Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,583
- 13,270
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amezindua Shule mpya ya Sekondari ya Yombo iliyojengwa katika Kata ya Ikuna Wilaya Njombe, Mkoani Njombe
Akizungumza Oktoba 03,2024 katika Kata ya Ikuna baada ya kuzindua shule hiyo Prof. Mkenda amesema kuwa Serikali inaendelea kuwekeza kwenye sekta ya elimu kwa kiasi kikubwa ili watoto wa kitanzania wapate elimu katika mazingira bora na kuwajengea ujuzi.
"Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuhakikisha vitabu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia vya kisasa pamoja na kuboresha mazingira ya walimu"amesisitiza Prof. Mkenda
Aidha, ameongeza kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatenga fedha kwa kila mwaka kwa ajili ya kutoa mafunzo kazini kwa walimu ili kuwawezesha kupata fursa za kujadiliana na kubadilishana uzoefu na kujadiliana mambo mbalimbali ya kuinua elimu nchini.
Mbunge wa Jimbo la Lupembe Enock Swale amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha maendeleo yanawafikia mpaka watu wa chini kabisa.
Mbunge huyo ameongeza kuwa katika jimbo hilo lenye Kata 12 lakini mpaka sasa lina Shule 13 za Kata mpya na kuongeza kuwa kazi za Mhe. Samia Suluhu Hassan zinajionyesha.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyombo Anastazia Nchemwa amesema kuwa shule ina wanafunzi 139 wa kidato cha kwanza na kwamba zaidi ya shilingi Milioni 583 zimetumika katika ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo.
Mwalimu Nchemwa ameongeza kuwa tayari serikali imeshawapatia vitabu kwa ajili ya ujifunzaji na ufundishaji na kwamba jumla ya shilingi Milioni 100 imeshawekwa katika akaunti ya shule kwa ajili ya ujenzi wa nyumba pacha ya walimu.
Kupitia mradi wa SEQUIP Serikali pamoja kazi nyingine inajemga shule za sekondari za kata 1000 ili kusogeza huduma hiyo karibu na Wananchi.
Kati ya hiyo tayari imeshajenga shule 760 zimekamilika na kuanza.