macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 24,803
- 47,883
Nadhani Nyerere alikuwa na hofu kuwa chama kingine kikishika madaraka kinaweza kumgeuka na kumweka kwenye wakati mgumu na hata kumfungulia mashtaka au kuvuruga maisha ya status quo ya wakati ule. Ndiyo maana hata baada ya kuondoka kwenye madaraka alipigana sana kuhakikisha kuwa nchi bado inaendelea kuwa ya CCM. Nadhani pia ndiyo mwanzo wa hofu yake ya kubadili katiba. Kihalali kabisa, tulitakiwa kubadili katiba na hata kuivunja CCM na kuwapa watanzania wote uhuru wa kuanzisha na kujiunga na vyama vipya.Naamanisha viongozi wote wanaotutawala ni zao lake, wamesoma kipindi chake, ni kweli alileta mfumo wa elimu wa hovyo kabisa ambao hauna faida yoyote, waliomfuata ni majangili tupu wametengenezwa na hii katiba mbovu ambayo hata yeye alikiri kuwa ni ya hovyo haswa, alishindwa nini kuibadili na uwezo alikuwa nao?