Sheikh Ponda Ahoji Uhalali wa Serikali: Vitendo vya Mauaji na Utekaji vinavyokithiri nchini. Watu wanauawa, Wanatekwa. Maisha ya Kinyama

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
7,893
16,963
Siongezi wala sipunguzi. Sikilizeni kabla mods hawa delete huu uzi.

Sheikh Ponda Issa Ponda ameibuka na kuonyesha kukerwa na vitendo vya mauaji na utekaji vinavyoendelea nchini. Katika maelezo yake, Sheikh Ponda amehoji uhalali wa serikali, akisema kuwa vitendo hivi vinaathiri usalama wa raia na kuleta wasiwasi mkubwa katika jamii. Ameitaka serikali kutoa majibu kuhusu
 
Hili ni jembe na Mtu anayejitambua, amekuwa mtetezi wa Haki za Watanzania muda mrefu na wala yeye hajali nani yuko Ikulu , pale mambo yanapoharibika haachi kukemea na kupaaza Sauti. Bravo Mtu wa Mungu Shekh Ponda. Chapa Kazi kwa Maslahi ya watu wa Mungu. Mungu anachukia wanafiki wale wanaoamua kukaa Kimya huku mambo yakiwa yanaharibika. Una umma wa watanzania nyuma yako na wewe ni mtetezi wao wote bila ya kujali itikadi za kisiasa na kidini, wewe ni mtetezi wa wote. Mungu akujalie Afya na masiah marefu. Umekuwa muhanga pia ila usiogope. Unapigignia wanyonge na maslahi ya Taifa zima..
 
Huyu Sheiky ni Mpambanaji ambaye haogopi kuiambia serikali ukweli!
Tangu enzi za Utawala wa BWM alipita katika misukosuko mingi lakini mpaka leo msimamo wake ni thabiti.
 
Kuna wapumbavu watasema sio msimamo wa Waislamu...
Sio wapumbavu tu ndio mafundisho ya uislamu, kiongozi hasemwi hadharani bali kama ana mambo ya kumfikishia aseme kwa staha au amfuate private, sio kupayuka mtandaoni au kwenye mimbar za misikiti kutukana viongozi, huo sio msimamo wa uislamu wala waislamu wenye maarifa.
 
Sio wapumbavu tu ndio mafundisho ya uislamu, kiongozi hasemwi hadharani bali kama ana mambo ya kumfikishia aseme kwa staha au amfuate private, sio kupayuka mtandaoni au kwenye mimbar za misikiti kutukana viongozi, huo sio msimamo wa uislamu wala waislamu wenye maarifa.
Tupe Aya za Quran ๐Ÿ˜€
 
Tupe Aya za Quran ๐Ÿ˜€
- ุฑูˆู‰ ู…ุณู„ู… ุนู† ูˆุงุฆู„ ุงู„ุญุถุฑู…ูŠุŒ ู‚ุงู„: ุณุฃู„ ุณู„ู…ุฉู ุจู† ูŠุฒูŠุฏ ุงู„ุฌุนููŠ ุฑุณูˆู„ูŽ ุงู„ู„ู‡ - ุตู„ู‰ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆุณู„ู… - ูู‚ุงู„: ูŠุง ู†ุจูŠ ุงู„ู„ู‡ุŒ ุฃุฑุฃูŠุชูŽ ุฅู† ู‚ุงู…ุช ุนู„ูŠู†ุง ุฃู…ุฑุงุก ูŠุณุฃู„ูˆู†ุง ุญู‚ู‘ูŽู‡ู… ูˆูŠู…ู†ุนูˆู†ุง ุญู‚ู‘ูŽู†ุงุŒ ูู…ุง ุชุฃู…ุฑู†ุงุŸ ูุฃุนุฑุถ ุนู†ู‡ุŒ ุซู… ุณุฃู„ู‡ ูุฃุนุฑุถ ุนู†ู‡ุŒ ุซู… ุณุฃู„ู‡ ููŠ ุงู„ุซุงู†ูŠุฉ ุฃูˆ ููŠ ุงู„ุซุงู„ุซุฉุŒ ูุฌุฐุจู‡ ุงู„ุฃุดุนุซ ุจู† ู‚ูŠุณุŒ ูˆู‚ุงู„ - ุตู„ู‰ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆุณู„ู… -: ((ุงุณู…ุนูˆุง ูˆุฃุทูŠุนูˆุงุ› ูุฅู†ู…ุง ุนู„ูŠู‡ู… ู…ุง ุญู…ู‘ูู„ูˆุงุŒ ูˆุนู„ูŠูƒู… ู…ุง ุญู…ู‘ูู„ุชู…))[

Hii ni hadithi sahihi iliyopokelewa kutoka kwa mtume muhammad swala na salaam ziwe juu yake, mwanzo inasema aliuliza salamah mtoto wa yaziyd allah amridhie kumuuliza mtume swala na amani ziwe juu yake akasema:-

"ewe mtume wa allah, unaonaje ikiwa watatusimamia sisi watawala ambao wanatuomba haki zao na wanatunyima sisi za kwetu? unatuamrisha nini?."
Mtume swala na amani ziwe juu yake akampuuza {hakumjibu} kisha akamuuliza tena akampuuza halafu katika mara ya pili au ya tatu akamjibu akamwambia: "sikilizeni na mfanye utiifu, kwasababu hakika mambo yalivyo ni juu yao yale waliyobebeshwa{katika usimamizi} na ninyi ni juu yenu yale mliyobebeshwa."


Na mafundisho haya katika uislamu ni mengi sana, bali aya za Qur'an kwenye kufundisha watu wawe na subra na wasiwe wenye kufanya mambo pasi na kutafakari mwisho wake ni nyingi sana, ila hawa watu aina ya shekhe ponda na wanaharakati wengine hawataki kusoma wanaona wanacheleweshwa, tangu lini shekhe akaingia kwenye mikutano ya siasa? mambo haya yanaingiliana tangu lini?.

Uislamu umejengeka juu ya msingi wa elimu na maarifa, sisi tunasoma mangi tena tunasoma hasa dini yetu imehifadhiwa kwa elimu, ukiinua mdomo leo ukaongelea uislamu pasi na elimu kesho asubuhi kuna wanaume kadhaa wameshakurekebisha na kukutaka ueleze umetoa wapi ulichokisema, hivyo kwenye uislamu sahihi ni kusema kwa elimu au kunyamaza kwa upole, naam.
 
Back
Top Bottom