Sijawahi kula nyama tamu kama konokono

Nilichokishuhudia wanachukua konokono wanawachemsha, wakishatokota kuna vijiti special kwa ajili ya kutolea konokono kwa nyumba zao, kwa sababu washatokota hivyo wanachomoka tu, then wanawapaka chumvi kisha wanawakaanga nataka nijaribu nitakukaribisha mkuu

sizonjemadawa
Hata hawa wa Tanzania.maana hizi mvua wako wengi.na kuna siku nilimuona konokono kataga njiani.ana mayai meeeengi.madogo Dogo meupe.
 
acd7586fe14d786342d433fe247a6e58.jpg
 
Habarini wakuu

Maisha ni safari,

katika mihangaiko ya maisha nchi tofauti nimekula wanyama na wadudu ambao kwa jamii za tanzania wengi hawali kama vile
Konokono
Chura wakubwa (ryumi)
Nyoka aina ya chatu
Chui
Kobe
Ngedere (tumbili)
Funza wakubwa (wanakaa kwenye miti) n.k
Hao ni baadhi tu, na nilikula sikulazimishwa ila sikuwa na jinsi, katika nyama zote niwe mkweli konokono nimetokea kumpenda sana, ni nyama tamu haina hata mfupa ukipata yule mwenye mayai duh hutoacha kula nawaambia,

ombi: kama hapa dsm kuna sehem wanauza konokono mnidirect tafadhali.. nataka ile iliyokaangwa

kama na ww ushawai kula vyakula ambavyo watanzania wengi wanaona uchafu vitaje, tufahamiane


Tembea ujionee Dunia inamengi vingine havisimuliki
Tanzania ni vile tu tumebarikiwa vyakula vingi sana ndio maana watu hawali kitu kama konokono na wanyama/wadudu wengine

Ila ukweli ni Kwamba konokono ni mtamu kuliko hata maini /firigisi/figo. Tena kwa mbali sana
 
Tanzania ni vile tu tumebarikiwa vyakula vingi sana ndio maana watu hawali kitu kama konokono na wanyama/wadudu wengine

Ila ukweli ni Kwamba konokono ni mtamu kuliko hata maini /firigisi/figo. Tena kwa mbali sana
Kabisa mkuu
 
Watu siku hizi wanakula " uvinza " yote mpaka inakauka, na ukijisahau watu wanakausha hadi mtandao pendwa, afu we unakuja kujitapa kwa kula kitu kama kono kono?? Fanya tafiti kwanza kabla ya kuja kujigamba hapa.
 
Kuna mdada mmoja wa Kiitaliano aliwahi niambia kuwa wao kule konokono ni chakula maarufu sana. Ila wanatushangaa Watz kwa kula kumbikumbi.
Btw, ngoja wakushangae na kukucheka. Siku wakisikia kuwa kula konokono kunatibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume au siku wakina mama wakisikia ni dawa ya kumdhibiti mume asitoke nje ya ndoa, na dozi yake ni lazima uwatafune mkubwa mmoja kwa siku saba utaona wanavyofuatilia na kuulizia wanapatikana wapi.
Umenikumbusha mayai mabichi ya Kware!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom