Serikali yasalimu amri kwa Bank binafsi, Akaunti zake kutohamishiwa BoT

Mimi ninachojua makusanyo yote yataenda hazina kabla ya idhini ya matumizi...huu uandishi ni wa waandishi makanjanja...Serikali ya Magufuli sii ya mchezo...ninapoongea hapa hadi malipo ya sh 10000 yatapitia benki
Jingalaooo. Huna tofauti na wakukurupuka.
 
Hiki kitu nilikitegemea kabisa kwa sababu serikal ikiondoa fedha zake kwenye ma benki ya biashara kutakuwa na uhaba wa deposit kwenye hizo benki hivyo fedha za kukopesha kutakuwa hamna na ambacho kingefuata ni discourage of lending, mikopo ingetolewa kwa watu wachache na kampuni zenye high profile pamoja na low risk na rate ingekuwa kubwa kwa sababu ya discourage of lending kwa vyovyote vile rate isingeweza kushuka namshangaa hata kimei alieunga mkono na kusema eti rate itapungua
 
Nina wasiwasi sana na hii habari. Maana jana waziri wa fedha ameongelea uamuzi huu. Leo unakanushwa kirahisi tu
 
MIZUKA ISHAIPANDA...
Waziri wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI, utumishi na Utawala bora, Yupo serkali gani..????
Hivi hii serkali haina coordination au kila wizara ina MZUKA wake...???

Tusubirie next MKURUPUKO....
 
Mkuu hii ni Serikali ya Majipu unatarajia nini hapo zaidi ya harufu ya Usaa!!
 
Wiki moja baada ya Serikali kutangaza kuchukua hatua za kupunguza riba za mabenki kwa wananchi kwa kuagiza akaunti za mashirika na taasisi zake katika mabenki ya kibiashara zifungwe na kuhamisha fedha zilizopo katika akaunti hizo kwenda Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Sasa imegonga mwamba.

Waziri wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI, utumishi na Utawala bora, George Simbachawene amesema huo mpango wa kuhamisha akaunti za mashirika na taasisi za Serikali umetolewa kimakosa.

Hata waziri wa Fedha na Mipango ameshafanyia marekebisho swala hilo kwenye mapendekezo Ya mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 uliouwasirisha Bungeni.

Agizo hilo lilitolewa na Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru hivi karibuni, akiwataka watendaji wakuu wote wa mashirika na taasisi hizo, kufuata maelekezo matano ya kufunga akaunti zao katika mabenki ya biashara na kuhamishia fedha hizo BoT.

Hatua hiyo iliungwa mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei ambaye majuzi aliongea na vyombo vya habari na kusema "tunafikiri maamuzi hayo hayana athari zozote kwani nchi mbalimbali zimekuwa zikitumia mfumo huo ikiwemo Uganda, Rwanda na Kenya ila kwa kwetu unaonekana mgeni kutokana na kutotumika kwa muda mrefu" alisema.

Sasa nashangaa leo Serikali kuachana na mpango huo uliokuwa na manufaa kwa Nchi.
hii misinformation siamini kama serikali imebadilisha uamuzi mzuri baada ya kukaa na bepari kimei.
 
Hiki kitu nilikitegemea kabisa kwa sababu serikal ikiondoa fedha zake kwenye ma benki ya biashara kutakuwa na uhaba wa deposit kwenye hizo benki hivyo fedha za kukopesha kutakuwa hamna na ambacho kingefuata ni discourage of lending, mikopo ingetolewa kwa watu wachache na kampuni zenye high profile pamoja na low risk na rate ingekuwa kubwa kwa sababu ya discourage of lending kwa vyovyote vile rate isingeweza kushuka namshangaa hata kimei alieunga mkono na kusema eti rate itapungua
Mbona sasa rate iko juu sana ilihali account za serikali ziko huko? Ina maana zikitolewa rates zitakuwa mara mbili au zaidi ya sasa au?
Ninavyoona BOT itakuwa na hela nu=yingi , itakopesha mabaenki kwa low rate na nayo mabenk itabidi wapunguze rates kwa mwongozo wa BOT
 
Wiki moja baada ya Serikali kutangaza kuchukua hatua za kupunguza riba za mabenki kwa wananchi kwa kuagiza akaunti za mashirika na taasisi zake katika mabenki ya kibiashara zifungwe na kuhamisha fedha zilizopo katika akaunti hizo kwenda Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Sasa imegonga mwamba.

Waziri wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI, utumishi na Utawala bora, George Simbachawene amesema huo mpango wa kuhamisha akaunti za mashirika na taasisi za Serikali umetolewa kimakosa.

Hata waziri wa Fedha na Mipango ameshafanyia marekebisho swala hilo kwenye mapendekezo Ya mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 uliouwasirisha Bungeni.

Agizo hilo lilitolewa na Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru hivi karibuni, akiwataka watendaji wakuu wote wa mashirika na taasisi hizo, kufuata maelekezo matano ya kufunga akaunti zao katika mabenki ya biashara na kuhamishia fedha hizo BoT.

Hatua hiyo iliungwa mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei ambaye majuzi aliongea na vyombo vya habari na kusema "tunafikiri maamuzi hayo hayana athari zozote kwani nchi mbalimbali zimekuwa zikitumia mfumo huo ikiwemo Uganda, Rwanda na Kenya ila kwa kwetu unaonekana mgeni kutokana na kutotumika kwa muda mrefu" alisema.

Sasa nashangaa leo Serikali kuachana na mpango huo uliokuwa na manufaa kwa Nchi.
Source
 
Hii serikali ya awamu ya 5 naanza kuidharau sasa.Hapo mafisadi wamesha lobby.Huo mpango ulikua mzuri sana hata mfumuko wa bei ungeshuka
 
Back
Top Bottom