Serikali yatangaza Kanuni zinazokataza Matumizi ya Fedha za Kigeni kulipia bidhaa au huduma nchini

Jun 26, 2024
23
27
Kufuatia kuongezeka kwa miamala ya fedha za kigeni katika manunuzi ya bidhaa na huduma mbalimbali nchini, Wizara ya Fedha kupitia Sheria ya Benki Kuu, Sura ya 197 imetangaza Kanuni za Matumizi ya Fedha za Kigeni za mwaka 2025. Kanuni hizi zimeanza kutumika rasmi Machi 28, 2025.

Kanuni namba 2 ya Kanuni hizi, inaelekeza kwamba bei zote za bidhaa na huduma nchini zitangazwe kwa shilingi ya Tanzania.

Aidha Kanuni zinaelekeza kwamba mtu yeyote atakayefanya yafuatayo atakua anatenda kosa;
(a) atalazimisha, atashiriki, atasaidia au kuwezesha upangaji bei ya bidhaa au huduma yoyote nchini kwa kutumia fedha ya kigeni;
(b) atanukuu, atatangaza, atabainisha au kuchapisha bei ya bidhaa au huduma yoyote nchini kwa kutumia fedha ya kigeni;
(c) atalazimisha au kuwezesha malipo ya bidhaa au huduma yoyote nchini kufanyika kwa kutumia fedha ya kigeni;
(d) atakataa bidhaa au huduma yoyote nchini kulipiwa kwa kutumia shilingi ya Tanzania; au
(e) atapokea malipo ya bidhaa au huduma ndani ya nchi kwa kutumia fedha ya kigeni.

1743270559636.png


Pia Kanuni zinakataza mtu yeyote kuingia katika mkataba wa bidhaa au huduma kwa malipo ya fedha ya kigeni ndani ya nchi isipokua kwa mikataba kadhaa.

Kufuatia hilo, Kanuni zimetoa muda wa mwaka mmoja kwa watu na makampuni kurekebisha mikataba yote ya utoaji wa bidhaa au huduma iliyosainiwa kabla ya Kanuni hizi kuanza kutumika ambayo imeelekeza malipo kwa fedha za kigeni. Endapo haitafanyiwa marekebisho ndani ya mwaka mmoja tangu tarehe 28, machi 2025, mikataba hiyo itakuwa batili.

Ikumbukwe kwamba bidhaa na huduma hizo ni pamoja na kuuza au kupangisha nyumba, viwanja na ofisi, ada za shule, pamoja na malipo na ushauri.

Miamala inayoruhusiwa kutozwa kwa fedha za kigeni ni kama ifuatayo;
  • Michango ya uanachama inayolipwa na Serikali kwa taasisi za kikanda zilizopo nchini
  • Miamala inahusisha Balozi na mashirika ya kimataifa yaliyopo nchini
  • Mikopo ya fedha za kigeni inayotolewa na benki za biashara na taasisi za fedha zilizopo nchini
  • Malipo ya bidhaa katika maduka yasiyotoza ushuru
 

Attachments

  • GN_NO_198_OF_2025_KANUNI_ZA_MATUMIZI_YA_FEDHA_ZA_KIGENI_ZA_MWAKA.pdf
    193.4 KB · Views: 3
Kutokana Na Kuporomoka Kwa Thamani ya Shilingi siku hadi siku Tanzania Imeamua Kudhibiti matumizi ya Fedha za Kigeni na Raia yoyote au Mgeni Akiwa Nchini Kwetu itamlazimu Kutumia Shilingi ya Tanzania Kwenye Kununua Bidhaa Au Huduma..

Sheria hiyo Iliyosainiwa Na Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba Jana Tarehe 28/03/2025..Imeanza Rasmi kutumika Baada ya Kanuni zake Kutungwa Leo hi..

Hivi hapa Ni Baadhi ya Masharti ya Kanuni ya Sheria Hiyo..

KANUNI ZA MATUMIZI YA FEDHA ZA KIGENI ZA MWAKA 2025: KWA KIFUPI.

1. Mtu anapaswa kufanya muamala ndani ya nchi kwa kutumia shilingi ya Tanzania pekee.

2. Mtu anatenda kosa endapo atafanya yafuatayo:-

- Atalazimisha, atashiriki, atasaidia au kuwezesha upangaji bei ya bidhaa au huduma yoyote nchini kwa kutumia fedha ya kigeni.

