Simba SC 'tumezubaa' sana, 'tunakomolewa' huku Yanga SC ikitumia mwanya huu 'Kujiimarisha' 'zaidi 'Kimkakati' ili kuwa 'Mabingwa wa NBC Premier League

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
60,044
119,619
Kwa masikitiko makubwa Asubuhi ya leo nilianzisha Uzi hapa JamiiForums nikisema kuwa Kitengo cha Umafia Simba SC Kinepwaya na kwamba nipewe Mimi na Wenzangu Sita (6) na Yanga SC hatokuwa Bingwa kwa Mshangao huo Uzi siuoni (kwa Lugha sahihi ni kama vile Umefutwa) kwasababu wazijuazo Walioufuta.

Ni kwamba kwa sasa naona Mapungufu makubwa ya Kimkakati (Kimafia) ndani ya Klabu yangu ya Simba kiasi kwamba Yanga SC wameshaanza kuyatumia Kujinufaisha nayo na wanaelekea Kufanikiwa.

Kitengo cha Umafia ( Mikakati ) cha Simba SC kingekuwa imara kamwe Mchezo wetu na Mtibwa Sugar FC usingepelekwa Manungu ila kutokana na Kuzubaa Kwetu, Kujisahau na Kuridhika TFF (hasa Bodi ya Ligi) kwa Kushirikiana na Yanga SC na Matajiri wao GSM sasa wanatumaliza tu.

Viongozi wa Simba SC waliomba Mechi isichezwe Manungu wamekataliwa kwa Kigezo kuwa Uwanja ni mzuri ila Yanga SC wameomba Mechi yao isichezwe Uwanja wa Ushirika na ikachezwe Sheikh Amri Abeid Kaluta Arusha wamekubaliwa wakati hali ya Uwanja wa Manungu ni sawa na ya Uwanja wa Ushirika.

Walichokifanya Yanga SC ni kupitia kwa Mtu ( Shabiki ) wao mkubwa IGP Sirro ili Kumshawishi ahakikishe Mevhi haichezwi Ushirika na kwa Kuzuga ( Kutuzuga ) Jeshi la la Polisi wakaja na Taarifa ya Utetezi kuwa Mchezo huo umehamishwa Ushirika kwakuwa Uwanja utatumika kwa Shughuli za Kijeshi wakati si kweli ila ni Mpango Maalum wa kuitengenezea Yanga SC Mazingira ya Ushindi.

Viongozi wa Simba SC wasichokijua ni kwamba baada ya Kutunishiana Misuli kwa CEO Barbara Gonzalez na Mwenyekiti wa Simba SC ( Wanachama ) Murtaza Mangungu na TFF pamoja na Bodi ya Ligi ( TPLB ) wametengeneza Bifu Kubwa ambapo Yanga SC na GSM yao wameamua Kutumia mwanya huu ( huo ) kwa Kuwahonga baadhi ya Viongozi wa TFF na TPLB ili waikomoe Simba SC ili iangushe ( ipoteze ) Alama ( points ) na Yanga SC aweze Kutuacha kwa mbali sana na ikiwezekana atangaze Ubingwa mapema mno na kwa GENTAMYCINE ninavyoona na Kuyasikia naliona hili Kufanikiwa.

UMAFIA ninaoumaanisha hapa unahusu Mambo Makuu matatu ambayo ni...

1. Rushwa
2. Uchawi
3. Propaganda

Najua kwa Wageni wa Soka la Bongo hapa mtanishangaa GENTAMYCINE, ila kwa wale Watu wa Mpira naamini wamenielewa na wala hapa tusifichane Klabu za Simba na Yanga Mafanikio yao ya Uwanjani Kitakwimu ni kama ifuatavyo.....

1. Rushwa....45%
2. Uchawi...40%
3. Propaganda....10%
4. Uchezaji...5%

Simba SC mpaka tuje Kushtuka kuwa tunahujumiwa na TFF na TPLB huku Yanga SC na GSM yao wakiutumia mwanya huu ( huo ) Kujinufaisha Kiushindi tayari Yanga SC watakuwa Mabingwa wa NBC Premier League Msimu wa 2021 / 2022.

Simba SC tuendeleeni tu Kuzubaa sawa?
 
