Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,884
- 31,943
Hapa ndipo penye mtihani wa BAKWATA.
BAKWATA wanataka kuwa kiongozi wa Waislam.
Kuwa kiongozi wa Waislam kunataka imani ya hali ya juu na kujitolea kwa lolote.
.
Kuwa kiongozi wa Waislam kunataka kumtegemea Allah na kutomuogopa yeyote ila Allah Pekee.
Ponda kasimama dhidi ya dhulma za Baraza la Mitihani (NECTA) dhidi ya wanafunzi Waislam na kutangaza maandamano kama haya ya kuwaunga mkono Wapalestina.
Polisi wakatoa onyo kali kwa watakaotoka kuandamana.
Sheikh Ponda katika sala ya Ijumaa Msikiti wa Kichangani akawaambia Waislam, 'Kama hatukuandamana kwa dhulma hii ya NECTA tufanywe lipi ili tuandamane?''
Sheikh Ponda aliwauliza Waislam akiwa kasimama mbele kwenye kibla cha msikiti wa Kichangani.
Hotuba yake kwa Waislam jinsi vijana wa Kiislam wanavyodhulumiwa na NECTA ulijaza msikiti nzima simanzi.
Akawaambia Waislam.
''Tumekusanya ushahidi wote tunao.''
Ndani ya msikiti wamejaa makachero.
Nje ya msikiti kuna Defender na askari wamevalia mavazi ya mapambano.
Juu inapita helicopter.
Matangazo yametolewa Waislam wasithubutu kuandamana.
"Kama hatukuandamana kwa hili tutaandamana kwa lipi?
Mimi nitatangulia mbele kuongoza maandamano haya."
Hapo akaipa mgongo hadhira yake akaelekea kibla akanyanyua mikono yake kumkabili Allah kuomba nusra ya umma ule uliokuwa tayari kulikabili Jeshi la Polisi lenye silaha.
Allah aliwanusuru waandamanaji wote.
Maandamano yanafika Jangwani habari zinatangazwa Waislam wanaombwa waandamane kwa amani waelekee Kidongo Chekundu wasiingie mjini hapo viongozi watapokelewa na Polisi na kupelekwa Makao Makuu ya Wizara ya Ndani na ndipo Waraka wa Shura utapokelewa.
Wataalamu haraka waliishauri serikali vizuri polisi wasipambane kwa kuwa yote aliyosema Sheikh Ponda msikiti ni kweli tupu.
Polisi haiwezi kuwashambulia Waislam kwani itakuwa fedheha kubwa ukweli utakapojulikana.
Vijana wote wanafunzi wa Kiislam waliodhulumiwa na NECTA walipata haki zao.
Sheikh Ponda alikuwa mstari wa mbele akiongoza maandamano yale.
Serikali ikijua yote yaliyofanyika NECTA dhidi ya wanafunzi wa Kiislam.
Hii ilikuwa mwaka wa 2012.
Leo Sheikh Ponda kasimama tena dhidi ya dhulma ya Ghaza na mauaji ya Wapalestina.
Kakamatwa.
Umma unasubiri.
Turejee nyuma miaka 10 iliyopita BAKWATA wanaotaka uongozi walisimama wapi sakata la NECTA?
Leo BAKWATA wamesimama upande gani katika mauaji ya Wapalestina Ghaza?
Sheikh Ponda akizungumza na Vyombo Vya Habari
(Picha ya zamani)