Siku ya Mwanamke: Bi. Mwamtoro bint Chuma wa Mtaa wa Kariakoo

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,901
31,972
Angalia hapo juu picha ya Bi. Mwamtoro bint Chuma mama yake Sheikh Haidar Mwinyimvua.

Picha hii inamwonyesha Bi. Mwamtoro bint Chuma akipiga kura Uchaguzi Mkuu wa 1970.

Bila ya shaka yoyote kura yake ilikwenda kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Haiwezi kuwa vinginevyo.

Bi. Mwamtoro alikuwa mmoja wa akina mama waliokuwa mstari wa mbele katika TANU.

Bibi huyu aliishi zaidi ya miaka 100 na alifariki tarehe 11 May 1981.

Nyumba yake ilikuwa Mtaa wa Kariakoo na New Street No. 69 nyuma ya ofisi ya TAA miaka ya 1930 na nyuma ya TANU katika miaka ya 1950.

Hii nyumba hivi sasa iko nyuma ya ofisi ndogo ya CCM, Lumumba Avenue.

Nyumba hii yenye historia kubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika bado ipo katika mikono ya familia ya Mzee Haidar Mwinyimvua.

Nyumba mbili hizi, Ofisi ya TANU na nyumba ya Bi. Mwamtoro ilikuwa zilikuwa katika miaka ile zkitenganishwa na ua wa makuti.

Siku ya mkutano wa ndani wa TANU Nyerere akija kuzungumza na wanachama wa TANU haya makuti yalikuwa yanaondolewa hivyo kuunganisha nyua hizi mbili kuwa ua mmoja.

Wanawake wakikaa nyuma na wanaume wakiwa mbele.

Huu ndiyo ulikuwa uwanja wao akina Bi. Titi Mohamed, Bi. Hawa bint Maftah, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Chiku bint Said Kisusa kwa kuwataja wachache.

Wakimaliza mkutano wanawake walikuwa wanaingia kwenye nyumba ya mtoto wa Bi.
Mwamtoro, Haidar Mwinyimvua.

Nyumba hii mlango wake ulikuwa Mtaa wa Udoe ukitumiwa makhsusi na wanawake kwa kuingia na kutoka kuepuka kupishana na wanaume.

Wakati wa uhai wake marehemu Rashid Mfaume Kawawa aliwaambia ndugu zake Sheikh Haidar Mwinyimvua kuwa nyumba yao hii imebeba kumbukumbu nyingi za harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na endapo watataka kuiuza basi wakifikirie chama kwanza kabla ya mnunuzi mwingine.
 
Ndugu Mohamed,
Mwaka 1970 Mwl Nyerere mpinzani wake alikuwa ni nani kwenye huo uchaguzi mkuu?
Na ndio maana katamka kwa yakini uchaguzi ule wa 1970 kura ya Bi. Mwamtoro bint Chuma (of course na wapiga kura wengine) ilienda kwa Mwl. na sio vinginevyo. There were no choices!
 
Dudus,
Mwaka wa 1962 Uchaguzi wa Rais ulikuwa kati ya Zuberi Mtemvu na Julius Nyerere.

Mtemvu hakupata kitu.

Kwa hawa waliounda TANU wakapigania uhuru mtu wao alikuwa Nyerere.

1710360709140.png

Kulia Zuberi Mtemvu, Julius Nyerere na John Rupia
Nyuma waliosimama na silaha za jadi ni Bantu Group kulia wa pili waliosimamani Al Msham miaka ya mwanzo ya TANU​
 
Angalia hapo juu picha ya Bi. Mwamtoro bint Chuma mama yake Sheikh Haidar Mwinyimvua.

Picha hii inamwonyesha Bi. Mwamtoro bint Chuma akipiga kura Uchaguzi Mkuu wa 1970.

Bila ya shaka yoyote kura yake ilikwenda kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Haiwezi kuwa vinginevyo.

Bi. Mwamtoro alikuwa mmoja wa akina mama waliokuwa mstari wa mbele katika TANU.

Bibi huyu aliishi zaidi ya miaka 100 na alifariki tarehe 11 May 1981.

Nyumba yake ilikuwa Mtaa wa Kariakoo na New Street No. 69 nyuma ya ofisi ya TAA miaka ya 1930 na nyuma ya TANU katika miaka ya 1950.

Hii nyumba hivi sasa iko nyuma ya ofisi ndogo ya CCM, Lumumba Avenue.

Nyumba hii yenye historia kubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika bado ipo katika mikono ya familia ya Mzee Haidar Mwinyimvua.

Nyumba mbili hizi, Ofisi ya TANU na nyumba ya Bi. Mwamtoro ilikuwa zilikuwa katika miaka ile zkitenganishwa na ua wa makuti.

Siku ya mkutano wa ndani wa TANU Nyerere akija kuzungumza na wanachama wa TANU haya makuti yalikuwa yanaondolewa hivyo kuunganisha nyua hizi mbili kuwa ua mmoja.

Wanawake wakikaa nyuma na wanaume wakiwa mbele.

Huu ndiyo ulikuwa uwanja wao akina Bi. Titi Mohamed, Bi. Hawa bint Maftah, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Chiku bint Said Kisusa kwa kuwataja wachache.

Wakimaliza mkutano wanawake walikuwa wanaingia kwenye nyumba ya mtoto wa Bi.
Mwamtoro, Haidar Mwinyimvua.

Nyumba hii mlango wake ulikuwa Mtaa wa Udoe ukitumiwa makhsusi na wanawake kwa kuingia na kutoka kuepuka kupishana na wanaume.

