SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 8,537
- 13,847
Kuna watu wanachukulia poa utaratibu na haki iliyopewa timu ngeni kufanya mazoezi katika uwanja utakaochezewa mechi siku moja kabla ya mechi.
Wachezaji wanapokuwa wamefanya mazoezi katika uwanja wa vita watakaoenda kuutumia, hili ni suala la kiufundi na linasaidia kuandaa wachezaji kimwili na kisaikolojia. Lengo kuu ni kuweka mizania sawa kati ya timu zote mbili kuelekea mchezo husika. Kumbuka football inaendeshwa na dhana nzima ya "fair play" na kanuni nyingi zimetengenezwa kulinda dhana hii.
Nakumbuka misimu miwili iliyopita Simba ilifanya kosa moja kubwa sana lililoigharimu timu na kufifisha harakati zake za ubingwa.
Simba ilihamishia mechi yake dhidi ya Prisons katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro na kupoteza mchezo ule kwa goli 1-2. Sikumbuki sababu hasa ilikuwa nini ila pamoja na kwamba ilikuwa ndiyo mwenyeji wa mchezo, Simba haikufanya mazoezi katika uwanja ule wa Jamhuri kabla ya mchezo husika. Nakumbuka kulaumu kuwa moja ya sababu ya Simba kupoteza mchezo ule hii inaweza kuwa ilichangia pakubwa sana.
SOMA HAPA:
Simba imeenda kuutumia uwanja wa Jamhuri bila kuujaribu
Utagundua issue siyo kuwa mwenyeji bali kuwa na familiarity na uwanja husika na kuutumia muda mfupi kabla ya mechi ni jambo muhimu kwa wachezaji wa timu zote mbili.
Kwa kulipanua zaidi hili suala na kuongeza uelewa, ndiyo maana mara nyingi utaona Simba huwa inaenda kufanya mazoezi Uwanja wa Mkapa walau siku moja kabla ya mechi za kimataifa na pia huwa inafanya hivyo pia katika uwanja wa KMC kabla ya mechi ya ligi. Hili ni suala la kiufundi zaidi na usipokuwa mtu wa mpira hauwezi kulielewa.
NYONGEZA: Hapa sijaongelea ukweli kuwa kuizuia timu iliyo na haki ya kutumia uwanja siku moja kabla ya mechi ni kuvuruga ratiba yake ya maandalizi ya mechi husika na inaua dhana nzima ya fair play. Ukiizuia timu kama ilivyotokea kwa Simba, itatakiwa kwenda katika mechi bila kuwa imefanya mazoezi kwa masaa 48. Hapo utimamu wa kimwili wa wachezaji utakuwaje?