maslahi na nyumba za walimu zimetengewa kiasi gani?
Acha siasa, kwa nini asiseme ukweli, na kwa nini afiche ukweli, ukifundisha hizo shule wewe mwenyewe unayefundisha lazima uwe fiti, maana madogo wapo vizuri, wanaelewa, idadi kubwa walioko pale, wanajiweza, kwa kipindi cha nyuma kila baada ya muda Fulani unapewa mtihani na kama utashindwa kufikisha hizo salama H/M anatafuta shule nyingine kwa ajili yakoHii ya mwisho "....pamoja na kuzipa shule hizi walimu wenye vigezo....", kidogo ina ukakasi na binafsi sijaipenda iwapo waziri alitumia lugha ya namna hii.
Kwani walimu wanaokuwa wanafundisha shule ambazo "sio za vipaji maalumu" hawana vigezo?.....Naiona kama ni kauli yenye chembe chembe ya unyanyapaa flani.....
Nadhani angesema tu ".....na kuhakikisha shule hizi zinakuwa na walimu wa kutosha....." ingetosha na kueleweka pasipo maswali kwani moja ya tatizo kubwa la shule za umma nyingi ziwe maalumu au hata hizi zisizo maalumu kwa mtazamo wao ni upungufu wa walimu wa baadhi ya masomo hasa ya sayansi.
Aidha, sisi wote pamoja na serikali yenyewe ambayo ndiyo inaratibu mchakato mzima wa kuandaa walimu, tunaamini kila mwalimu akiajiriwa ktk shule za serikali basi maana yake anakuwa amethibitishwa kuwa ana sifa na vigezo vyote kulingana na level anayopaswa kufundisha mwalimu huyu!!
Hao hata hizi shule walikuwepo sana, ila wana utaratibu wa kupitisha mchujo kwa kuwapa mitihani Mara kwa Mara kupima uwezo, ukishindwa wanakutoa, Nadhani miiko imekiukwa(Shule za private ndo wanaendeleza utaratibu huu), kama ukulifeli hata uwe na pesa kujaza chumba husomiSijui wanamaanisha nini wanavyosema shule za vipaji maalumu. Mimi nilisoma Weruweru cha kushangaza wakati tunaanza form one kuna wanafunzi walikuja na ufaulu wa alama za juu kabisa lakini walikuwa hawajui kusoma wala kuandika.
Kaka upo sahihi ndio mana tunachemka.....Moja ya shule (nadhani) anazozungumzia waziri ni Tabora Schools (Boys & Girls)
Mimi nimesomea Tabora Boys kwa masomo yangu ya A'level miaka ya tisini nikitokea Kibaha S.S nilikomalizia masomo yangu ya sekondari O'level
As for the case ya wanafunzi wenye "vipaji maalumu". Hii dhana kwa Tanzania hata sijawahi kuielewa
Hebu niambie kwa mfano pale Iliboru S.S hivi kuna wanafunzi wenye vipaji maalumu au ni shule tu iliyotengwa kwa wanafunzi walio na ufaulu wa alama za juu bila kujali amefaulu kwa njia gani?.....Kwangu mimi ndicho ninachokiona!!
Ni kwanini hizi shule ziitwe za vipaji maalumu eti? Ni kwa kigezo hiki cha kupata alama za juu ktk masomo yoote?
Hoja yangu ilikuwa ni walimu wenye vigezo. Na kamwe sikuona tofauti ya walimu walionifundisha Kibaha na hawa wa Tabora Boys as a special school!!
Na labda nikuambie kitu kimoja kuwa hakuna cha wanafunzi wenye vipaji maalumu wala nini.
Mimi naamini kuwa wanafunzi woote ktk shule zoote kila mmoja ana kipaji chake!!
Kuna wenye vipaji vya kuimba, kucheza, ubunifu wa kisayansi, mavazi, sanaa za uchoraji nk
Je, shule zetu zimekuwa categorized kwa kuzingatia components za vipaji hivi ili kila mwanafunzi aende ktk shule husika kulingana na kipaji chake?