Mkuu;
Kwa nini unasema hivyo?
Kama kutumiwa kwa mambo mengine ''mabaya'' wanaweza tu kutumiwa kwa sababu moja ya nidhamu ya jeshi ni kukubali kwanza amri halafu maswali baadaye.
Serikali imetumia JWTZ ili kusaidia kubana matumizi.
Hivyo vifaa wameletewa wafanyie mitihani.Bado kuna tatizo la upatikanaji wa walimu wa masomo ya sayansi.
Kesho watapewa tenda ya kukutafuta wewe mpinga maendeleoTumpongeze tu lakini hizi sio dalili nzuri sana... Leo jeshi linapewa kazi Kama hiyo huwezi jua kesho na keshokutwa watapewa hukumu gani
Ila mkuu tusilaumu kila kituTumpongeze tu lakini hizi sio dalili nzuri sana... Leo jeshi linapewa kazi Kama hiyo huwezi jua kesho na keshokutwa watapewa hukumu gani
Akhsante kwa ufafanuzi wako mkuu!Kampuni ilishinda zabuni ya kuuza vifaa kwa serikali. Huu sio msaada.
Kwann jeshi letu lipewe jukumu hiloWIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imepokea vifaa vya maabara ya masomo ya Fizikia, Kemia na Baolojia vyenye thamani ya Sh bilioni 16.9 kwa ajili ya shule za sekondari nchini.
Vifaa hivyo vimetolewa na Kampuni ya Lab Equip Ltd ambayo ni miongoni mwa wazabuni watano walioshinda kusambaza vifaa hivyo kwa kanda 11 ambazo ni Kanda ya Kaskazini Mashariki na Kanda ya Kaskazini Magharibi.
Nyingine ni Kanda za Magharibi, Kati, Kusini, Ziwa, Nyanda za Juu, Dar es Salaam, Mashariki, Ziwa Magharibi na Nyanda za Juu Kusini.
Akipokea msaada huo Dar es Salaam, Kaimu Kamishna wa Elimu wizarani hapo, Nicolas Buretta alisema vifaa hivyo vitasambazwa kwa shule za sekondari 1,696 nchini, kati ya hizo, shule 1,625 ni za kata na shule 71 ni shule kongwe za Serikali.
Alisema vitasambazwa katika shule zilizokamilisha ujenzi wa vyumba vya maabara na kwamba, hiyo ni changamoto kwa shule ambazo hazijakamilisha majengo yao ili zikamilishe.
Kaimu Kamishna huyo alisema vifaa hivyo vitasambazwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), na kwamba kazi hiyo ya usambazaji itakamilika mwishoni mwa mwezi huu.
“Vifaa hivi vitaleta matokeo chanya katika masomo ya sayansi. Ujifunzaji wa vitendo utainua ari kwa wanafunzi katika kujifunza. Italifanya taifa kuwa na wataalam wa kutosha kwa kuwa hatutakuwa na changamoto ya vifaa,” alisema.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni ya Lab Equip Ltd, Hassan Raza aliishukuru na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako na timu yake kwa kuwaamini.
Wakati huo huo serikali inatoa ajira kwa walimu 3,104 wenye fani ya sayansi huku akiendelea kusaka walimu wengine 46,382 wenye fani ya sayansi ili kukidhi mahitaji katika masomo ya sayansi nchini.
VIDEO:
Soma kwa umakini usikurupuke mkuuJana nilipokuwa naangalia hiyo taarifa niliikuta katikati sikujua kumbe ni msaada mimi nilifikiri ni serikali imenunua.
Kumbe sio kodi yetu ni msaada kutoka majuuJana nilipokuwa naangalia hiyo taarifa niliikuta katikati sikujua kumbe ni msaada mimi nilifikiri ni serikali imenunua.
Vifaa kwa shule zote vimeletwa na kwa maana hii mkimaliza kujenga mtapewa vifaa.Hongera kwa hilo, Sie imekula kwetu maabara hakuna, tuliagizwa kutoa elf 20 au bati mbili kila mtu....
Hakuna ujenzi utakaofanyika make walimu ndo wanatakiwa kutoa elf 20 za ujenzi....Vifaa kwa shule zote vimeletwa na kwa maana hii mkimaliza kujenga mtapewa vifaa.
Kanda ya kaskazini mbona imesahauliwa kwenye teuzi zenu za kikanda?''Vifaa hivyo vimetolewa na Kampuni ya Lab Equip Ltd ambayo ni miongoni mwa wazabuni watano walioshinda kusambaza vifaa hivyo kwa kanda 11 ambazo ni Kanda ya Kaskazini Mashariki na Kanda ya Kaskazini Magharibi''.
kwasababu!Kwa nini JWTZ?
Tatizo la maslahi nchini sio kwa walimu pekee bali kwa wafanyakazi wote wa serikalini na sekta binafsi.Ni muda muafaka sasa maslahi ya walimu kuthaminiwa.....Hata kama shule inakila kitu, kama mwalimu maisha yake ni ya kuungauunga ni kazi bure.
Hizo nafasi unazosema zote wako mbioni kuitwa baada ya majina kupelekwa hazina.Walimu wako wa kutosha wa sayansi,zile nafasi walizotoa mpaka sasa awajaitwa.