Wakati wa uhai wake marehemu Rashid Mfaume Kawawa aliwaambia ndugu zake Sheikh Haidar Mwinyimvua kuwa nyumba yao hii imebeba kumbukumbu nyingi za harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na endapo watataka kuiuza basi wakifikirie chama kwanza kabla ya mnunuzi mwingine.
Ukisikia msemo "kujitolea hali na mali" basi hawa ndio mfano mkubwa kwa jitihada zao katika kudai uhuru.
Ingefaa hizi sehemu muhimu katika historia zinge bandiikiwa vibao vidogo (plaque) kueleza kwa muhtasari tukio la kihistoria lililo tokea kwenye nyumba hiyo.

Hivi vibao vinatumika sana nchi nyingi kuelezea matukio ya kihistoria katoka jengo hata kama kwa sasa linamilikiwa na mtu mwingine.
 
Huku kwetu historia inafunikwa
 
Huku kwetu historia inafunikwa
Fidel...
Soko la Kariakoo ofisini kwa Market Master Abdul Sykes pale ndipo Mwalimu Nyerere alipojuana na wanachama maarufu wa mwanzo wa TANU mfano wa Mzee Mshume Kiyate.

Pale palitakiwa pawekwe kibao kueleza historia hii achilia nyumbani kwa Abdul Sykes ambako aliishi na Mama Maria baada ya safari ya UNO na kuacha kazi ya ualimu.
 
Asante ustaadhi Mohamed Said Kwa Historia nzuri sana, sasa tunaomba utupe historia ya mchango wa kanisa katoliki katika kupigania uhuru na maendeleo ya Tanzania Kwa ujumla mpaka miaka ya 1980
 
Matawi,
Ahsante sana kwa kunidhania kuwa ninaweza kuwa naijua hata historia ya Kanisa Katoliki.

Mimi nimeijua historia hii unayoisoma hapa kwa kuwa ni historia ya wazee wangu.

Ukitaka kusoma historia ya Kanisa Katoliki soma: ''Pugu Hadi Peramiho 1888 - 1988 Wabenediktini wa Peramiho.''

Historia hii imeandikwa na wao wenyewe.

Napenda nikufahamishe kuwa mimi si ustadhi.

Unanivika kilemba kisicho changu.

Kuna watu wanapenda kuniita "Dr."

Huwakataza.

1710387451102.jpeg
 
Angalia hapo juu picha ya Bi. Mwamtoro bint Chuma mama yake Sheikh Haidar Mwinyimvua.

Picha hii inamwonyesha Bi. Mwamtoro bint Chuma akipiga kura Uchaguzi Mkuu wa 1970.

Bila ya shaka yoyote kura yake ilikwenda kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Haiwezi kuwa vinginevyo.

Bi. Mwamtoro alikuwa mmoja wa akina mama waliokuwa mstari wa mbele katika TANU.

Bibi huyu aliishi zaidi ya miaka 100 na alifariki tarehe 11 May 1981.

Nyumba yake ilikuwa Mtaa wa Kariakoo na New Street No. 69 nyuma ya ofisi ya TAA miaka ya 1930 na nyuma ya TANU katika miaka ya 1950.

Hii nyumba hivi sasa iko nyuma ya ofisi ndogo ya CCM, Lumumba Avenue.

Nyumba hii yenye historia kubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika bado ipo katika mikono ya familia ya Mzee Haidar Mwinyimvua.

Nyumba mbili hizi, Ofisi ya TANU na nyumba ya Bi. Mwamtoro ilikuwa zilikuwa katika miaka ile zkitenganishwa na ua wa makuti.

Siku ya mkutano wa ndani wa TANU Nyerere akija kuzungumza na wanachama wa TANU haya makuti yalikuwa yanaondolewa hivyo kuunganisha nyua hizi mbili kuwa ua mmoja.

Wanawake wakikaa nyuma na wanaume wakiwa mbele.

Huu ndiyo ulikuwa uwanja wao akina Bi. Titi Mohamed, Bi. Hawa bint Maftah, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Chiku bint Said Kisusa kwa kuwataja wachache.

Wakimaliza mkutano wanawake walikuwa wanaingia kwenye nyumba ya mtoto wa Bi.
Mwamtoro, Haidar Mwinyimvua.

Nyumba hii mlango wake ulikuwa Mtaa wa Udoe ukitumiwa makhsusi na wanawake kwa kuingia na kutoka kuepuka kupishana na wanaume.

Wakati wa uhai wake marehemu Rashid Mfaume Kawawa aliwaambia ndugu zake Sheikh Haidar Mwinyimvua kuwa nyumba yao hii imebeba kumbukumbu nyingi za harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na endapo watataka kuiuza basi wakifikirie chama kwanza kabla ya mnunuzi mwingine.
Kumbukumbu nzuri, kama hutojali naomba kufahamu chimbuko la mbadilishano wa madaraka kati ya waislamu na wakatoliki from

nyerere-mwinyi-mkapa-kikwete-magufuli

Huu utaratibu ulianzishwaje anzishwaje ahsante
 
Kaza...
Bahati mbaya sijui.

Ila mbona ccm na serikali ikiwaenzi watu kama hawa na vizazi vyao hakika walikuwa wazalendo wa kweli wanatoa mali zao kwa ajili ya kupigania nchi ila viongozi wa sasa wanaiba mali za nchi na kuzifanya zao, embu jiulize kulikuwa na ulazima gani wa mkapa na magufuli kugawa nyumba za swrikali halafu kuwapangia watumishi wa uma nyumba na hoteli?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom