Inevitable
Senior Member
- Apr 27, 2012
- 111
- 276
Sheikh Ibrahim Bombo kutoka Mkoani Mbeya amependekeza Serikali ianzishe utaratibu wa kulipa mishahara kwa Viongozi mbalimbali wa Dini kutokana na kazi nzuri wanayoifanya ya kulinda amani na kuhamasisha maendeleo Nchini Tanzania ambapo amependekeza kiwango chao cha chini cha mshahara kisipungue Tsh. laki tisa (900,000/=).
Sheikh Bombo ametoa maoni yake kwenye kongamano la kikanda, Kanda ya Kusini la kukusanya maoni ya Wannanchi kuhusu Dira mpya ya maendeleo ya mwaka 2050.
“Viongozi wa Dini wanafanya kazi nzuri sana kwenye hili Taifa hasa kuliombea amani na jambo lingine, ningependa kuona Viongozi wa Dini waingizwe kwenye pay roll ya Serikali kila mwezi wapate maokoto, ni muhimu sana na kiwango cha chini iwe 974,310, hiyo ianze kulipwa kuanzia mwaka 2025 kwenda 2050”