Serikali yavuna Bilioni 340 toka Barrick

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,533
3,186
SERIKALI imesema imeshapokea Dola za Marekani milioni 140 (zaidi ya Sh. bilioni 340) kutoka kwa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Barrick ikiwa ni makubaliano waliyoingia na serikali.

Katika makubaliano ya mapitio ya mkataba wa kampuni hivo na serikali, Barrick watatoa Dola bilioni 300 na fedha ambazo imepata ni sehemu ya fedha hizo.

Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa kampuni hiyo, serikali ya mkoa na Wizara ya Madini, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Steven Kiruswa, aliwashukuru Barrick kwa kuendelea kutekeleza makubaliano ya mkataba huo.
Alisema serikali itaendelea kushirikiana na wawekezaji ambao wanafuata na kusimamia makubaliano waliyoingia.

"Serikali tunaendelea kunufaika na makubaliano maya na kampuni hii ya Barrick, hii yote ni kuhakikisha rasilimali za nchi zinanufaisha taifa letu," alisema Kiruswa.

Aidha, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa ndani kutoka ofisi ya hazina, Lightenes Mauki, alisema pia kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 31, mwaka huu, serikali pia imepokea gawio la Dola za Marekani milioni 36 kati ya Dola milioni 52 wanazotakiwa kupata kutokana na ushirikiano wa kampuni hiyo na kampuni ya Serikali ya Twiga Mineral Coop-eration.

"Tunafahamu pesa zilizobaki za gawio ziko kwenye mchakato wa kulipwa" alisema Mauki

Oktoba mwaka 2017, serikali na Barrick ziliafikiana kuwa kampuni hivo kuilipa Serikali ya Tanzania hisa ya asilimia 16 na mgawo wa asilimia 50 ya mapato ya mauzo ya dhahabu kutoka mi godi inayoimiliki.

Barrick pia walikubali kutoa Dola za Kimarekani milioni 300 kama malipo ya kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato ku-tokana na biashara ya kampuni hiyo.
 
Japo bado wanatupiga lakini angalau wanaleta kidogo.bibi aige hawa barrick kuhusu bandari na siyo anavyotaka kuiuza pasipokuwa na uwazi mkataba utaisha lini,tutapata nini na vikorokocho vingine vingi tu havijawekwa wazi
 
Afadhali Magufuli kaacha alama na pesa tumeanza kuvuna, hivo shoo lazima uwe katili tofauti na hapo utapigwa kama wanavyopigwa kenya na kampuni ya DP world
 
Back
Top Bottom