Shule ina mwalimu mmoja na wanafunzi 195, akisafiri inafungwa

Elimu bureee, niliahidi na nimetekeleza. Mengine usiniuliza, mimi sikuahidi. STOP.

Ukidadafua zaidi nakuweka ndani.
 
TATIZO SIO KWMBA WALIMU HAWATOSHI ILA KUNA UKILITIMBA MKUBWA AMBAO UMEAMBATANA NA RUSHWA KWA MAAFISA ELIMU KATIKA HALMSHAURI KWA KUTOTOA MGAWANYO SAWA WA WALIMU KATIKA SHULE ZOTE, YAANI KILA MWALIMU AKIJA HUPANGIWA MJINI UKIULIZA UNAAMBIWA NI MGONJWA KWA HIYO AKAE KARIBU NA HOSPITALI! SASA UNAJIULIZA KAMA NI MGONJWA ALIKUJA KUFANYA NINI? KWANI HUKO KWINGINE WATU HAWAUMWI? YAANI SIKU NIKIWA KIONGOZI MWENYE MAAMUZI AU MDARAKA YA KUTOA AMRI/MAAGIZO KWA WAKUU WA IDARA NITAANZA NA MAAFISA WATUMISHI NA IDARA ZA ELIMU (MSINGI NA SEKONDARI)! JAMANI HIZI IDARA KUNA MAMBO YA AJABU SANA AMBAYO YANASABABISHA WANAFUNZI KUFELI NA WATUMISHI KUTOFURAHIA KAZI ZAO! HAKIKA NITAWABANA MPAKA WATASEMA POOO NA KUBADILI TABIA ZAO ZA OVYOO OVYOOO!
 
Hii Habari ni ngeni sana!

Inawezekanaje?!

Hapa nlipo nimepigwa na butwaa.

Yaani kama siamini amini vile.

Kwa kweli inasikitisha sana.

Hii si kawaida
 
==uwanja wa chato kwani umebeba Sh ngapi, tunaomba hata picha tu tuuone isije ikawa kila mada hoja za watu na mawazo yetu tunahamishiwa Uwanja wa Chato kumbe hauna hata hadhi ya ku_divert comment za watu wenye point heshima==
 
Huko Nyasa kuna Mkuu wa Wilaya,kuna Mkurugenzi wa Wilaya,kuna Afisa Elimu wa Wilaya,kuna Afisa Elimu Wilaya Msingi sio issue ya kitaifa hiyo mpaka mnapeleka lawama Kwa Rais.

Afisa Elimu Wilaya wanatakiwa awapange walimu ndani ya Wilaya kutoka na Idadi ya shule alizo Nazo kupitia Ofisi ya Utumishi Wilaya.

Tuache Siasa na Propaganda za kitoto.mambo ya kawaida ya utendaji Wilaya ni haya nibsa hapo tu may be kuna maeneo mengi yenye shida kama hizi
 
Aisee hii Shule ipo Jirani na Liparamba napitaga sana nikipita tena nitashka nimhoji kidogo Mwl.Gaudence
 
Ngojeni wahamie Dom kwanza..
Tumewekeza ktk ndege na mambo ambayo hayana umuhimu tumeacha mambo ya msingi
 
Hivi Viwanda bila Wataalamu vitakuwaje au ndo tunatengeneza cheap labour? Nini maana ya kuwa na uongozi katika ngazi za chini kama wanashindwa kudeal na vitu kama hivi?

Mambo ya nchi hii yanaweza kukufanya uwe na hasira bila kupenda.

========

JANUARI 9, 2017 wanafunzi 195 wa Shule ya Msingi Matarawe katika Kijiji cha Marungu, Tarafa ya Mpepo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, walikuwa wakiendelea na likizo licha ya kwamba ndiyo siku shule nyingi zilifunguliwa.

Siyo kwamba walitega shule, la hasha! Bali mwalimu pekee aliyepo, Gaudence Msuha, alikuwa amesafiri kwenda mjini Songea kuhudhuria mafunzo ya siku nane ya kujengewa uwezo masomo ya Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) yaliyotolewa kwa walimu wote wa awali kutoka wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma kati ya Januari 10 hadi 18, 2017.

Hii haikuwa mara ya kwanza kufungwa kwa muda kwa shule hiyo yenye darasa la awali, la kwanza na la pili tangu ilipoanzishwa mwaka 2016.

Shule ina mwalimu mmoja na wanafunzi 195, akisafiri inafungwa | FikraPevu
Acha uchochezi walimu wametosha na waliopo wana kinga ya kutokufa na hawatazeeka kwa uwezo wa malaika mzima mitandao. Idadi ya wanafunzi ikiongezeka nao wanajigawanya ma kujiongeza kama bacteria.
 
Hivi Viwanda bila Wataalamu vitakuwaje au ndo tunatengeneza cheap labour? Nini maana ya kuwa na uongozi katika ngazi za chini kama wanashindwa kudeal na vitu kama hivi?

Mambo ya nchi hii yanaweza kukufanya uwe na hasira bila kupenda.

========

JANUARI 9, 2017 wanafunzi 195 wa Shule ya Msingi Matarawe katika Kijiji cha Marungu, Tarafa ya Mpepo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, walikuwa wakiendelea na likizo licha ya kwamba ndiyo siku shule nyingi zilifunguliwa.

Siyo kwamba walitega shule, la hasha! Bali mwalimu pekee aliyepo, Gaudence Msuha, alikuwa amesafiri kwenda mjini Songea kuhudhuria mafunzo ya siku nane ya kujengewa uwezo masomo ya Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) yaliyotolewa kwa walimu wote wa awali kutoka wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma kati ya Januari 10 hadi 18, 2017.

Hii haikuwa mara ya kwanza kufungwa kwa muda kwa shule hiyo yenye darasa la awali, la kwanza na la pili tangu ilipoanzishwa mwaka 2016.

Shule ina mwalimu mmoja na wanafunzi 195, akisafiri inafungwa | FikraPevu

Asipo hudhuria kwenye mafunzo(kkk) hayo pia anakula adhabu...

mm nadhani wa husika muache upuuzi....
 
Back
Top Bottom