- Atanukuu, atatangaza, atabainisha au kuchapisha bei ya bidhaa au huduma yoyote nchini kwa kutumia fedha ya kigeni.

- Atalazimisha au kuwezesha malipo ya bidhaa au huduma yoyote nchini kufanyika kwa kutumia fedha ya kigeni.

- Atakataa bidhaa au huduma yoyote nchini kulipiwa kwa kutumia shilingi ya Tanzania.

- Atapokea malipo ya bidhaa au huduma ndani ya nchi kwa kutumia fedha ya kigeni.

3. Mtu yeyote hataruhusiwa kuingia mkataba wa bidhaa au huduma kwa malipo ya fedha ya kigeni ndani ya nchi, isipokuwa kwa mkataba unaohusisha malipo yaliyoruhusiwa kwa mujibu wa masharti ya kanuni ya 4.

4. Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1)(a) malipo kwa ajili ya wafanyakazi, huduma au bidhaa zitakazonunuliwa nchini wakati wa utekelezaji wa mkataba yatafanyika kwa kutumia shilingi ya Tanzania, isipokuwa kwa mikataba itakayoruhusiwa kwa mujibu wa kanuni ya 4;

- (b) mkataba wowote wa utoaji wa bidhaa au huduma ndani ya nchi ulioingiwa kwa fedha ya kigeni kabla ya kuanza kutumika kwa Kanuni hizi utapaswa kufanyiwa marekebisho ndani ya muda wa mwaka mmoja tangu tarehe ya kutangazwa kwa Kanuni hizi.

- (3) Mkataba ambao hautafanyiwa marekebisho ndani ya muda ulioainishwa katika kanuni ndogo ya (2)(b) utakuwa batili isipokuwa pale ambapo Waziri atatoa idhini ya kuongeza muda usiozidi muda wa mkataba ulioingiwa.

NA Hii ndo kanuni yenyewe Kanuni Namba 198 ya Mwaka 2025 Kanuni ya Matumizi ya Fedha za Kigeni..
inayotokana na Sheria namba 197 ya Mwaka 2025, Sheria ya benki Benki kuu ya Tanzania..
 

Attachments

  • GN NO. 198 OF 2025 - KANUNI ZA MATUMIZI YA FEDHA ZA KIGENI ZA MWAKA 2025.pdf
    193.4 KB · Views: 3
Ujue hii rahisi sana, hii mtu anachofanya ni kuangalia rate ya siku husika na kubadilisha kuwa Tzs, maana yake bado mtu atatozwa kwa Tzs ila in USD
 
Naomba wana uchumi wanisaidie kuwa hii itasaidia shilingi ya Tz kupanda dhidi ya Dola? Au hii pia inaweza kusaidia kupunguza kukosekana kwa dola nchini?
 
Kwa kufanya hivyo thamani ya shilingi itapanda?

Kwanini timu y wataalamu isiende japani kuchukua ujuzi wa namna ya ku control shilingi? Unatunga sheria na kanuni zake wakati mambo yanayo sisimua uchumi au tuseme mambo yatakayo fanya shilingi ipande thamani hayapo au tuseme ni yaleyale yaliyo iporomosha?
 
1. Mtu anapaswa kufanya muamala ndani ya nchi kwa kutumia shilingi ya Tanzania pekee.

2. Mtu anatenda kosa endapo atafanya yafuatayo:-

- Atalazimisha, atashiriki, atasaidia au kuwezesha upangaji bei ya bidhaa au huduma yoyote nchini kwa kutumia fedha ya kigeni.

- Atanukuu, atatangaza, atabainisha au kuchapisha bei ya bidhaa au huduma yoyote nchini kwa kutumia fedha ya kigeni.
Will it apply to all equally? Hata kwa Abduli? Riz1?
 
Naomba kuuliza kitu!?
Je hizi sheria ni kwa watanzania pekee au mpaka viongozi (including Rais Samia na wateule wake?)
Je ni Tanganyika ama pamoja na Zanzibar?
 
Kwa nini wasiende cashless, watoe Kodi kwenye lipa kwa mpesa watu walipe kwa simu. Utaona kama watu hawatazitafuta tsh
 
Back
Top Bottom