Siku ya Wanawake duniani:- Ni aibu mwanaume kuomba lift kwenye gari ya mwanamke, kumuomba mwanamke vocha, rent ya nyumba etc

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
76,275
160,443
Huna gari, huna nauli, msomeshe mwanaume mwenzako akusaidie. Sio umuombe Hela, mweleze, nafika sehemu Fulani ila nimekwama nauli, je unanisaidiaje ili nifike huko niendako?

Kama atajisikia kukupa pesa, sawa, kama atakuitia boda sawa, kama atakuombea lift kwa jamaa zàke waendao huko uendako ni sawa, kama atakutukana, sawa kabisa, usimkasirikie chukulia kama changamoto ya kunoa ubongo wako ili uweze kujikwamua kutoka kwenye shida mbalimbali.

Kamwe usimuombe mwanamke lift, labda akwambie, bro twende nikisogeze.

Kuna vijana hawana aibu kabisa wanaomba kwa Wanawake Hela ya mafuta. Utasikia Rehema, uko POA? Niko Tegeta nimeishiwa petroli nirushie 20k. Hii ni laana, acha mara Moja, ulinunua gari ya Nini kama huwezi kuihidumia?

Mwingine anaomba Hela ya pango, utasikia nimeishiwa rent, nisaidie ya mwezi Mmoja..
Fvck you idiot... Acha mara Moja.

Usimwombe mwanamke vocha, wala pesa, ni dhambi. Jikaze kiume. Hamna neno mwanaume aliumbiwa jikaze kikike...
Halipo
 
Mh! kaka mbona wewe ulijiitaga jina lakike hapa jukwaani almaarufu kama "GiLesi".
Mpaka pale wanaume wakakuumbua!, ndo wakaunga ID hiyo yakike na hii..!
Vipi unalisemeaje hilo ama ni ilikuwa katika harakati za moja na mbili au mambo yaliingiliana kaka..??
 
Back
Top Bottom