Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 62,317
- 109,373
Mkuu;
Kwa nini unasema hivyo?
Kama kutumiwa kwa mambo mengine ''mabaya'' wanaweza tu kutumiwa kwa sababu moja ya nidhamu ya jeshi ni kukubali kwanza amri halafu maswali baadaye.
Serikali imetumia JWTZ ili kusaidia kubana matumizi.
Sio mara moja au mbili nimekuwa nikishauri kuliko wanajeshi kukaa huko vikosini wakiwa wanacheza darts na pool table kwani sasa hivi hakuna vita, ni bora wangepewa jukumu la kujenga nyumba za bei rahisi katika miji yetu. Sasa hivi si ajabu kumkuta mwanajeshi ana kitambi na sifa kubwa ni kupiga raia pindi wakinyang'ang'anyana warembo.