Aisee leo umenifumbua macho mkuu, Kumbe kwa miaka minne mfululizo Simba amechukua ubingwa kwa hizi mbinu ulizotutajia hapa chini?
Rushwa 45%,
Uchawi 40%
Propaganda 10%
Uwezo wa kiuchezaji 5%
Subili wale mbumbumbu wenzako wasiojua kutumia akili zao vizuri watakavokushambulia kwa Mada hii iliyojaa ukweli mtupu
 
Aisee leo umenifumbua macho mkuu, Kumbe kwa miaka minne mfululizo Simba amechukua ubingwa kwa hizi mbinu ulizotutajia hapa chini?
Rushwa 45%....
Yanga SC wakati wa Rais wa TFF akiwa Jamal Malinzi walibeba Ubingwa mara Nne ( 4 ) Mfululizo kwa UMAFIA huu niliouelezea hapa.

Simba SC yangu pamoja na kuwa Bingwa mara Nne ( 4 ) mfululizo na kufanya vizuri Kimataifa ila na yenyewe ilifanya UMAFIA huu.

CEO wa Azam FC Popat aliwahi Kunukuliwa kuwa alishaambiwa na Mwamuzi Mmoja kuwa wakiendelea kuwa Wabahili ( Walugume ) Ubingwa wa Ligi nchini watausikia katika Bomba tu kwani Wenzao wa Simba na Yanga wanawahonga ( wanatoa ) sana.

Binafsi GENTAMYCINE nina Mwamuzi Mmoja Rafiki yangu ananiambia huwa Wanahongwa Mamilioni na Simba na Yanga na wanazichukua kwakuwa TFF inawapa Pesa Kiduchu ( Kidogo ) hivyo hakuna namna na Wao pia wana Familia zao.

Simba na Yanga ni wahongaji Wakuu!!!!
 
Kwa taarifa yako uwanja wa Manungu ni mzuri kuliko Jamhuri kwa maana ya pitch. So simba itacheza pira lake bila shida, tutamuona Chama vizuri tu.

Changamoto tu kule ni uwezo wa kubeba washabiki.
Pumbavu kaa Kimya huna ukijuacho Ok?
 
Ukizoea kuwa mwizi na ukafanikiwa unaona kila anayefanikiwa ni mwizi. Mpira ni mchezo wa wazi kabisa na sio wa kificho. Yanga anapambana kivyake tena kwa jasho na damu.
 
Yanga SC wakati wa Rais wa TFF akiwa Jamal Malinzi walibeba Ubingwa mara Nne ( 4 ) Mfululizo kwa UMAFIA huu niliouelezea hapa.

Simba SC yangu pamoja na kuwa Bingwa mara Nne ( 4 ) mfululizo na kufanya vizuri Kimataifa ila na yenyewe ilifanya UMAFIA huu.

CEO wa Azam FC Popat aliwahi Kunukuliwa kuwa alishaambiwa na Mwamuzi Mmoja kuwa wakiendelea kuwa Wabahili ( Walugume ) Ubingwa wa Ligi nchini watausikia katika Bomba tu kwani Wenzao wa Simba na Yanga wanawahonga ( wanatoa ) sana.

Binafsi GENTAMYCINE nina Mwamuzi Mmoja Rafiki yangu ananiambia huwa Wanahongwa Mamilioni na Simba na Yanga na wanazichukua kwakuwa TFF inawapa Pesa Kiduchu ( Kidogo ) hivyo hakuna namna na Wao pia wana Familia zao.

Simba na Yanga ni wahongaji Wakuu!!!!
Hapa kuna urongo mwingi.
 
umafya una nafasi yake ktk soka letu, bt umafya bila kikosi bora ni sawa na kazi bure, kwa sasa vyura umafya unawalipa coz wanakikosi bora hivo tuache kujidanganya kama umafya pekee unaweza kutusaidia bila kuwa na kikosi bora.

nakumbuka misimu yote tulofanya vizuri, yanga walitufanyia umafya sana mechi zetu za ndani na mechi za kimataifa kwa wapinzani wetu bt hawakufanikiwa coz tulikua na kikosi bora sana.

kilicho bora kwetu sasa ni kupambania kuimarisha kikosi chetu coz ukiwa na kikosi bora kufanya umafya ni kazi rahisi sana.
 
