Siku za malori Dar zahesabika

Pongezi kwa serikali naona ina nia njema ya kupunguza foleni Dar, lakini inashangaza kuona kuna watu wanapinga kila kitu. Hivi hili suala la folen Dar mnajua linaliingizia taifa hasara gani? Mnajua mtu mmoja mmoja anaathiriwa vipi?
 
Safi sana Magufuli wanyooshe Hawa wapinzani uchwara mpaka wakose hoja
Shida ni maendeleo au upinzani?hivi usa au uk pamoja na maendeleo yao kuna siku upinzani ilikosa hoja?
Iq ya vijana wakitanzania ipo shida
 
Tunapaswa kuwa makini sana na porojo pamoja na maigizo ya wanasiasa. Wakati wa kampeni mwaka jana Rais Kikwete "alizindua" ujenzi wa Reli ya Kati ya kisasa. Huo ujenzi umefikia wapi? Wanasiasa wa hii nchi hawafikirii zaidi uchaguzi ujao! Awamu ya kwanza ya barabara za mabasi yaendayo kasi (RBT) una urefu wa 21.1km tu lakini umegharimu $290m (zaidi ya Sh 600bil/-) ikiwa ni matumizi ya wastani wa karibu Sh 30bil/- kwa kila kilomita!! Huu ni ufisadi wa kutisha na ni dhahiri mradi wa RBT hauwezi kutupatia thamani ya pesa yetu. Hizo Sh 600bil/- zingetosha kabisa kujenga barabara zote za mduara zinazohitajika pamoja na kuweka lami barabara zote Dar hadi za vichochoroni; na hii ingeondoa kabisa foleni za magari barabarani. Kufikiria kujenga jumla ya 130km za RBT ni sawa na kubariki ufujaji wa zaidi ya Sh 3 trilioni za ziada!
 
Kwa hiyo chakula na mifugo italetwaje dar?
Utafiti unahitajika zaidi
Tanker nazo zitaishia wapi?
Mkuu hizo treni si zinaenda Na makontena ruvu then zikirudi Dar zinabeba hivyo vyakula vya kuku??
 
Tunapaswa kuwa makini sana na porojo pamoja na maigizo ya wanasiasa. Wakati wa kampeni mwaka jana Rais Kikwete "alizindua" ujenzi wa Reli ya Kati ya kisasa. Huo ujenzi umefikia wapi? Wanasiasa wa hii nchi hawafikirii zaidi uchaguzi ujao! Awamu ya kwanza ya barabara za mabasi yaendayo kasi (RBT) una urefu wa 21.1km tu lakini umegharimu $290m (zaidi ya Sh 600bil/-) ikiwa ni matumizi ya wastani wa karibu Sh 30bil/- kwa kila kilomita!! Huu ni ufisadi wa kutisha na ni dhahiri mradi wa RBT hauwezi kutupatia thamani ya pesa yetu. Hizo Sh 600bil/- zingetosha kabisa kujenga barabara zote za mduara zinazohitajika pamoja na kuweka lami barabara zote Dar hadi za vichochoroni; na hii ingeondoa kabisa foleni za magari barabarani. Kufikiria kujenga jumla ya 130km za RBT ni sawa na kubariki ufujaji wa zaidi ya Sh 3 trilioni za ziada!
Kwako wewe kila kitu Ni siasa! Huna taarifa mpya tangu Raisi Magufuli atoe ahadi hiyo??
Hivi kweli hujui kwamba tayari mikataba ya ujenzi huo imeshasainiwa??
 
Hukuzielewa ndio maana umekimbilia kupost,
Utaposti kitu ambacho ukielewi? Utakuwa unaakili? Kwanza unaandika nini wakati huelewi? Hata kama huelewi si unaandika sijakuelewa. Hapa labda uje na hoja kuwa umanielewa vibaya au tofauti na makusudio yangu basi mchezo uishe.
 
Hii habari imekaa kipropaganda na haishangazi imechapishwa kwenye gazeti la propaganda la serikali (Habari Leo). Kwanza ujiulize kwa nini usafirishaji kwa njia reli umekuwa hapewi kipaumbele na serikali katika miaka ya hivi karibuni? Na mazingira yaliyopelekea hii hali iwepo sasa yamebadilika? Nani kasema "uchawi" wa kuepukana na utegemezi wa malori katika usafirishaji mizigo ni kujenga reli ya "standard gauge (SG)"? Na kwa nini reli ya Tazara nayo haitumiki kikamilifu na hakuna mpango wa kuigeuza kuwa ya SG? Hoja yangu hapa ni kwamba njia za reli zilizopo zimetelekezwa makusudi na siyo kwamba haziwezi kuendelea kutumika "economically" kama zikikarabatiwa inavyotakiwa kuwa na mabehewa ya kutosha. Sana sana ukizingatia gharama kubwa ya hiyo reli ya SG hakika itakuwa "white elephant" kama uchambuzi wa kitaalamu ulivyothibisha kwa reli inayojengwa Kenya.
Tazara ni standard gauge....hilo ni la kuniuliza ila ile hatuwezi kutumia peke yetu kwani wazambia wana hisa vile vile, ila nahisi penye nia pana njia, mazungumzo tu ......
 
Utaposti kitu ambacho ukielewi? Utakuwa unaakili? Kwanza unaandika nini wakati huelewi? Hata kama huelewi si unaandika sijakuelewa. Hapa labda uje na hoja kuwa umanielewa vibaya au tofauti na makusudio yangu basi mchezo uishe.
Soma ulichokiandika
 
Ni initiative nzuri kuwa na reli, lakini pia serikali isibebe kila mzigo wa miundo mbinu. Ingepaswa ama kujaribu kuleta wawekezaji waje wajenge iwe private. Na pia mashirika tofauti tofauti ya reli yaendeshe ma train yao ktk hizo reli wachuane ktk utoaji huduma.

Yani reli iwe kama barabara so long as una trains zako zimekidhi ubora na umelipa kinachotakiwa basi waruhusiwe kuendesha trains zao ktk hizo reli. Yani kuwa na mashirika mengi ya reli ya private. Na mjenga reli anaweza kuwa private ambaye atawatoza hawa wenye train.
 
Tunapaswa kuwa makini sana na porojo pamoja na maigizo ya wanasiasa. Wakati wa kampeni mwaka jana Rais Kikwete "alizindua" ujenzi wa Reli ya Kati ya kisasa. Huo ujenzi umefikia wapi? Wanasiasa wa hii nchi hawafikirii zaidi uchaguzi ujao! Awamu ya kwanza ya barabara za mabasi yaendayo kasi (RBT) una urefu wa 21.1km tu lakini umegharimu $290m (zaidi ya Sh 600bil/-) ikiwa ni matumizi ya wastani wa karibu Sh 30bil/- kwa kila kilomita!! Huu ni ufisadi wa kutisha na ni dhahiri mradi wa RBT hauwezi kutupatia thamani ya pesa yetu. Hizo Sh 600bil/- zingetosha kabisa kujenga barabara zote za mduara zinazohitajika pamoja na kuweka lami barabara zote Dar hadi za vichochoroni; na hii ingeondoa kabisa foleni za magari barabarani. Kufikiria kujenga jumla ya 130km za RBT ni sawa na kubariki ufujaji wa zaidi ya Sh 3 trilioni za ziada!
Ni kweli kabisa,Ila kipi bora wajenge kwa gharama kubwa kabisa au wapige huo mpunga wakale na familia zao?
Ile ya Jk ya kufungua reli ilikua Kiki tu za uchaguzi mkuu!si unajua mzee wa maigizo
 
Back
Top Bottom