LGE2024 Shauku na hamasa ya wanafunzi ngazi mbalimbali kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwa kero na maumivu kwa upinzani kulikoni hasa?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
19,857
21,856
Hamasa na shauku ya wasomi hawa vijana wa shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu wenye sifa na vigezo vya kujiandikisha na hatimae kushiriki zoezi la maamuzi kupitia sanduku la kura, unadhni kwanini linawaudhi sana watu wa upinzani?

Wengi wao watafikisha umri wa miaka 18 kesho jumamosi tar 19.10.2024, kwanini asiandikishwe huyo?

Lakini pia wengine kwa maelfu yao watafikisha umri kama huo wa miaka 18, mapema mwaka ujao Sept.2025. Hao nadhani hao nao wana haki stahiki ya kuandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili mwaka ujao waweze kushiriki uchaguzi mkuu kwa mujibu wa sheria, right? Kuna makosa gani hapo my friends, ladies and gentlemen?

Soma Pia: UVCCM yataka upinzani kuacha kulalamikia uandikishaji wa wanafunzi

So,
Sio sawa kuwanyima fursa na haki yao ya msingi vijana hao wazalendo na wanaojielewa katika zoezi hilo muhimu la kihistoria. Wala hakuna haja ya kuwakasirikia kana kwamba woa ni CCM 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Hamasa na shauku ya wasomi hawa vijana wa shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu wenye sifa na vigezo vya kujiandikisha na hatimae kushiriki zoezi la maamuzi kupitia sanduku la kura, unadhni kwanini linawaudhi sana watu wa upinzani...
Nafikiri zoezi la kuandikisha wapiga kura kwenye daftari la kudumu lingekuwa endelevu sio leo liko wazi kesho limefungwa
 
Back
Top Bottom