Serikali zetu za kulakula bila kujali wananchi kuliko vifaa vya zimamoto na uokoaji

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
7,375
10,169
Serikali hizi zetu za kulakula bila kujali wananchi.

Ukijiuliza ni kwanini wanasiasa tu machawa ndiyo wana nunuliwa magari ya milioni 300 na mia nne kwa kazi za kufuta wagombea wa vijiji wakati zimamoto hawana vifaa vya kuokoa watu na mali zao.

Hakuna hata mtu mmoja anafukuzwa kazi. Kila kitu serikali inasingizia Polisi. Kuokoa watu polisi, watu kutekwa polisi, majengo mabovu waokoaji polisi, kuhoji wamiliki ni Polisi.

Yaani hakuna uwajibikaji wa aina yeyote. Kibaya zaidi kwasababu hakuna ulalamikaji wa watu serikali haitafanya lolote.

Hizo ripoti za mauaji na utekaji mpaka leo hazijatoka na watu wana cheka cheka. Hivyo tujilaumu wenyewe
 
Kuna fedha za kuhudhuria Kila mkutano nje ya nchi huku ATCL imepaki nje lakini hakuna ya kununua hata crane moja kufikia ghorofa hata kumi tuu. Ingekuwepo ingeanza kuondoa vifusi toka juu.
 
Back
Top Bottom