Ndo maana
Nguruvi3 hapa kila siku anahubiri mfumo
tuwe na mfumo unaowajibisha watu bila kusubiri Rais aseme
manake kwa haya mambo yalivyo mengi huyo Magufuli wataanza kumlaumu bure tu..
haya mambo yawe kwenye mfumo tu
Mkuu taratibu wataelewa, wamegoma kata kata, hawasikii hawaelewi. Jiulize, hivi kampuni hiyo ilikuwa inalipa kodi kweli.
Hapa kungalikuwa na uhusiano mkubwa sana kati ya serikali(kijiji, wilaya na mkoa) serikali kuu kupiitia BRELA na TRA. Haya yasingeweza kutokea
Wenzetu wa mataifa yanayojali na yenye mfumo, yaani ile status yako tu katika nchi inaeleza kila kitu
Ukiwa na visitor's visa, permanent resident, green card, citizenship etc' hivyo vinakupeleka mahali husika bila kupenda.
Ukiomba kazi utaulizwa status kama una work permit. Ukitaka ku invest utaulizwa status , ukitaka kusoma pale unapokwenda kusoma tu kutaeleza kila kitu.
Halafu kuna link kati ya vyombo hivyo, kwamba lazima uwe na social insurance itakayoamua matibabu na kodi yako. Mwajiri anaweza kukushutukia kwa jambo rahisi, namba yako ya social insurance haikubaliki na kampuni inayotoa insurance. Hapo kila timbwili litakuwa wazi hata kama ni fundi wa kufoji kiasi gani
Mzunguko huo hauwezi kutoa nafasi ya mtu kuja kuchimba kitu katika nchi za wenzetu bila kujulikana
Yaani the local authority tu ya kijiji inatosha kujua huyu ni mwekezaji yule ni mwizi
Hatuna mfumo wa namna hiyo, watu wanaingia wanafanya watakavyo
Vyombo havifanyi kazi kwa ushirikiano, tunasubiri single ipakuluwe tuanza kughani makoo yakikauka
Tukisema wanatutia vigagula, wanasema tuna paranoia na mfumo.
Wanachukia kwasababu tunahoji kwanini tufunge manyanga na njuga tukizungusha makalio left to right kwa mirindimo ya Hapamzigo ikiwa tunaona tatizo?