BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
364
433
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetoa msimamo wake kuhusu masuala ya uraia pacha nchini baada ya hivi karibuni kuwa na mijadala mbalimbali ya uraia pacha.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Agnesta Kaiza leo Bungeni Jijini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema kwamba sheria ya Tanzania hairuhusu uraia wa nchi nyingine kwa watu wazima bali kwa watoto chini ya miaka 18 tu.

"Uraia wa Tanzania unaoongozwa na Sheria ya Uraia sura ya 357 Toleo la mwaka 2002. Sheria hii inabainisha aina tatu tu za uraia wa Tanzania ambao ni Uraia wa kuzaliwa, uraia wa kurithi pamoja na uraia wa tajirisi. Hivyo, kwa mujibu wa Sheria tajwa hapo juu, Serikali hairuhusu Uraia pacha kwa watu wazima isipokuwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 18 ambao wanakuwa na uraia wa Tanzania na uraia wa nchi nyingine." Alisema.

Mbunge Agnesta aliendelea kuhoji kama Sheria sio msahafu kwanini Serikali sasa isije na Muswada wa Sheria ya kuruhusu uraia pacha nchini ambapo Waziri Masauni alisema ni kweli Sheria hizi sio msahafu na kwamba Sheria zote zinatungwa kwa maslahi na matakwa ya watu hivyo Serikali bado haijajiridhisha kama Uraia pacha ni matakwa ya Watanzania walio wengi na kama Serikali ikijiridhisha basi haitaona shida kuja Muswada wa Sheria hiyo.

"Hata kwenye mchakato wa Katiba uliokwama ambao ulihusisha maoni ya wananchi mbalimbali, suala la uraia pacha halikuwa matakwa ya Watanzania walio wengi na ndio maana Serikali ilipendekeza hadhi maalum na sio Uraia pacha kwasababu halikuwa takwa la wananchi walio wengi." Alisema Waziri Masauni.

Waziri Masauni aliongeza kuwa Serikali iko pamoja na Watanzania wote walio Nje na ndio maana kwasasa iko katika hatua za mwisho kabisa kuanzisha hadhi maalum ili kuwapa fursa mbalimbali kwa Watanzania waliochukua uraia wa nchi nyingine.

PIA SOMA
- Tanzania kuanza kutumia Hadhi Maalumu badala ya Uraia Pacha


 
Asilimia kubwa ya sheria zote sio takwa la wananchi, hata sheria inayounda muungano wananchi walio wengi hawataki ndio maana kwenye mchakato ule wa katiba mpya wengi walitaka eidha serikali 3 .
Lakini matakwa ya wanasiasa waliona haifai kwao wakaachana nayo.

Hili swala la uraia pacha ungekuwa unamaslahi ya moja kwa moja kwa wanasiasa siku nyingi lingekuwa limemalizika.
 
Swali gumu majibu rahisi!
Nchi za sub Saharan Africa "logic" itafika wakati Dunia inamalizika!

Ukisema maoni ya walio wengi hawataki uraia pacha swali linakuja je lini kulifanyika kura za maoni kwa raia wote wakaulizwa na walio wengi , ukitaja asilimia, ndo wakasema Hawataki uraia pacha!!

Nchi masikini ngumu sana kuishi! Inaboa sana kuwafanya raia wote ni wajinga!

Bora Waziri angesema hatutaki uraia pacha bongo hauna faida nendeni popote hata Miga mkashtaki, full stop.

Haya majibu dizaini hii yanaboa tangu Niko chekechea hadi Leo jua Linazama Bado wanayo tu bungeni! Mara utasikia kwakuwa kwakuwa kwakuwa kwakuwa milioni inaboa sana! Mara utasikia hili tutalifanyia kazi hadi lini my foot!!

Bunge naomba mshughulikie kwanza report ya CAG!majizi yakamatwe!
 
Yaani bado watunga sera wanafikiri kijima kweli hatuoni faida wenzetu wanazopata kwa raia wao kuwa na uraia wa nchi nyingine faida gani tunapata kwa kuwapoka raia wetu uraia wao wanapoomba uraia wa nchi nyingine tunakuja eti na hadhi maalumu ujima kabsa huu uliopitwa na wakati
 
Iko ni sawa na kikao cha nani ata mfunga paka kengele. Wanakutana kupiga soga, kupoteza muda wajipatie pesa
 
Uraia wa nchi mbili hauna maslahi kwa wananchi wa hali ya chini na ni hatari kwa usalama wa nchi, ina maana mtanzania/ mnyarwanda mtanzania/mkenya mtanzania/ oman etc si la kukimbilia sana suala hili.
 
Halikuwa matakwa ya wananchi wengi"
Kuna sheria nyingi zimepita bila matakwa ya wengi
Uraia pacha ni maslahi ya Taifa pia
Sasa mtu aliepo nchini wala hajui maana ya uraia pacha atakubalije?

Je kuna wangapi wana hata hizo passport?
Tz ni waoga tu
Fekeni kabisa hawa
 
Roho mbaya Yao ya uraia Pacha wameanzia kwenye kupata passport ambalo ni hitajio la msingi hawa watu nusu wachawi kabisa. Eti uraia Pacha Kwa under 18 sasa impact inatoka wapi hapo au ni mianya ya kupeleka vizazi vyao nje Tu.Waeendelee kuibania hiyo haki na siku wakiitoa watakuja watawala wanyama wa National parks maana kundi kubwa litaamka mno na kuona tumecheleshwa na upuuzi wao.
 
Si matakwa, labda yawe matako.. Sheria ngapi wamejipitishia wenyewe tu huko.
Pumbavu kabisa.
 
Back
Top Bottom