Siku 100 Za Rais Magufuli Zinavyojadiliwa na Wadau

Baada ya siku mia moja za Rais magufuli kuwa madarakani wananchi tumejionea kwa macho yetu mawili jinsi chama cha mapinduzi kilivyoweza kutoa tunda bora ambalo kupitia kura yetu sisi wananchi tumefanikiwa kuleta kiongozi bora aliyetuletea heshima watanzania , jukumu letu sasa kama wanachama na wapenzi wa chama cha mapinduzi nikufanya kazi kwa bidii na maarifa huku tukimuunga mkono Mh. Rais na kama kuna kosa tunapaswa kumkosoa ili alekee kwenye ulekeo sahihi.... Kwa niaba ya wananchi wa huku niliko napenda kusema VIVA VIVA MAGUFULI VIVA CCM VIVA TANZANIA.
 
co
Siku 100 za mambo meengi ambayo mwisho wa siku nothing has changed..

Bado IPTL inalipwa bilioni 8 kila mwezi licha ya mahakama kuwahi kusema ifilisiwe

Bado Konyagi wanalipa kodi kuliko vodacom

bado kibuku wanalipa kodi kuliko kampuni zote zinazoiuzia TANESCO umeme

Bado miji mingi michafu

bado wagonjwa wanalala chini mahospitalini nchi nzima

bado wanafunzi wanakaa chini shule nyingi nchi nzima

bado katiba mpya rasimu ya Warioba hakuna mabadiliko

bado mawaziri hadi wakuu wa wilaya wanaendesha mashangingi

Seating allowance kwa wabunge bado ipo

Andrew Chenge ni mwenyekiti wa bunge

Mwakyemba na Muhongo ni mawaziri katika baraza la mawaziri
copy and paste ya ZZK wewe ndani ya siku 100 umefanya nini?
 
KAMA kuna kitu ambacho Rais Magufuli amefanikiwa katika siku zake 100 za kwanza ni kuongeza msukumo katika ukusanyaji wa mapato na kuzuia matumizi yasiyo ya lazima. Lakini, baada ya kukusanywa, mabilioni hayo yamefanya nini?
Raia Mwema limezungumza na Mkurugenzi wa Bajeti wa Wizara ya Fedha na Mipango, John Mihayo Cheyo, kuhusu namna gani fedha ambazo Magufuli alizikusanya katika siku zake 100 zilitumika.
Kwanza, si siri tena kwamba Magufuli ameweka rekodi mpya katika ukusanyaji wa mapato. Sasa anakusanya shilingi bilioni 1,200 kulinganisha na shilingi bilioni 900 zilizokuwa zikikusanywa wakati anaingia madarakani.
“Kwa sababu ya kuongeza ukusanyaji wetu wa mapato, serikali imefanikiwa kupunguza deni la wakandarasi kwa kuweza kulipa shilingi bilioni 379.85. Haya ni makampuni yanayofanya kazi zake na sisi hapa na kutowalipa maana yake tulikuwa tunahatarisha uwepo wake. Kwa kulipa hizi fedha, tumeokoa ajira na kuwawezesha kuendelea kufanya kazi zaidi.
“Serikali pia imeweza kulipa kiasi cha shilingi bilioni 110 kwa kampuni ya Sumitomo ya Japan kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa Kinyerezi II. Fedha hizo ni asilimia 15 ya gharama za jumla za mradi huo. Malipo hayo yalibidi yafanyike kwani wanaotukopesha walitaka tulipe hiyo halafu na wao ndiyo walipe shilingi bilioni 740. Kwa kufanya malipo hayo, mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha megawati 250 kwa mwezi utaanza,” alisema.
Mradi wa Kinyerezi II unatarajiwa kupunguza utegemezi wa Tanzania wa kutumia nishati ya maji kuzalisha umeme kutoka asilimia 60 ya sasa hadi asilimia 15. Kwa kuzalisha megawati hizo, mradi huo ambao utakuwa unamilikiwa na serikali kwa asilimia 100, utakuwa mkubwa zaidi ya mara mbili kuliko ule wa kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ambao umekuwa ukilalamikwa kuinyonya nchi.
Kwenye sherehe za Uhuru ambazo Magufuli aliamua kwamba zisiadhimishwe kwa gwaride na mbwembwe nyingine na badala yake zipelekwe zinakohitajika, gazeti hili limeambiwa kiasi cha shilingi bilioni nne ziliokolewa.
Kwa mujibu wa Cheyo, fedha hizo sasa zimetumika kwenye ujenzi wa barabara ya kutoka eneo la Morocco hadi Mwenge jijini Dar es Salaam ambao tayari umeanza. Fedha nyingine, kiasi cha shilingi bilioni mbili zilizopangwa kutumika kwenye semina elekezi, zimepelekwa kununua vifaa tiba.
Wakati wa kampeni, Magufuli aliahidi kwamba atatoa elimu bure kwa wanafunzi wa ngazi ya msingi na sekondari, ingawa kwenye bajeti ya serikali ya mwaka huu wa fedha, suala hilo halikuwamo.
Kwenye mahojiano na gazeti hili, Cheyo alisema tangu mwezi Desemba mwaka huu, serikali imekuwa ikitumia kiasi cha shilingi bilioni 18. 8 kwa ajili ya kugharamia elimu hiyo ya msingi na sekondari na kwamba wanafunzi 9,734, 497 wamenufaika na hatua hiyo ya serikali.
Akitoa ufafanuzi, Cheyo alisema wanafunzi wa shule za msingi walionufaika na mpango huo wa serikali ni 8,269,651 (milioni 8.3) huku upande wa sekondari ikiwa ni wanafunzi 1,464,846 (milioni 1.5).
Katika eneo la elimu ya juu, Cheyo alisema kuimarika kwa makusanyo ya serikali kumeifanya iweze kutoa mikopo kwa wanafunzi wengine 23,717 ambao wametumia kiasi cha shilingi bilioni 245.17.
 
mimi nikiwa mtanzania mwenye akili timamu na mwenye kujielewa. jpm ajafanya lolote na hataweza maana ni zao la mfumo ule ule wa rushwa na ufisadi
Wakati maisha yanasogea mbele wewe utabakia na akili hizo hizo negative. Unapima kazi ya mtu kwa kuangalia yanayokuzunguka wewe na ndugu zako. Kuna maisha yanayoendelea mbali kabisa na mlango wa nyumba yako.
 
Back
Top Bottom