Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,196
- 5,573
Hatimaye kijana Shadrack Yusuph Chaula (24) mkazi wa kijiji cha Ntokela kata ya Ndanto Tukuyu wilayani Rungwe, ameachiwa huru kutoka mikononi mwa jeshi la magereza baada ya kufanikiwa kulipa faini ya shilingi million tano kutokana na hatia aliyokutwa nayo ya udanganyifu juma lililopita.
Kijana Shadrack Chaula amelipa fedha hizo baada ya kuchangwa na wanaharakati na wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Chaula alihukumiwa na mahakama ya wilaya ya Rungwe kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya shilingi million tano baada ya kukiri kosa la kudanganya.
Baada ya hukumu hiyo juma lililopita, kijana huyo alienda gerezani kuanza kutumikia kifungo cha miaka miwili jela ndipo baadaye wanaharakati akiwemo Godlisten Malisa wakaanzisha mchango ili kupata fedha za kumtoa gerezani na kufanikiwa kupata zaidi ya shilingi million sita.
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Mbeya: RC Homera aagiza kukamatwa kwa kijana aliyemkashifu Rais Samia na kuichoma picha yake
- Aliyekamatwa kwa kuchoma picha ya Rais Samia ahukumiwa faini Tsh. Milioni 5 au miaka miwili jela
- Baada ya alichechoma picha ya Rais Samia kuhukumiwa Miaka miwili Jela, Wakili asema wanafikiria kukata rufaa
- Mvutano wa kisheria, tuhuma ya msanii aliyechoma picha ya Rais
- Baada ya alichechoma picha ya Rais Samia kuhukumiwa Miaka miwili Jela, Wakili asema wanafikiria kukata rufaa