Kamanda bwana!Kuna siku, miaka mitatu iliyopita, nilikuwa kwenye moja ya Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya mkoa wa Dar es Salaam kwa shughuli zangu za kikazi. Kabla ya shauri langu kuitwa liliitwa shauri linalomhusu mwananchi mmoja huko mtaani akipambana na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhusu umiliki wa ardhi iliyo na nyumba inayotumiwa kama Ofisi ya CCM.
Ilikuwa ni siku ya kusikilizwa kwa shauri hilo. CCM walikuwa wanaendelea na ushahidi wao kupitia mashahidi wao. Kuna shahidi mmoja wa CCM alijitaja kama Katibu wa CCM sehemu yenye mgogoro. Akasema kuwa alikuwepo tangu kununuliwa kwa eneo hilo na mnunuzi akiwa ni CCM. Akasema ardhi hiyo ilinunuliwa na CCM mwaka 1975. Akatoa na hati ya manunuzi inayoonesha muuzaji, mnunuzi-CCM na mwaka wa mauziano ambao ni 1975.
Akatoa ushahidi huo 'ulioshiba' mbele ya Baraza la Ardhi huku akijiamini na kusisitiza sana uwepo wake tangu mwaka huo hadi sasa ndani ya CCM. Shahidi alirudia mara kwa mara kuwa Mlalamikaji-huyo mwananchi hana umiliki wowote kwakuwa aliwakuta CCM wakiwa wameshanunua ardhi hiyo mwaka 1975.
CCM ilianzishwa tarehe 5/2/1977 baada ya kuungana kwa TANU na ASP. Surprisingly, CCM iliweza kununua ardhi, kwa mujibu wa shahidi, mwaka 1975 hata kabla haijazaliwa. Siku hiyo nikajua kuwa CCM si chama cha siasa cha mchezo mchezo!