Sijaona kosa la Rais Magufuli kujenga kiwanja cha ndege Chato, hata Nyerere alijenga Musoma

Mleta uzi Hivi huo uwanja aliouacha mwalimu pale Musoma unaujua ulivyokuwa? Nilikuwa Musoma Alliance miaka hiyo pale palikuwa vumbi tu ya kutua "foka" kama ilivyokuwa Tabora na kwingine.
 
Kiwanja cha ndege cha Musoma kipo 45 km toka Butiama, kulikuwa na nini cha maana kujengwa huko Musoma. Ni kurahisisha tu kiongozi kwenda kusalimia nyumbani.

Hata Rais Magufuli yupo sahihi kujenga kiwanja Chato.
Huwezi ukajua kama ni kosa au sio kosa mpaka uwe na ufahamu wa kiasi fulani na imani ya kidini.Kukurahisishia kamtafute mtu aitwae Mobutu Sese Seko na sehemu inayoitwa Bandolite.Utagundua kwa nini watu wanakuwa na wasiswasi kwa uwekezaji mkubwa kiasi hicho katika eneo hilo.
 
Ile ndege ya Rais inatua kwenye kiwanja cha ubora gani? Na shauri tuanzie hapo kabla ya kulalama maana Rais anastahiki zake katika usafiri pia.

Na washawasha!
 
Mnajitahidi sana kufunika kombe. ..
Tofautisha Airstrip iliyopo Musoma ambayo hutumika kwa ndege ndogo ndogo na International Airport ya Chato. Mwalimu alistaafu bila kuwa na nyumba nzuri mpaka JKT walipomjengea nyumba ambayo ilipomalizika tu alifariki. Mwalimu Nyerere hakuacha Barabara ya lami Butiama wala traffic light, Mwalimu Nyerere hakuifanya Butiama kuwa wilaya aliacha Butiama ni kijiji.
Mtoa mada usijaribu kumlinganisha Mwalimu Nyerere na Kiongozi yeyote kwenye uadilifu.
 
Nani kakudanganya kuwa mawazo ya kifukara kuwa ndio uadilifu? Tuambie Nyerere ikulu alitumia gari ya aina na thamani gani?

Na washawasha!

Tofautisha Airstrip iliyopo Musoma ambayo hutumika kwa ndege ndogo ndogo na International Airport ya Chato. Mwalimu alistaafu bila kuwa na nyumba nzuri mpaka JKT walipomjengea nyumba ambayo ilipomalizika tu alifariki. Mwalimu Nyerere hakuacha Barabara ya lami Butiama wala traffic light, Mwalimu Nyerere hakuifanya Butiama kuwa wilaya aliacha Butiama ni kijiji.
Mtoa mada usijaribu kumlinganisha Mwalimu Nyerere na Kiongozi yeyote kwenye uadilifu.
 
Kiwanja cha ndege cha Musoma kipo 45 km toka Butiama, kulikuwa na nini cha maana kujengwa huko Musoma. Ni kurahisisha tu kiongozi kwenda kusalimia nyumbani.

Hata Rais Magufuli yupo sahihi kujenga kiwanja Chato.

Kuna kiwanja cha ndege na Airstrip, cha musoma ni Airstrip, lakini cha Chato ni kiwanja cha Ndege chenye hadhi ya kimataifa, ruway yake ni kubwa kuliko hata kiwanja cha Mwanza, yaani kiwanja cha Chato ni sawa na JNIA-Dar, au Kilimanjaro, kwa nini kijengwe chato na sio labda Geita Mkoani?
 
Ni mambo ya kiusalama! ni lazima Rais anakoishi kuweze kuwa na options mbalimbali za usafiri...... wanaopiga kelele hawana cha maana zaidi ni kulalamika tuuuuu...!!
 
Kuna kiwanja cha ndege na Airstrip, cha musoma ni Airstrip, lakini cha Chato ni kiwanja cha Ndege chenye hadhi ya kimataifa, ruway yake ni kubwa kuliko hata kiwanja cha Mwanza, yaani kiwanja cha Chato ni sawa na JNIA-Dar, au Kilimanjaro, kwa nini kijengwe chato na sio labda Geita Mkoani?
Una uhakika unachokisema au umechukua taariafa za udaku kutoka JF ukafikiri ni kweli??
 
