Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,782
- 13,541
Wamesema mazingira kama hayo yanachangia kuwarudisha nyuma Wakulima na kutotimiza malengo yao, hivyo wanaomba Serikali Kuu iingilie na kuwasaidia kwani wanapitia kipindi kigumu kwa kutopata malipo yao.
Akizungumza na JamiiForums, Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Kilimo, Gungu Mibavu amesema “Tunaendelea kuwalipa wiki hii, ucheleweshaji ulitokana na kulipa madeni ya awali. Tumepata wanunuzi, hivyo hakutakuwa na shida tena.
"Tulianza kununua tangu katikati ya mwezi Juni hadi mwishoni mwa mwezi wa Agosti. Malipo yamekwishafanyika kwa Awamu Mbili, wale wa mwezi Juni na Julai wameshalipwa na sasa ni awamu nyingine ambapo Wakulima wote walioleta watamaliziwa malipo yao.
"Bodi inanunua kutoka kwa Wakulima wadogo na wakubwa moja kwa moja lakini kutoka kwenye vikundi vya Wakulima pia, ili kuwa soko la uhakika kwa Wakulima, kama yalivyo malengo ya Bodi hii. Tunashughulikia malipo yao kwasababu tunajua wako waliowezeshwa na Taasisi za Fedha kufanya shughuli zao na wanatakiwa kurejesha.
"Tunawaomba wawe watulivu, muda si mrefu wataona malipo yao, lakini pia Bodi inawashukuru kwa uvumilivu wao na tunaomba Ushirikiano wao kwa siku zijazo."
Pia soma - Wauzaji wa mahindi hatujalipwa pesa zetu tangu mwezi wa 8. Serikali isikie kilio chetu