milele amina
JF-Expert Member
- Aug 16, 2024
- 4,500
- 6,204
Kuna kundi la nyumbu linasema mitano TenaWakuu,
Leo nimetoka Mwanza kwenda Nairobi kwa ndege ya Air Tanzania. Ndege hizi zinakera sana.
Kwanza kutoka Mwanza ilichelewa kwa nusu saa. Tukavumilia
Kasheshe imetokea tena usiku huu hapa uwanja wa Mwalimu Nyerere. Fikiria ndege ilipaswa kuondoka saa 2 usiku, wakasema itakawia mpaka saa 4 usiku. Robo saa kabla ya kuondoka wanasema itaondoka saa 8 usiku. Kama nchi tupo serious na biashara hii kweli?
Sisi wengine tunaconnection ya ndege na tayari tumeshachelewa. Tutafikaje tunakoenda, hasara hii nani atafidia?
Inakuwaje taarifa ya sitisho la safari inatolewa robo saa kabla ya ndege kuondoka? Maswali ni mengi kuliko majibu.
Serikali ijitafakari, mtasingia kuhujumiwa bure kumbe mnaua biashara wenyewe.
Nimechoka sana kama jina langu lilivyo.
Pia soma: KERO - ATCL imulikwe huenda kuna hujuma, ratiba za safari zao hazieleweki