Unafikiri kila mtu ni kiazi humu, we endelea kudanganyika tu, Unajua maana ya Runway?, nimekwambia runway ya chato iko kwenye level ya international ambayo ni more than 2.5Km na upana wa 45m, kiwanja cha Chato kiko kwenye Category hiyo sawa na JNIA na Kilimanjaro
 
Tofautisha Airstrip iliyopo Musoma ambayo hutumika kwa ndege ndogo ndogo na International Airport ya Chato. Mwalimu alistaafu bila kuwa na nyumba nzuri mpaka JKT walipomjengea nyumba ambayo ilipomalizika tu alifariki. Mwalimu Nyerere hakuacha Barabara ya lami Butiama wala traffic light, Mwalimu Nyerere hakuifanya Butiama kuwa wilaya aliacha Butiama ni kijiji.
Mtoa mada usijaribu kumlinganisha Mwalimu Nyerere na Kiongozi yeyote kwenye uadilifu.
Chato haiwezi kuwa International Airport wewe acha uongo kiwanja ili kiweze kuitwa International airport kuna vigezo vingi vya kuzingatiwa. Huo ni uwanja wa ndege tu wa kawaida ambao utaweza kutua ndege ya Rais na ndege zingine kama hiyo!
 
Unafikiri kila mtu ni kiazi humu, we endelea kudanganyika tu, Unajua maana ya Runway?, nimekwambia runway ya chato iko kwenye level ya international ambayo ni more than 2.5Km na upana wa 45km, kiwanja cha Chato kiko kwenye Category hiyo sawa na JNIA na Kilimanjaro
Nimekuambia acha uongo usifikiri humu wote tuna akili za kuambiwa tu lazima tunachanganya na zetu!
 
Kiwanja cha ndege cha Musoma kipo 45 km toka Butiama, kulikuwa na nini cha maana kujengwa huko Musoma. Ni kurahisisha tu kiongozi kwenda kusalimia nyumbani.

Hata Rais Magufuli yupo sahihi kujenga kiwanja Chato.
Inaelekea una kaujinga Fulani.
Kiwanja cha Musoma kipo pale hata kabla ya uhuru, na ni kakiwanja Fulani hakana hata lami.
Mimi nilishangaa kilivyo kibovu na huo ulikuwa mwaka 1982 nikitoka Dsm via Mwanza, Air Tanzania Fokker Friendship ya wakati huo.

Tusimlaumu Mwalimu kwa sababu ya uelewa wetu finyu.
 
bila ushabiki wala nini? bwana huyu kafeli sana, na mnao mtetea mnazidi feli kwa kuleta mifano ya ajabu ajabu.

on mkuu unavyo umbuka kwa kuleta mada ya kitoto
 
Chato haiwezi kuwa International Airport wewe acha uongo kiwanja ili kiweze kuitwa International airport kuna vigezo vingi vya kuzingatiwa. Huo ni uwanja wa ndege tu wa kawaida ambao utaweza kutua ndege ya Rais na ndege zingine kama hiyo!
Uwanja wa ndege unapimwa urefu wa uwanja na ndege ya aina gani inaweza kutua. Musoma ina kiwanja ambacho ndege ndogo tu zinaweza kutua lakini uwanja wa Chato utakuwa Na uwezo wa ndege kubwa hata aina ya Boeing ama Airbus kutua. Je serikali ikiamua kutumia uwanja huu kibiashara haiwezi kuwa International Airport ? Jaribu kuwa Kuchambua hoja kwa akili badala ya kuruka na kumuita mtu mwongo.
 
Ona ulivyo kiazi upana wa 45km???!!!!!
Hiyo ni 45m na nilisharekebisha kule, na wewe kwa ujinga wako nimekwambia 2.5km UREFU sasa upana utakuwaje 45Km?,
Mbona unapenda matusi?, nini maana ya mjinga, hivi kweli ukishaishiwa hoja ndio unakimbilia kwenye matusi?

Kwa taarifa yako hata Songwe ni International Airport
 
Mwalimu alistaafu bila kuwa na nyumba nzuri mpaka JKT walipomjengea nyumba ambayo ilipomalizika tu alifariki.
Nilisikitika sana niliposikia ile nyumba (Niliiona kwa macho mwaka jana) aliishi kwa siku 14 tu
 
Back
Top Bottom