KERO Shule ya Ufundi Moshi imepunguza walimu wa elimu maalum, hivyo wanafunzi wanakosa elimu bora

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ninaomba Serikali kupitia TAMISEMI na Waziri wa Elimu waingilie kati shule ya sekondari Moshi Ufundi iliyopo Moshi Manispaa mkoani Kilimanjaro yenye wanafunzi wenye mahitaji maalum viziwi mwaka huu walihamishwa walimu zaidi ya 10 na kati yao wapo walimu wa masomo ya elimu maalum na kupelekea wanafunzi kukosa walimu wenye utaalam wa kuwafundisha

Wapo na walimu ambao hawana utaalam na hii imewafanya waone shule ni ngumu kwa sababu hawelewi hawana mawasiliano

Serikali iangalie nanma ya kuwasaidia hao watoto wapate elimu sawa na wenzao kwa sababu wana haki kama wenzao na wametengwa kwenye madarasa kwa madai ya kufundishika kwa wepesi lakini ndio kama wamesahaulika

Pia liangaliwe suala la michango ya taaluma na ukuta tunayochangishwa wazazi hatupewi mrejesho wa kiasi kilichopatikana na matumizi yake wala hakuna mkeka wa waliotoa na wasiotoa ni usanii mkubwa kama uliofanyika kwenye kuhamisha walim wa watoto wenye mahitaji maalum bila kuleta mmbadala na afisa elimu maalum manispaa yupo anatazama tu
 
walihamishwa walimu zaidi ya 10 na kati yao wapo walimu wa masomo ya elimu maalum na kupelekea wanafunzi kukosa walimu wenye utaalam wa kuwafundisha
Wanapohamisha walimu 10 kwa wakati mmoja pasipokuwa na uhakika wa kupata wengine kunairudisha shule kuwa ya kawaida na si ya ufundi tena, mmlaka ziko wapi tusaidie watoto wetu hawa?
 
Kamuone Mkenda yuko huko Rombo kwa ajili ya Pasaka. Ana uwezo mkubwa kulibena hili. Ni simu tu aongeens Waziri mwenzake wa Tamisemi.
 
Back
Top Bottom