Shule zote za sekondari ziwe na masomo ya VETA

Niliwahi ongea na baadhi ya wazee waliosoma zamani wakaniambia zamani walisoma shule za msingi zilizokuwa na masomo ya Ufundi zote(TRADE SCHOOLS).Wakitoka walikuwa wanaweza kujitegemea kwani walikuwa wanaweza fanya kazi kama za useremala nk

Ili mwanafunzi akitoka awe na uwezo wa kujitegemea nashauri katika mipango ya elimu shule zote za sekondari masomo yaliyoko VETA yawe sehemu ya masomo ya lazima mwanafuzi kusoma.Masomo yatakayoingizwa kwenye mitaala yawe yale yanayohusiana hasa na mazingira yetu yanayotuzunguka.Masomo yanayoweza kuwemo ni kama kilimo,ufugaji wa mifugo mbali mbali ikwemo ufugaji wa samaki,Upishi,utengenezaji bidhaa mbali mbali kutokana na vile tunavyozalisha nchini au malighafi zake nyingi ziwe zile za nchini.

Watoto wengi wamekuwa wakionekana kama hawapendi kilimo na ufundi sababu ni kuwa hawafundishwi mashuleni.Mtoto kazaliwa gorofani kakulia gorofani unategemea atapenda kilimo na ufugaji wakati saa zote anasoma vitabu tu vya tuition kutwa? Ndio maana lazima kama nchi iwasaidie masomo yawepo sekondary kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Nimependekeza sekondary sababu walau watoto wanakuwa wakubwa kidogo ndio umri wa kufundishwa kujitegemea
Wapinzani watapinga tena
 
Back
Top Bottom