Kwa masikitiko makubwa Asubuhi ya leo nilianzisha Uzi hapa JamiiForums nikisema kuwa Kitengo cha Umafia Simba SC Kinepwaya na kwamba nipewe Mimi na Wenzangu Sita (6) na Yanga SC hatokuwa Bingwa kwa Mshangao huo Uzi siuoni (kwa Lugha sahihi ni kama vile Umefutwa) kwasababu wazijuazo Walioufuta.

Ni kwamba kwa sasa naona Mapungufu makubwa ya Kimkakati (Kimafia) ndani ya Klabu yangu ya Simba kiasi kwamba Yanga SC wameshaanza kuyatumia Kujinufaisha nayo na wanaelekea Kufanikiwa.

Kitengo cha Umafia ( Mikakati ) cha Simba SC kingekuwa imara kamwe Mchezo wetu na Mtibwa Sugar FC usingepelekwa Manungu ila kutokana na Kuzubaa Kwetu, Kujisahau na Kuridhika TFF (hasa Bodi ya Ligi) kwa Kushirikiana na Yanga SC na Matajiri wao GSM sasa wanatumaliza tu.

Viongozi wa Simba SC waliomba Mechi isichezwe Manungu wamekataliwa kwa Kigezo kuwa Uwanja ni mzuri ila Yanga SC wameomba Mechi yao isichezwe Uwanja wa Ushirika na ikachezwe Sheikh Amri Abeid Kaluta Arusha wamekubaliwa wakati hali ya Uwanja wa Manungu ni sawa na ya Uwanja wa Ushirika.

Walichokifanya Yanga SC ni kupitia kwa Mtu ( Shabiki ) wao mkubwa IGP Sirro ili Kumshawishi ahakikishe Mevhi haichezwi Ushirika na kwa Kuzuga ( Kutuzuga ) Jeshi la la Polisi wakaja na Taarifa ya Utetezi kuwa Mchezo huo umehamishwa Ushirika kwakuwa Uwanja utatumika kwa Shughuli za Kijeshi wakati si kweli ila ni Mpango Maalum wa kuitengenezea Yanga SC Mazingira ya Ushindi.

Viongozi wa Simba SC wasichokijua ni kwamba baada ya Kutunishiana Misuli kwa CEO Barbara Gonzalez na Mwenyekiti wa Simba SC ( Wanachama ) Murtaza Mangungu na TFF pamoja na Bodi ya Ligi ( TPLB ) wametengeneza Bifu Kubwa ambapo Yanga SC na GSM yao wameamua Kutumia mwanya huu ( huo ) kwa Kuwahonga baadhi ya Viongozi wa TFF na TPLB ili waikomoe Simba SC ili iangushe ( ipoteze ) Alama ( points ) na Yanga SC aweze Kutuacha kwa mbali sana na ikiwezekana atangaze Ubingwa mapema mno na kwa GENTAMYCINE ninavyoona na Kuyasikia naliona hili Kufanikiwa.

UMAFIA ninaoumaanisha hapa unahusu Mambo Makuu matatu ambayo ni...

1. Rushwa
2. Uchawi
3. Propaganda

Najua kwa Wageni wa Soka la Bongo hapa mtanishangaa GENTAMYCINE, ila kwa wale Watu wa Mpira naamini wamenielewa na wala hapa tusifichane Klabu za Simba na Yanga Mafanikio yao ya Uwanjani Kitakwimu ni kama ifuatavyo.....

1. Rushwa....45%
2. Uchawi...40%
3. Propaganda....10%
4. Uchezaji...5%

Simba SC mpaka tuje Kushtuka kuwa tunahujumiwa na TFF na TPLB huku Yanga SC na GSM yao wakiutumia mwanya huu ( huo ) Kujinufaisha Kiushindi tayari Yanga SC watakuwa Mabingwa wa NBC Premier League Msimu wa 2021 / 2022.

Simba SC tuendeleeni tu Kuzubaa sawa?
Acha kulalama, timu yako mbovu tu. Ulishindwaje pale kwa Mbeya City wakiwa pungufu zaidi ya 50 minutes. Utajua hujui.
 
Back
Top Bottom