Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,492
- 7,033
Serikali ya Tanzania imewaonya watu waliojipanga kuleta fujo, kujihusisha na rushwa ama kuleta sitofahamu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kuwa ipo macho na haitatoa mwanya wa kufanyika hila hizo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene ameyasema hayo leo Jumatano Aprili 9, 2025 wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Mwera (CCM), Zahoro Mohamed Ally.
Mbunge huyo amehoji Serikali imejipangaje kupambana na rushwa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2025 ukizingatia kuna upungufu wa watumishi na vitendea kazi.
Akijibu swali hilo, Simbachawene amesema Serikali imejipanga na kudhamiria kuwa na uchaguzi wa huru na wa haki ambao viongozi watachagua kwa uwezo wao wa kuongoza na kuwahudumia wananchi, na sio kwa kuwarubuni wapiga kura kwa rushwa.