SoC02 Siku moja tajiri namba moja Tanzania atakuwa kijana mwanzilishi wa Startup

Stories of Change - 2022 Competition

Orako

New Member
Aug 30, 2022
2
6
Asilimia kubwa ya wasomaji wa andiko hili wanamjua Elon Musk na matajiri wengi wenye utajiri unaokadiriwa kufikia hadi mamia ya mabilioni ya dola za kimarekani. Kinyume na uhalisia wa hapa nyumbani ambapo mabilionea wengi utajiri wao upo kwenye akaunti za benki mbalimbali na majengo.

Mabilioni ya matajiri wa Marekani yapo katika mfumo wa thamani za hisa katika makampuni waliyoanzisha au kuwekeza. Hata ukuaji wake kwa wastani wa muongo mmoja na kuendelea huwa ni mkubwa.

Mfano mzuri; hisa moja ya Amazon mwezi wa disemba, 2002 ilikuwa na thamani ya $0.98 na mwaka huu 2022, baada ya miongo miwili hisa moja ya Amazon ni sawa na $130 baada ya kutawanya hisa (stock split) ili kuzifanya ziwe nafuu bila kuathiri thamani. Naweza kusema hivyohivyo pia kwa makampuni kama Facebook, Tesla, Microsoft, n.k

Kwenye chati za Bloomberg, Forbes na machapisho mengine ya maudhui ya utajiri na uwekezaji majina mengi kwenye kumi bora ni waanzilishi wa startups zilizokua kupitia wawekezaji wa hatua za awali na ukuaji (Angel Investors na Venture Capitalists) na baadae kuorodhesha hisa zake kwenye masoko ya hisa. Kwa hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla tumeona mafaniko katika hatua za mwanzo na ukuaji kwa makampuni yanayoanzishwa na vijana wa kitanzania yanayojikita kwenye sekta ya teknolojia. NALA money ni mfano mzuri wa hili.

Lakini ni lini nitafungua kurasa za Forbes na kuona majina ya vijana hawa wajasiriamali na wanaojituma katika orodha ya matajiri wakubwa hapa Tanzania na hata Afrika?

Ni lini nitasoma ripoti ya utajiri isiyo ongelea wamiliki wakongwe wa viwanda (Industrialists) pekee kama matajiri vinara nchini?

Kuna haja kubwa yakufanya mabadiliko ya kimkakati (strategic reforms) katika masoko ya hisa na mitaji hapa nchini. Mamlaka inayosimamia sekta hii lazima ije na miongozo na sera zitakazo chochea makampuni binafsi kujiorodhesha katika soko la hisa la Dar es salaam kwa utaratibu rafiki na wenye unafuu pia kuwe na miondombinu imara itakayowezesha wananchi kununua na kuuza hisa kwa urahisi na usalama.

Mfano wa sera rafiki zilizochochea ukuaji wa sekta na biashara mbalimbali duniani ni kama sera ya kutoa kodi ya mauzo (sales tax) kwenye vitabu vilivyokuwa vinauzwa mtandaoni wakati Amazon inaanza kule Marekani. Sera hii ilichochea ukuaji wa bishara ya ununuzi wa kimtandao (e-commerce) na kufanya Amazon ikue. Pia, sera ya kugawa ruzuku kwa makampuni yanayotengeneza magari ya umeme.

Tuliona Tesla ikifaidika na mpango huu wa serikali ya Marekani. Haswa wakati Tesla inapitia kipindi kigumu ikiwa katika hatihati ya kufirisika. Hoja ni kwamba serikali na mamlaka zake zina nguvu kubwa na uwezo wa kukuza masoko ya mitaji nchini kwa kuja na sera kabambe kwa ajili ya ukuaji wa masoko haya.

Kwa mfano; sera ya unafuu wa kodi au kuyapa makampuni ya teknolojia yatakayojiorodhesha kwenye soko la hisa la Dar es salaam aina yeyote ya motisha kutachochea ukuaji wa idadi ya makampuni katika soko la hisa.

Vijana wa kitanzania watendelea kujifua na kunoa maarifa yao ili wajiajiri kwa kuanzisha makampuni yao ya teknolojia na nyanja nyingine lakini ni wachache watapata mitaji mikubwa (Venture capital) kwaajili ya kujiendeleza na labda kuja kununuliwa kwa bei kubwa na kampuni za magharibi.

Mifano halisi ni KopaGas kwa hapa Tanzania na Paystack kule Nigeria.

Lakini kama vijana wajasiriamali wa kitanzania haswa kwenye sekta ya teknolojia wanataka kutengeneza utajiri wenye tija na wa kudumu vizazi na vizazi (generational wealth) kama ule wa J.P morgan, Henry Ford, Rothschilds na wengineo basi soko la hisa ndio jawabu.

Kama Martin Luther Jr alivyosema

”Nina Ndoto”

Mimi binafsi ndoto yangu ni kusoma orodha ya matajiri vinara Tanzania iliyosheheni majina ya vijana wajasiriamali walioajiri vijana wengine milioni wa Kitanzania.

Tukumbuke masoko ya hisa na mitaji yakiwa thabiti na shirikishi kwa wananchi wengi. Uchumi wa nchi pia utakua. Kwa kiwango fulani tutapunguza gharama ya mikopo ya serikali.

Leo hii, mikopo mikubwa ya nje tunailipa kwa dola za kimarekani, hii inamaanisha shilingi inavyopoteza thamani yake ukilinganisha na dola za kimarekani kati ya kipindi cha kupata mkopo na kuiva kwa mkopo gharama ya kulipa huongezeka maradufu kutokana na gharama kubwa za ubadilishaji fedha muda wa kulipa madeni ya nje.

Tukiwa na wigo mpana wa wawekezeji wa ndani wa madeni ya serikali, gharama inapungua kwasababu madeni haya yatalipwa kwa pesa za kitanzania. Japani ni mfano mzuri wa hili. Inaongoza duniani kwa kuwa na deni kubwa ukilinganisha na pato la taifa lakini deni hilo kwa asilimia kubwa ni la wawekezaji wazawa wa kijapani. Hivyo ni nafuu na salama.

Rai yangu kwa vijana wajasiriamali

Kwanza kabisa usikate tamaa. Najua ni ushauri uliozoeleka lakini nitaongeza mambo makuu mawili.

1. Adabu ya muda na watu ni nguzo kubwa sana kwenye mafanikio hasa katika medani ya biashara. Mahusiano mazuri na washika dau ni kitu cha msingi. Ili kujenga na kukuza mahusiano hayo hakuna namna zaidi ya kuwa na adabu na muda wako na watu wanaokuzunguka katika kusukuma gurudumu.

2. Ili kufanikiwa kibiashara haswa katika nyanja za kimataifa katika uchumi wa kidigitali ni muhimu kuwa mtu wa mikakati. Watu wengi waliofanikiwa katika viwango vya kimataifa ni watu wa mikakati. Anzisha utamaduni wa kufanya vitu kimkakati katika maisha binafsi, ya kazi na pia ya kijasiriamali. Na usisahau kumtanguliza Mungu katika kila hatua.
 
Very nice thread.... Umeongea ukweli mtupu mkuu, shida ni serikali kutoandaa mazingira rafiki kwa Hawa vijana, kwani ndoto vijana wanazo, shida mazingira sio rafiki ikiwemo na tatizo la Mtaji. Bila kuandaa mazingira thabiti hapa nchini tutaishia tu kusoma story za akina Mark Zuckerberg, Jack Ma, Warren Buffet, Steve jobs na wengineo Lakini kuzarisha wa Kwetu inakua changamoto.
 
Back
Top Bottom