kubadili mfumo ili stricker wapate pass za mojakwa moja.Huu mfumo unalinda mno hadi nguvu ya kushambulia inakua ndogo_Omogi afanye namna ya kubadili mfumo kidogo hapo mbele.
 
Back
Top Bottom