Sibonike
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 17,295
- 18,029
Sina sababu ya kumtetea Mwakyembe lakini itoshe kusema ilikuwa ni kazi ya waziri mwenye dhamana ya madini.Nilikuwa nashangaa kusikia wasichana wa Nigeria walivyofichwa na Boko Haram, kumbe hata kwetu inawezekana. Lakini naamini kabisa kwamba baadhi ya wabunge sasa wanaifanya maliasili ya nchi kama miradi yao binafsi. Mwakyembe hakujua? halafu nimesikia pia hata Ludewa kulikuwa na WAchina wakifanya hayo hayo! Huko nako marehemu Filikunjombe hakujua?
Kuna trend ya aina moja ktk maeneo haya na yaweza kuwa kweli kwamba ile mirahaba ya madini ni midogo kwa kuwa sehemu ya pesa hizo viongozi wetu wanalipwa ktk akaunti zao binafsi. Mabutu-like.
Waziri ku query issue za wizara nyingine si rahisi.