Siioni 'vita' dhidi ya dawa za kulevya, nasikia kelele tu!

Nimekuwa nikijiuliza lakini nakosa jibu. Hivi kweli haya mapambano dhidi ya madawa haya ni mapambano ya kisiasa? Kama jibu ni hapana, kwa nini sasa mjadala huu umewekwa kwenye jukwaa la siasa? Na kama jibu ni ndiyo, sababu yake ni nini?
Umefuatilia mkutano wa jana? Kama ulifuatilia jibu unalo sasa.
 
Umefuatilia mkutano wa jana? Kama ulifuatilia jibu unalo sasa.
Mkutano wa jana mbona ulikuwa wa kiutendaji tu na siyo wa kisiasa. Waliohudhuria ni wakuu wa idara wakiongozwa na RAS na makamishina wa mapambano ya madawa ya kulevya. Kilichokuwa kinafanyika ni kampeni dhidi ya madawa haya. Kampeni haikuwa ya kisiasa hata kama kuna baadhi ya wanasiasa walihudhuria. Kwani wanasiasa kampeni zao huwa ni za kisiasa tu saa zote? Wakihamasisha wakulima watumie mbolea, watoto wapelekwe shule, watu wanawe mikono baada ya kutoka chooni na kabla ya kula, hapo wanafanya siasa? Jana walikuwa wanahamasisha vijana waogope kutumia madawa haya na wale wanao wauzia nao waogope sheria. Sikuona siasa pale. Just because Madabida was one of the facilitators?
 
Back
Top Bottom